50 Bing Coupons

  • Subscribe to our RSS feed.
  • Twitter
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • Facebook
  • Digg

Tuesday, 1 October 2013

mtuhumiwa wa mauaji auawa na wananchi makete

Posted on 13:09 by Unknown
Na Edwin Moshi, Makete
Katika hali isiyo ya kawaida wananchi wanaodhaniwa kuwa ni wa kijiji cha Usagatikwa kata ya Tandala wilaya ya Makete mkoani Njombe wameamua kuchukua sheria mkononi kwa kumpiga hadi kumuua Bw. Festo Sigala(44) kwa tuhuma za mauaji

Tukio hilo limetokea Septemba 29 mwaka huu katika kijiji cha Tandala wilayani hapo, baada ya wananchi hao kumfuata mtuhumiwa huyo kwa lengo la kumdhuru kutokana na tuhuma za mauaji ya mwananmke aliyetambulika kwa jina la Furaha Datovu Sanga(37)

Akithibitisha hilo ofisini kwake Mkuu wa polisi(OCD) wilaya ya Makete Alfred Kasonde (Pichani) amesema Bw. Nesco Thobias Chaula mkazi wa kijiji cha Usagatikwa aligundua kupatikana kwa mwili wa marehemu Furaha ambaye aliripotiwa kupotea tangu Mei 15 mwaka huu ambapo alitafutwa bila mafanikio ambapo mwili huo wa marehemu ulikutwa ndani ya choo cha shimo kinachomilikiwa na Festo Sigala ambaye kwa sasa ni marehemu
 
Amesema baada ya hapo wananchi waliamua kumsaka mtuhumiwa huyo ambapo walimkuta eneo la stendi ya mabasi katika kijiji jirani cha Tandala wakati akijaribu kutoroka baada ya kupata taarifa kuwa wamegundua kama alifanya mauaji, na wakaanza kumpa kipigo

"Walimkuta stendi huyo mtuhumiwa akiwa anataka kutoroka baada ya kujua kuwa anatuhumiwa kwa mauaji na mwili wa marehemu ulikutwa kwenye choo chake na wakaanza kumpiga kwa mawe, fimbo wakati alipotaka kutoroka eneo hilo" alisema Kasonde

Kufuatia kipigo cha wananchi hao kuwa kikali, mtuhumiwa huyo aliamua kutimua mbio kuelekea kituo cha polisi Tandala kwa lengo la kujisalimisha, lakini wananchi hao waliendelea kumfukuza na wakafanikiwa kumzingira na kuendelea kumshambulia kwa kipigo hasa maeneo ya kichwani amapo ubongo na damu vilimwagika kwa vingi hadi alipofariki dunia kabla hajafika kwenye kituo cha polisi

Amesema kutokana na wingi wa wananchi hao walioamua kujichukulia sheria mkononi, polisi waliokuwa kazini katika kituo hicho walizidiwa nguvu na kundi hilo la watu hivyo kushindwa kumnusuru mtuhumiwa huyo asiuawe kwani nguvu ya wananchi ilikuwa ni kubwa
 
hata hivyo baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamedai kuwa marehemu huyo aliuawa akiwa ndani ya kituo hicho cha Polisi baada ya wananchi kuwazidi nguvu polisi na kuvinja chumba alichokuwepo marehemu, lakini suala hilo limekanushwa na OCD Kasonde na kusema kuwa kituo hicho kipo salama na wala marehemu hakuuawa kwenye kituo cha polisi

"Hakuna ukweli wowote wa taarifa kuwa ameuawa akiwa lokapu ya kituo cha polisi Tandala, hakuna kituo kilichovunjwa na badala yake wananchi wenye hasira kali ndio waliomuua wakati akikimbilia polisi kunusuru maisha yake" alisema OCD Kasonde

Katika hatua nyingine ameiomba jamii kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwani ni kosa kisheria na badala yake wakimkamata mtuhumiwa wanatakiwa kumfikisha polisi ili sheria ichukuliwe

hadi sasa hakuna anayeshikiliwa kuhusiana na mauaji hayo na uchunguzi bado unaendelea
Email ThisBlogThis!Share to XShare to Facebook
Posted in | No comments
Newer Post Older Post Home

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to: Post Comments (Atom)

