50 Bing Coupons

  • Subscribe to our RSS feed.
  • Twitter
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • Facebook
  • Digg

Monday, 30 September 2013

HIKI HAPA KILIO CHA WANAFUNZI WA UDAKTARI BUGANDO KWA SERIKALI YA RAIS KIKWETE

Posted on 23:20 by Unknown

Rais wa Serikali ya Wanafunzi Madaktari wa Chuo cha Bugando (CUHASSO) Musa Leonard Mdede (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa tamko kwa niaba ya wanachuo kuiomba Serikali kutoa udhamini wa ada kwa asilimia 100 kwani wanafunzi wengi wanashindwa kumaliza masomo yao kutokana na kujikita kwenye shughuli za usakaji pesa kwaajili ya malipo, nazo ada zikiendelea kupanda kila misimu huku Serikali ikiendelea kutoa ufadhili kwa asilimia ileile.

"Tunaiomba Serikali kuongeza kiwango cha ufadhili ili wanafunzi au vijana walio na nia ya kusoma fani ya udaktari wakiwa wanalenga kuokoa maisha ya watanzania watimize ndoto zao. Tunatambua kuwa nchi yetu ina upungufu wa asilimia 60 ya madaktari wa sekta ya afya"

"Na kwa takwimu daktari mmoja anahudumia zaidi ya wagonjwa 33,000 kutokana na idadi ya watanzania wote, sasa kuendelea kuwa na vijana wanaoshindwa kuendelea na masomo ya sekta ya afya kwa sababu ya kukosa karo, nikurudi nyuma na kamwe malengo hayatotimia" Alisema Musa Leonard Mdede

Makamu wa Rais wa Serikali ya Wanafunzi Madaktari wa Chuo cha Bugando (CUHASSO) Atukuzwe Mordekai Gwihangwe (katikati) akitoa ufafanuzi jinsi ada kubwa inayotozwa kwa wanafunzi inavyokwamisha malengo ya wanafunzi wa sekta ya Afya nchini hali inayopelekea serikali kukosa wataalamu wa kutosha. Kushoto ni Rais wa CUHASSO Musa Leonard Mdede na kushoto ni Benjamin Thomas.



Ndugu wana habari,napenda kuchukua nafasi hii kama Rais wa serikali ya wanafunzi chuo kikuu katoliki cha sayansi ya Afya na Tiba(CUHAS-Bugando) kwa niaba ya wanazuoni wote wa chuo hiki na kwa niaba ya wanafunzi wa sekta ya Afya wa vyuo vikuu vyote visivyokua vya umma nchini(yaani vyuo vikuu vikuu vyote vya fani ya afya vinavyomilikiwa na mashirika ya dini na mashirika ya watu binafsi).Kuweza kueleza kilio chetu kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na vyombo mbalimbali vya kiserikali vyenye mamlaka ya kusimamia Elimu ya juu na vyuo vikuu nchini.

I:DHANA YA ASILIMIA MIA MOJA YA MKOPO.Watanzania wengi  wakiwemo ndugu na jamaa wa karibu wanaotugharamikia katika masomo yetu wanaelewa kwamba mwanafunzi anayesoma fani za Afya kama Udakatari,Ufamasia,Uuguzi na nyinginezo kama hizo analipiwa kila kitu na serikali kupitia bodi ya mikopo kwa hiyo hahitaji msaada wowote wa kifedha kutoka kwa wazazi au walezi kwa kua anjitosheleza kwa kila kitu.Dhana ambayo kwa mwanafunzi anayesoma katika chuo kikuu kisichokua cha Umma ni tofauti kabisa.Kwa kua asilimia mia moja inayoongelewa ni kama asilimia hamsini tu ya karo zinazotozwa katika vyuo hivi.

Wanafunzi wote wa vyuo hivi vya fani ya Afya visivyokua vya umma tumekua tukipokea kiasi cha shilingi za kitanzania milioni mbili na laki sita tu(Tsh.2,600,000/=)  toka bodi ya mikopo kama mkopo kwa ajili ya Ada.Kiwango hiki kipo hivo toka wakati huo ambapo katika vyuo hivi Ada ilikua inatozwa kwa kiwango hicho.Ni takribani miaka sita sasa kiwango hiki kimebakia kama kilivo bila kuongezeka.Wakati kutokana na kuongezeka kwa gharama za uendeshaji wa taasisi hizi.

