Tuesday 1 October 2013
Tanzania katika hatua za muhimu za kuanza utekekelzaji wa mradi wa "Single Window System"
Posted on 14:14 by Unknown
Mkurugenzi wa TEKNOHAMA (ICT) wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Ndg. Phares Magesa (kulia) akiongoza ujumbe wa TPA kwenye teleconference na Trade Mark East Africa(TMEA) katikati ni Ndg. Mark wa TMEA na Ndg. Alfred wa TPA .... Tanzania iko katika hatua muhimu ya utekelezaji wa mradi wa "electronic Single Window System" mradi huu utasaidia kuharakisha na kurahisisha mfumo wa mzima wa ufanyaji biashara ya uagizaji(import) na usafirishaji(export) wa bidhaa nje ya nchi.
washindi wa chemsha bongo wapatikana
Posted on 13:30 by Unknown
Washindi wanne kati ya watano waliohitajika wa Chemsha Bongo ya kueleza tairi hili lilivyowekwa hapo wamepatikana baada ya wote kutaja kwa usahihi kwamba upande mmoja (usioonekana) wa hilo tairi ulikatwa kabla ya kuvishwa shinani.
Wadau wengi walijaribu (nasi tumewashukuru kwa kujaribu) na tunawapongeza sana, japo walikosea kusema kuwa tairi liliwekwa hapo tokea mti ukiwa mdogo. Ahsanteni wote kwa kushiriki.
Washindi wetu ni: Frank Msillu,
Waheed Humoud, na amina Anita Daudi.
Tunaomba wadau mlioshinda mtupe anuani zenu kwa njia ile ile mliyojibia swali ili tufanye mipango kuwapatia zawadi za T-shirt za Michuzi Blog 2014 mara tu zitapokuwa tayari.
Huu ni mwanzo tu wa michezo ya Globu ya Jamii ambayo imepania kutoa zawadi za hizo T-shirt kwa wadau mara kwa mara. Hivyo kaeni chonjo...
mtuhumiwa wa mauaji auawa na wananchi makete
Posted on 13:09 by Unknown
Na Edwin Moshi, Makete
Katika hali isiyo ya kawaida wananchi wanaodhaniwa kuwa ni wa kijiji cha Usagatikwa kata ya Tandala wilaya ya Makete mkoani Njombe wameamua kuchukua sheria mkononi kwa kumpiga hadi kumuua Bw. Festo Sigala(44) kwa tuhuma za mauaji
Tukio hilo limetokea Septemba 29 mwaka huu katika kijiji cha Tandala wilayani hapo, baada ya wananchi hao kumfuata mtuhumiwa huyo kwa lengo la kumdhuru kutokana na tuhuma za mauaji ya mwananmke aliyetambulika kwa jina la Furaha Datovu Sanga(37)
Akithibitisha hilo ofisini kwake Mkuu wa polisi(OCD) wilaya ya Makete Alfred Kasonde (Pichani) amesema Bw. Nesco Thobias Chaula mkazi wa kijiji cha Usagatikwa aligundua kupatikana kwa mwili wa marehemu Furaha ambaye aliripotiwa kupotea tangu Mei 15 mwaka huu ambapo alitafutwa bila mafanikio ambapo mwili huo wa marehemu ulikutwa ndani ya choo cha shimo kinachomilikiwa na Festo Sigala ambaye kwa sasa ni marehemu
Amesema baada ya hapo wananchi waliamua kumsaka mtuhumiwa huyo ambapo walimkuta eneo la stendi ya mabasi katika kijiji jirani cha Tandala wakati akijaribu kutoroka baada ya kupata taarifa kuwa wamegundua kama alifanya mauaji, na wakaanza kumpa kipigo
"Walimkuta stendi huyo mtuhumiwa akiwa anataka kutoroka baada ya kujua kuwa anatuhumiwa kwa mauaji na mwili wa marehemu ulikutwa kwenye choo chake na wakaanza kumpiga kwa mawe, fimbo wakati alipotaka kutoroka eneo hilo" alisema Kasonde
Kufuatia kipigo cha wananchi hao kuwa kikali, mtuhumiwa huyo aliamua kutimua mbio kuelekea kituo cha polisi Tandala kwa lengo la kujisalimisha, lakini wananchi hao waliendelea kumfukuza na wakafanikiwa kumzingira na kuendelea kumshambulia kwa kipigo hasa maeneo ya kichwani amapo ubongo na damu vilimwagika kwa vingi hadi alipofariki dunia kabla hajafika kwenye kituo cha polisi
Amesema kutokana na wingi wa wananchi hao walioamua kujichukulia sheria mkononi, polisi waliokuwa kazini katika kituo hicho walizidiwa nguvu na kundi hilo la watu hivyo kushindwa kumnusuru mtuhumiwa huyo asiuawe kwani nguvu ya wananchi ilikuwa ni kubwa