Popular Posts

  • tamasha la 32 la sanaa la bagamoyo lawasha moto, Mhe Makala asema utamaduni ni ajira kwa vijana
    NAIBU Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Mhe. Amos Makala amesema Sanaa na Utamaduni nchini itaendelea kuenziwa ili kuwaleta a...
  • wadau farida na paul wameremeta
     Wakila pozi baada ya kumeremeta katika Kanisa la Mtakatifu Petro jijini Dar es salaam kabla ya kwenda kwenye mnuso wao wa nguvu katika hote...
  • WAZIRI DK. NCHIMBI AMTEMBELEA PADRI ALIYEMWAGIWA TINDIKALI HOSPITALI YA MUHIMBILI LEO
    Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akisalimiana na Padri Joseph Monesmo Magamba wa Kanisa la Romani Katoliki Pa...
  • Naibu Spika aongoza Mkutano wa ACP nchini Ubelgiji
    Mhe.Job Ndugai,Mbunge wa Kongwa na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania akiongoza Mkutano wa Kamati ya Mazingira na Jamii cha Umoja wa Mabunge y...
  • Sherehe za kufunga mafunzo katika kikosi cha 842 Kj Mlale Jkt, Songea
      Mkuu wa wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma Mhe Senyi Ngaga kushoto akiangalia shehena ya mahindi ya chakula katika kikosi cha 842 Kj mlale Jkt...
  • barabara ya Mtoni-mbagala ilivyo
  • BACK TO THE SUA SEASON 2 EPISODE 2, KIJENGE, ARUSHA
    YECHU! YECHU! YECHU! HII HAILIPIWI HATA KUMI ARIFU  YAANI KIINGILIO NDO KITU HAMNAGA Pale Pale fasi ya K-JUU mwisho wa daladala mkabala na k...
  • JK ALIPOKUTANA NA WADAU WASHINGTON DC
    Rais wa Tanzania Dr.Jakaya Kikwete alipokutana na mpiganaji SundayShomari wa VOA siku ya Jumatano kwenye ofisi za ubalozi washington Dc. Rai...
  • KATIBU MKUU UTUMISHI, Bw. GEORGE YAMBESI AFUNGUA MAFUNZO YA MFUMO WA KUSIMAMIA RASILIMALI WATU SEREKALINI (HUMAN CAPITAL MANAGEMENT INFORMATION SYSTEM, HCMIS - LAWSON) KWA WAKURUGENZI NA MAKATIBU
    TAWALA WA MIKOA Katibu mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. George Yambesi leo amefungua rasmi mafunzo ya mfumo wa komp...
  • WAZIRI MEMBE AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA KOSOVO
    Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kosovo, Mhe. Enver...

Blog Archive

  • ▼  2013 (500)
    • ▼  October (22)
      • barabara ya Mtoni-mbagala ilivyo
      • Tanzania katika hatua za muhimu za kuanza utekekel...
      • washindi wa chemsha bongo wapatikana
      • mtuhumiwa wa mauaji auawa na wananchi makete
      • UTAFITI WAONESHA KIFUA KIKUU(TB) KUSUMBUA VIJIJINI...
      • Dar lauded for KILIMO KWANZA (Agriculture First) I...
      • PEMBE ZA NDOVU, UGAIDI NI VITA YA KIMATAIFA: KIKWETE
      • President Obama Delivers a Statement on the Govern...
      • Kali TV: This week, meet Nazizi Hirji
      • Lindi na Mtwara wapata washirika kutoka Norway
      • President Kikwete congratulates Nigeria on achievi...
      • Mvua yakata barabara kijiji cha Ndungu Wilayani Same
      • KONGAMANO LA JUMUIYA YA WAZEE WASTAAFU,WAKULIMA NA...
      • Rais Dk.Shein akutana na Balozi wa Uholanzi na Bal...
      • Balozi wa Marekani aiaga Wizara ya Mambo Ndani ya ...
      • MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI KILELE CHA MAAD...
      • SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR YAWATAHADHARISHA...
      • TAARIFA MBALIMBALI ZA MICHEZO KUTOKA KWA SHIRIKISH...
      • MAALIM SEIF AKUTANA NA VIONGOZI WA CHAMA CHA WALIM...
      • KIJIWE CHA UGHAIBUNI
      • TASWIRA HALISI YA MJI WA DUBAI ASUBUHI YA LEO.
      • Here is CPwaa's New Hit Single "Chereko Chereko"
    • ►  September (478)
Powered by Blogger.

About Me

Unknown
View my complete profile