Ada zimekua zikiongezeka mwaka hadi mwaka na sasa kufikia takribani milioni nne,na zaidi kama karo katika vyuo hivi mbalimbali Ikiwa ina maana kwamba kiasi kinachobaki baada ya Tsh.2,600,000/= kutolewa kama mkopo mwanafunzi mwenyewe inatakiwa ajilipie pamoja na gharama zingine ambazo si sehemu ya karo zinazohitajika kutolewa.Wanafunzi wengi katika vyuo hivi wanasoma na kuishi katika mazingira magumu sana kwa kua gharama anazotakiwa kuchangia binafsi ni kubwa kiasi cha kuwalemea wanafunzi wengi ambao wengi wetu ni watoto wa wakulima ila tukiwa na haki ya kupata Elimu bila kujalisha hali ya uchumi wa familia zetu

.CHANGAMOTO;hali hii imepelekea wanafunzi wengi wanaochaguliwa kushindwa kujiunga na vyuo hivi kwa kushindwa kumudu gharama hizi,lakini pia imepelekea wanafunzi wengi kupoteza mda wao mwingi katika kufanya vibarua ili kupata kiasi cha kumalizia ada ambayo imepelekea ufaulu wao kushuka na wengine kupoteza kabisa nafasi ya kuendelea na masomo.

OMBI LETU KWA SERIKALI;kwa kua tumejiunga na vyuo hivi kwa mfumo halali wa Tume ya vikuu Tanzania(TCU) ambao haukuangalia hali ya kiuchumi ya familia zetu kama tutamudu au hatutamudu kulipa gharama hizi,kwa kua tulijiunga na vyuo hivi kwani tulikua na vigezo vya kusoma fani hizi kama wenzetu wanaosoma katika vyuo vikuu vya umma na hata zaidi na kwa kua tukihitimu sisi wote yaani wenzetu wanaosoma vyuo vikuu vya umma na sisi tunaosoma vyuo vikuu visivyokua vya umma tunakwenda kuhudumia na kuokoa uhai wa watanzania walewale.

Tunaiomba serikali iongeze kiwango hiki tunachopewa kama mkopo kwa ajili ya ada,ili hiyo Asilimia mia moja inayosemwa iwe na maana kwetu kwa kua kwa sasa ni kama nusu tu.Wengi wanashindwa kujiunga na vyuo hivi kwa kushindwa kumudu gharama hizo.Katika nchi yenye upungufu wa 60% ya madaktari na wataalamu afya kwa ujumla,pia katika nchi ambayo daktari mmoja anahudumia wagonjwa zaidi ya 33 elfu.Si vema kuona vijana wenye dhamira na nia thabiti ya kuokoa maisha ya watanzania wanashindwa kutimiza ndoto hizo za kua wataalamu wa Afya ati kwa kushindwa kulipa karo.

Tume ya vyuo vikuu Tanzania(TCU):Upandishwaji Ada katika vyuo vikuu visivyokua vya umma usiofuata utaratibu na Kile kinchojulikana kama “List of Approved programme fees” ikiainisha gharama za ada zinazotozwa katika vyuo vikuu vyote nchini.Tume vya vikuu Tanzania imepewa mamlaka kisheria kwa mujibu wa sheria ya vikuu No.7,2005.Kusimamia kuanzia udahili na uendeshaji wa vyuo vikuu vyote nchini vya umma na visivyokua vya umma.Central Admission system
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII;Institute of Health and Allied Health sciences.

Kumekuwa na changamoto kubwa katika gharama za ada, chakula na makazi kwa wanafunzi wa stashahada katika vyuo vya Afya hasa vile vya binafsi ambapo gharama za uchangiaji zinazidi kuwa kubwa ikizingatiwa kuwa wanafunzi hao hutejigemea kiasi kikubwa na kuwa serikali kupitia wizara ya afya imekua ikitoa fedha kwa ajiri ya wanafunzi hao.

OMBI LETU:-Tunaiomba Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii kuweka wazi ni kiasi gani inachangia kwa kila mwanafunzi mmojammoja wa stashada katika vyuo vya afya kwa kueleza mchanganuo halisi ili kuwawezesha wanafunzi hao kutambua ni kwa kiasi gani Serikali kupitia wizara ya Afya na ustawi wa jamii inachangia kama ulivyo utaratibu wa bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa shahada .

