Mmoja kati ya Wakulima wa Kijiji cha Nguruweni Dole Mzee Kitwana Mustaha aliishukuru na Kuipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwa kukamilisha ahadi yake ya kuwapatia hati za umiliki wa mashamba wakulima hao kwa ajili ya kilimo katika maeneo yaliyowahi kuleta mgogoro kwa muda mrefu.
Baadhi ya wananchi na wakulima wa Kijiji cha Nguruweni wakiwa katika mkutano maalum uliotishwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif wa kukabidhiwa hati za umiliki wa mashamba ya kilimo katika maeneo yao.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akizungumza na wakulima wa Kijiji cha Nguruweni kabla ya kuwakabidhi hati za umiliki wa mashamba ya kilimo wakulima hao.
Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi Hati ya umiliki wa shamba Bibi Josephine Yohana kwenye hafla maalum ya kumaliza mgogoro wa mashamba katika kijiji hicho.
Balozi Seif akimpatia Hati Bwana Mohd Ali Pili ya kumiliki eneo la kilimo katika Kijiji cha Nguruweni ambako kuliibuka mgogoro uliosababishwa na kuinbgizwa watu wasiohusika na maeneo hayo kwa kilimo. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
0 comments:
Post a Comment