hata hivyo baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamedai kuwa marehemu huyo aliuawa akiwa ndani ya kituo hicho cha Polisi baada ya wananchi kuwazidi nguvu polisi na kuvinja chumba alichokuwepo marehemu, lakini suala hilo limekanushwa na OCD Kasonde na kusema kuwa kituo hicho kipo salama na wala marehemu hakuuawa kwenye kituo cha polisi
"Hakuna ukweli wowote wa taarifa kuwa ameuawa akiwa lokapu ya kituo cha polisi Tandala, hakuna kituo kilichovunjwa na badala yake wananchi wenye hasira kali ndio waliomuua wakati akikimbilia polisi kunusuru maisha yake" alisema OCD Kasonde
Katika hatua nyingine ameiomba jamii kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwani ni kosa kisheria na badala yake wakimkamata mtuhumiwa wanatakiwa kumfikisha polisi ili sheria ichukuliwe
hadi sasa hakuna anayeshikiliwa kuhusiana na mauaji hayo na uchunguzi bado unaendelea
UTAFITI WAONESHA KIFUA KIKUU(TB) KUSUMBUA VIJIJINI ZAIDI UKILINGANISHA NA MIJINI
Posted on 12:52 by Unknown
Mtoa mada na Mtafiti wa Ugonjwa wa Kifua Kikuu(TB)Dr Said Egwaga akizungumza na waandishi wa habari leo katika Hoteli ya Ngurdoto mkoani Arusha juu ya utafiti walioufanya mwaka 2011 katika wilaya 62 nchini ulibaini kati ya watu Laki moja kuna wagonjwa wa Kifua Kikuu 295 na waliothirika zaidi ni wanaume ukilinganisha na wanawake na idadi kubwa iko maeneo ya Vijijini ukilinganisha na mijini tofauti na walivyotarajia.
Mratibu wa Magonjwa yasiyopewa Kipaumbele nchini.Dr Upendo Mwingira akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika mkutano wa Kimataifa cha taasisi za afya za jamii unaofanyika mkoani Arusha.
Wataalamu wakifatilia mada zilizokua zikiwasilishwa na mabingwa wa tafiti za magonjwa ya binadamu leo
Wataalamu wakifuatilia mada zilizokua zikiwasilishwa na mabingwa wa tafiti za magonjwa ya binadamu leo.
Dar lauded for KILIMO KWANZA (Agriculture First) Initiatives
Posted on 12:50 by Unknown
United States journalists who had paid a courtesy visit to the Honorable Minister Eng. Christopher Chiza. The 15 US journalists are in the country from September 29 to October 9, 2013 through the John Hopkins International Reporting Project, funded by the Bill and Melinda Gates Foundation. The Bill and Melinda Gates Foundation had been devoting most of its time and resources to support any efforts aimed at transforming Africa from poverty eradication through its agriculture sector.
Listening on is Dr. Mary Shetto, Head of the Interim Ministerial Delivery Unit under Big Results Now Initiative. Dr. Shetto is also the Coordinator for SAGCOT.
Also in attendance is Mr. Frank Mhina (left), Foreign Service Officer in the Ministry of Foreign Affairs, Mr. Job Mika (center), Private Assistant to Hon. Eng. Chiza and Mr. Erick Kabendera, Freelance Journalist.
Hon. Eng. Christopher Chiza (MP), Minister for Agriculture, Food Security and Cooperatives explains about SAGCOT and Kilimo Kwanza initiatives.
Part of the US team of journalists during the meeting.
By TAGIE DAISY MWAKAWAGO
The Minister for Agriculture, Food Security and Cooperatives, Eng. Christopher Chiza (MP), said that Tanzania is first an agricultural-country, placing Southern corridor strategically as a starting point in yielding resources for the country’s economy.
The Minister said earlier today when he was speaking with the 15 journalists from the United States of America, who are in the country to learn more about agriculture sector and food security initiatives.
The journalists have selected Tanzania for an in-depth fact-finding mission because of its notable record on agriculture, food security and scaling-up nutrition initiatives. “We want to learn more about the success of SAGCOT and Kilimo Kwanza,” said Ms. Alexandra Frank, Project Manager from the John Hopkins University, where the group is enrolled in an International Reporting Project (IRP) in Washington DC.