 Vilevile kumekuwa na changamoto ya mabadiliko ya gharama za ada kwa wanafunzi wa stashahada katika vyuo vya afya na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wanafunzi hao hivyo Tunaiomba Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii Kutoa gharama halisi ambazo wanafunzi wa stashada katika vyuo vya Afya watapaswa kuchangia katika vyuo mbalimbali ikiwemo vile vya binafsi.

Kulingana na changamoto mbalimbali zinazozidi kujitokeza kwa wanafunzi wa stashahada katika vyuo vya afya, Tunaiomba Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii Kuboresha  mfumo wa uwezeshaji kwa wanafunzi wa stashada na kuweka mfumo na taratibu zitakazosimamia mabadiliko ya ada katika vyuo mbalimbali vya Afya ili kuweza kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza vyuoni hasa vya binafsi.

Kumekuwa na uchakavu wa miundombinu inayomilikiwa na wizara ya Afya katika vyuo vya afya na hivyo kupunguza ufanisi wa masomo kwa wanafunzi hivyo Tunaiomba Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii Kuboresha miundombinu mbalimbali inayomilikiwa na wizara ya afya katika vyuo vya Afya vinavyotoa stashahada.
Read More
Posted in | No comments

Posted on 22:49 by Unknown

Read More
Posted in | No comments

BREKING NYUUZZZZZZ: SERIKALI YA MAREKANI YAFUNGA SHUGHULI ZA IDARA ZOTE ZISIZO MUHIMU

Posted on 22:41 by Unknown
Rais Barack Obama amelihutubia taifa Jumatatu usiku akisiistiza kwamba jeshi la taifa litaendelea na kazi zake wakati sehemu za serikali kuu zinafungwa kuanzia leo Jumanne baada ya bunge kushindwa kukubaliana juu ya bajeti ya mwaka 2013 - 2014. Hatua hii inajulikana kama Government Shutdown.

Baada ya wabunge wa Baraza la Wawakilishi kushindwa kukubaliana ilipofika usiku wa manane Jumatau, juu ya bajeti ya matumizi, serikali kuu ililazimika kutangaza kwamba sehemu za idara kadhaa zitabidi kufungwa.
Mvutano wa kisiasa umekuwa ukiendelea bungeni kuhusiana na sheria ya kihistoria ya Rais Obama, ya kutoa huduma nafuu za afya ambayo imekuwa mashuhuri kwa jina la "Obamacare".
Baraza la wawakilishi linaoongozwa na chama cha Republican liliidhinisha mswada wa matumizi ya serikali lakini kwa kuambatanisha kufutwa kwa sheria ya Obamacare. Na mara tatu Baraza la Seneti linalodhibitiwa na chama cha Demokrat limepinga mswada huo.
Kutokanana Bunge kutokubaliana juu ya kupitisha mswada wa kuongeza muda wa matumizi ya serikali kuu sheria ya Marekani inahitaji idara zote ambazo hazina shughuli muhimu kusita kufanya kazi kuanzia Oktoba mosi, yaani leo Jumanne
Jumla ya wafanyakazi wa serikali wapatao 800,000 wanakwenda likizo bila malipo
ambapo inatarajiwa kutakuwa na hasara ya dola bilioni moja kwa wiki.
Chanzo:VOA
Read More
Posted in | No comments

Posted on 22:40 by Unknown

Read More
Posted in | No comments

NATURAL PRODUCTS FOR your skin

Posted on 22:39 by Unknown

Aloe Fleur de Jouvence-Flower of Youth is one of the most effective restorative beauty collections ever assembled. It is a collection of six wonderful components – each designed to fill a special part in a complete regimen of facial skin care.

To create one of the most effective restorative beauty regimes ever assembled, we took pure, stabilized Aloe Vera gel, combined it with nature’s own collagen, and added exceptional moisturizers, emulsifiers and humectants.

Each product in Aloe Fleur de Jouvence has been developed with great care and attention to the daily needs of your skin. We start with pure, Stabilized Aloe Vera gel, and combine it with nature’s unique cellular substance, Collagen, along with exceptional moisturizers, emulsifiers and humectants. This creates a unique skin care range that helps counteract the threat of time, weather and environmental elements. The preventive and restorative Aloe Fleur de Jouvence program provides a daily skin care regime to help promote the naturally occurring attributes of youth, vigor, freshness and radiance of the skin.

