50 Bing Coupons

  • Subscribe to our RSS feed.
  • Twitter
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • Facebook
  • Digg

Tuesday, 1 October 2013

MAALIM SEIF AKUTANA NA VIONGOZI WA CHAMA CHA WALIMU ZANZIBAR

Posted on 02:54 by Unknown
 
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na viongozi wa Chama Cha Walimu Zanzibar (ZATU), Ofisini kwake Migombani.
  Rais wa Chama Cha Walimu Zanzibar (ZATU), Salim Kitwana Sururu (kushoto), akiwasilisha maoni ya chama hicho kwa Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, Ofisini kwake Migombani.
Baadhi ya viongozi wa Chama Cha Walimu Zanzibar (ZATU), walimsikiliza Maalim Seif, walipokutana nae Ofisini kwake Migombani. (Picha na Salmin Said, OMKR).
=====   =======  =========
Chama Cha Walimu Zanzibar (ZATU), kimepongezwa kutokana na uvumilivu walionao katika kutafuta njia muafaka za kutatua kero zinazowakabili.
 
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, ametoa pongezi hizo Ofisini kwake Migombani, wakati akizungumza na viongozi wa  Chama hicho wakiongozwa na Rais wa ZATU, Salim Kitwana Sururu.
 
Amesema takriban nchi zote za Afrika Mashariki zimekuwa zikikumbwa na migogoro kati ya serikali na vyama vya walimu, lakini ni jambo la kufurahisha kuona Chama Cha Walimu Zanzibar hakiingi katika migogoro hiyo na badala yake kimekuwa kikitumia njia za Kidiplomasia katika kutatua kero zake.
 
Amekitaka Chama hicho kuendeleza moyo huo, kwani njia bora ya kutatua mizozo ni mazungumzo, na wala sio malumbano au migomo.
Amefahamisha kuwa uzoefu unaonesha kuwa mara nyingi inapotokea migomo ya walimu linaloathirika ni Taifa na vijana, na kwamba hakuna haja ya kushiriki au kushabikia malumbano ya aina hiyo. 
 
Ameeleza kuwa Serikali kwa upande wake iko tayari kukutana na wadau mbali mbali kujadiliana juu ya kero zinazowakabili, ili kutafuta njia ya kuzitatua kwa njia ya amani bila ya kuwepo malumbano.“Hakuna lisilozungumzika, na mimi nasema njia muafaka ya kutatua kero za namna hiyo ni mazungumzo. Kwa hivyo endeleeni na moyo huo huo na bila ya shaka kero zenu zitatatuka”, alisema Maalim Seif kuwambia wakuu wa ZATU.
 
Kwa upande wake Rais wa Chama Cha Walimu Zanzibar (ZATU), Salim Kitwana Sururu, amesema ni heshima kubwa kwa Zanzibar kutokumbwa na migomo ya walimu ambayo imekuwa ikijitokeza katika nchi jirani mara kwa mara.Ameahidi kuwa ZATU kitaendelea kutumia njia za mazungumzo katika kutatua kero zinazowakabili, na kwamba kitafanya hivyo ili kulinda heshima ya Zanzibar.
 
Naye Katibu Mkuu wa Chama hicho Mussa Omar Tafurwa, ameiomba Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kuitekeleza kikamilifu Sera ya Elimu Zanzibar, ili kuleta maendeleo yaliyokusudiwa katika sekta ya elimu.
 
Amefahamisha kuwa bado yapo mambo mengi ambayo hayajatekelezwa ndani ya sera ya elimu ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa Mamlaka ya uajiri wa walimu, pamoja na Baraza la Walimu Zanzibar, mambo ambayo yanapaswa kufanyiwa kazi.
Email ThisBlogThis!Share to XShare to Facebook
Posted in | No comments
Newer Post Older Post Home

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to: Post Comments (Atom)