During their discussion, Hon. Eng. Chiza said that the country is blessed with water resources, but still needs a contribution of about 25 percent of agricultural irrigation to self-sustain its economy.
“Our Government has initiated Big Results Now (BRN) which targets an increase of over 100,000 tons of maize and 250,000 tons of sugar and 190,000 tons of rice, all to be added to the national basket through combination of irrigation and improvement of agricultural marketing systems in the coming two years,” said the Minister.
When posed with question about Kilimo Kwanza and how Tanzania has been able to materialize on agriculture sector, Eng. Minister Chiza said that the Government had initiated the Southern Agricultural Growth Corridor of Tanzania (SAGCOT), as part of implementing Kilimo Kwanza initiative which encompasses broader aspect of green revolution and economic development of the country.
“We are trying to bring in large scale farmers to co-exist with the small scale farmers,” said Minister Chiza, adding that the Government wants the SAGCOT model to be the future replica for other corridors in the countries. The current Southern corridor includes Mbeya, Iringa, Njombe, Dar es Salaam, Morogoro, Coast, Rukwa and Ruvuma Region.
The Minister further said that the country’s investment targets its own agriculture production and productivity, and as such, the Government has allocated 10 percent of its National Budget to the agriculture sector, however, its current allocation figure surges steadily at an 8 percent, noted the Minister. The allocation derived from the implementation of the Maputo Declaration which was reached by the heads of state and government of the African Union (AU) at its second ordinary session held between July 10 and 12, 2013 whereby member-states agreed to allocate at least 10 percent of their national budgetary resources to agriculture.
Discussing the success story of the Kilombero rice plantation in Morogoro, Minister Chiza cited statistics of maize production which had increased for some smallholder farmers from 1.5 to 4.5 tons per hectare, while the yields for rice have increased from 2.5 to 6.5 tons per hectare in the target areas.
As for young generation, Minister Chiza said that the Government has put in place a Youth in Agriculture program, which targets young people who are “capable, marketable and have a conducive atmosphere set for them to get employment or employ themselves”. He however acknowledges the need for more investment in science and technology in order to increase farm machineries. “Currently, there is about 70 percent of farmers are still using hand hoe tools and about 64 percent of farmers using tractors,” said the Minister.
In addressing the climate change issue, the Minister said that Tanzania is taking all necessary measures within its capacity in making sure to put in place mitigation and adaptation measures to address challenges brought about by climate change. Tanzania rests on a 945,000 square kilometres and that the rain is therefore limited. “Our goal is to produce more crops suitable for rainy seasons and crops that are drought resistible,” explained Hon. Eng. Chiza.
“Taste can be an issue to some farmers as they tend to grow more maize rather than finding alternative crops to grow that can likely be sustainable and resistible to the particular seasonal-weather,” said the Minister.
The Minister further explained that there is also a need to improve transport network and educate farmers about agro ecological zones and green revolution. “We need long term measures that can address permanent maintenance strategy in order to improve transport network, increase fertilizer use per hectare currently at an 8 kilogram to about 11 kilograms per hectare,” he explained.
The 15 US journalists are in the country from September 29 to October 9, 2013 through the John Hopkins International Reporting Project, funded by the Bill and Melinda Gates Foundation. The Bill and Melinda Gates Foundation had been devoting most of its time and resources to support any efforts aimed at transforming Africa from poverty eradication through its agriculture sector.
The group is expected to wrap up its tour by visiting the KINU Innovation Space in Dar es Salaam, the iAGRI Project at Sokoine University in Morogoro, the One Acre Fund in Iringa and the Oikos East Africa group in Arusha, before returning back to the United States on October 9, 2013.
PEMBE ZA NDOVU, UGAIDI NI VITA YA KIMATAIFA: KIKWETE
Posted on 12:27 by Unknown
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amesema ujangili wa pembe za ndovu na faru ni tatizo la kimataifa linaolohitaji kutokomezwa kwa ushirikiano huku akitaka mataifa makubwa kudhibiti soko la pembe hizo, hatua ambayo amesema inaweza kukomesha uwindaji haramu unaoathiri utalii barani Afrika.
Katika mahojiano amaaluma na Joseph Msami wa idhaa ya Kiswahili ya radio ya Umoja wa Mataifa mjini New York, rais Kikwete ambaye pia ameelezea hatari ya ugaidi nchini mwake na duniani kwa ujumla amesema hata hivyo nchi yake imechukua tahadhari kujihami na mashambulizi hayo. Kwanza Rais Kikwete anaanza kufafanua ukubwa wa tataizo la uwindaji wa pembe za ndovu na faru.
Subscribe to:
Posts (Atom)