Washindi wanne kati ya watano waliohitajika wa Chemsha Bongo ya kueleza tairi hili lilivyowekwa hapo wamepatikana baada ya wote kutaja kwa usahihi kwamba upande mmoja (usioonekana) wa hilo tairi ulikatwa kabla ya kuvishwa shinani.
Wadau wengi walijaribu (nasi tumewashukuru kwa kujaribu) na tunawapongeza sana, japo walikosea kusema kuwa tairi liliwekwa hapo tokea mti ukiwa mdogo. Ahsanteni wote kwa kushiriki.
Washindi wetu ni: Frank Msillu,
Waheed Humoud, na amina Anita Daudi.
Tunaomba wadau mlioshinda mtupe anuani zenu kwa njia ile ile mliyojibia swali ili tufanye mipango kuwapatia zawadi za T-shirt za Michuzi Blog 2014 mara tu zitapokuwa tayari.
Huu ni mwanzo tu wa michezo ya Globu ya Jamii ambayo imepania kutoa zawadi za hizo T-shirt kwa wadau mara kwa mara. Hivyo kaeni chonjo...
0 comments:
Post a Comment