Popular Posts

  • tamasha la 32 la sanaa la bagamoyo lawasha moto, Mhe Makala asema utamaduni ni ajira kwa vijana
    NAIBU Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Mhe. Amos Makala amesema Sanaa na Utamaduni nchini itaendelea kuenziwa ili kuwaleta a...
  • WAZIRI DK. NCHIMBI AMTEMBELEA PADRI ALIYEMWAGIWA TINDIKALI HOSPITALI YA MUHIMBILI LEO
    Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akisalimiana na Padri Joseph Monesmo Magamba wa Kanisa la Romani Katoliki Pa...
  • wadau farida na paul wameremeta
     Wakila pozi baada ya kumeremeta katika Kanisa la Mtakatifu Petro jijini Dar es salaam kabla ya kwenda kwenye mnuso wao wa nguvu katika hote...
  • RAIS KIKWETE ATUNUKIWA SHAHADA YA UZAMIVU YA CHUO KIKUU CHA GUELPH JIMBONI ONTARIO, CANADA
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mheshimiwa ...
  • GLOBAL LANGUAGE NETWORK (GLN) ILIYOFANYIKA WASHINGTON, DC YAFANA
    Katibu wa Jumuiya ya Tanzania akielezea nini maana ya GLN na kwanini Jumuiya ya Tanzania DMV ni moja ya washiririki  Banda la Tanzania lilki...
  • ACCT members attending Master Builders South Africa Congres 2013
    Basically ACCT members were invited by CIDB Construction Industry Development Board South Africa to attend at 2 days congress here in Joanes...
  • KANISA LA TGMIT LAFANYA IBADA MAALUMU KUIOMBEA AMANI TANZANIA
     Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akishiriki kuwasha mshumaa kama tendo la kuiangaza nchi ya Tanzania.  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape ...
  • TAARIFA YA MSIBA WA MAMA ROSE HEINRICH SANGIWA MATAJI
    Familia ya Marehemu Chief Shaaban Mtengeti II, inasikitika kutangaza kifo cha shangazi yao mpendwa  Mama Rose Heinrich Sangiwa Mataji, mama ...
  • MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR MAALIM SEIF SHARIFF HAMAD AWASILI MKOANI RUKWA KUSHIRIKI IJITIMAI YA KIMATAIFA
    Makamu wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad akilakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya a...
  • Timu ya Taifa ya Pool yaanza kujifua huko Mkoani Morogoro
    Kocha wa Timu ya Taifa, Denis Lungu (kulia) akiwaelekeza jambo wachezaji wa timu ya Taifa ya mchezo wa Pool (Safari National Pool team) wak...

Blog Archive

  • ▼  2013 (500)
    • ▼  October (22)
      • barabara ya Mtoni-mbagala ilivyo
      • Tanzania katika hatua za muhimu za kuanza utekekel...
      • washindi wa chemsha bongo wapatikana
      • mtuhumiwa wa mauaji auawa na wananchi makete
      • UTAFITI WAONESHA KIFUA KIKUU(TB) KUSUMBUA VIJIJINI...
      • Dar lauded for KILIMO KWANZA (Agriculture First) I...
      • PEMBE ZA NDOVU, UGAIDI NI VITA YA KIMATAIFA: KIKWETE
      • President Obama Delivers a Statement on the Govern...
      • Kali TV: This week, meet Nazizi Hirji
      • Lindi na Mtwara wapata washirika kutoka Norway
      • President Kikwete congratulates Nigeria on achievi...
      • Mvua yakata barabara kijiji cha Ndungu Wilayani Same
      • KONGAMANO LA JUMUIYA YA WAZEE WASTAAFU,WAKULIMA NA...
      • Rais Dk.Shein akutana na Balozi wa Uholanzi na Bal...
      • Balozi wa Marekani aiaga Wizara ya Mambo Ndani ya ...
      • MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI KILELE CHA MAAD...
      • SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR YAWATAHADHARISHA...
      • TAARIFA MBALIMBALI ZA MICHEZO KUTOKA KWA SHIRIKISH...
      • MAALIM SEIF AKUTANA NA VIONGOZI WA CHAMA CHA WALIM...
      • KIJIWE CHA UGHAIBUNI
      • TASWIRA HALISI YA MJI WA DUBAI ASUBUHI YA LEO.
      • Here is CPwaa's New Hit Single "Chereko Chereko"
    • ►  September (478)
Powered by Blogger.

About Me

Unknown
View my complete profile