Aloe Vera has always been great for the skin. Now, pamper yourself even more with Aloe Fleur de Jouvence!

The Aloe Fleur de Jouvence Collection includes:
Aloe Cleanser
Rehydrating Toner
Firming Day Lotion
Recovering Night Creme
Mask Powder
Aloe Activator
Mixing spoon, applicator brush

For more information Call 0718 14 40 39 / 0786 76 60 28
Read More
Posted in | No comments

SIKU YA UTALII DUNIANI YENYE KAULI MBIU UTALII NA MAJI YAFANA ZANZIBAR

Posted on 22:38 by Unknown
 Mmoja wa watalii akijikuta akiingia katikati ya ngoma za utamaduni baada ya kunogewa na ngoma ya Msewe maarufu kama 'Kibati'  siku ya Utalii Duniani iliyoadhimishwa Zanzibar.
 Ngongoti huyu akiwa mmoja wa kiburudisho katika sherehe hizo.
 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali  Mh. Ali Juma Shamuhuna akifunguwa resi za ngalawa Foroza Mchangani mjini Zanzibar.
 Ngalawa zikionekana kuanza resi hizo siku ya Utalii Duniani .
Mshindi wa mwanzo wa ngalawa ya Lailati Bw Khalidi Khamis akipokea zawadi kwa mgeni rasimi Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mh Ali Juma Shamuhuna.
Read More
Posted in | No comments

President Kikwete sends Congratulatory Message to the People's Republic of China

Posted on 22:06 by Unknown
H.E. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania has sent a Congratulatory Message to H.E. Xi Jinping, President of the People’s Republic of China on the occasion of the 64th anniversary of the founding of the People’s Republic on the 1st October, 2013.

The message reads as follows.

““H.E. Xi Jinping,
President of the People’s Republic of China,
Beijing,
CHINA.

Your Excellency,

On behalf of the people and government of the United Republic of Tanzania and on my own behalf, I wish to convey my sincere congratulations to you on the occasion of the founding of the People’s Republic of China.

I am confident that with the good will and understanding on both sides, the bilateral relations between Tanzania and China will continue to flourish as both countries pursue the shared ideas and objectives for the benefit of the two countries and peoples.

      Your Excellency, as we approach a Jubilee of our bilateral relations, let me express our gratitude and appreciation to the Government of the People’s Republic of China for its fervent and continued efforts in bringing sustainable development to the people of Tanzania.

         Please accept, your Excellency, my best wishes for your personal good health and peace and prosperity for the people of China.

Jakaya Mrisho Kikwete

PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA”


Issued by: 

The Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation, 

Dar es Salaam,
1st October, 2013.
Read More
Posted in | No comments

WAKAZI WA KIKUYU KUSINI WAANDAMANA KUPINGA BOMOABOMOA ILIYOPANGWA NA CDA MKOANI DODOMA, MKUU WA MKOA AINGILIA KATI

Posted on 21:44 by Unknown
 Maelfu ya Wananchi wa Kata ya kikuyu kusini wakiandamana katika mitaa ya mji wa Dodoma kwa ajili ya kupinga kubomolewa na mamraka ya ustawishaji makao makuu  [CDA] wanaotarajia kubomoa nyumba, mapagale na misingi ya wakazi hao.
  Maelfu ya Wananchi wa Kata ya kikuyu kusini wakiandamana katika mitaa ya mji wa Dodoma kwa ajili ya kupinga kubomolewa na mamraka ya ustawishaji makao makuu  [CDA] wanaotarajia kubomoa nyumba, mapagale na misingi ya wakazi hao.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Rehema Nchimbi akipaza sauti ya matumaini kwa wakazi wa Kata ya kikuyu kusini walioandamana kupinga Bomoabomoa ya CDA waliokuwa wamepanga kubomoa nyumba na misingi katika eneo hilo.  Alisema “Naitengua amri hiyo na namwagiza Mkurugenzi akutane na wananchi hawa pamoja na viongozi wao ili kuweza kufikia muafaka kwani kubomoa sio suluhu hamuwezi kubomoa Dodoma nzima na ningependa kuletewa taarifa juu ya sula hili … mnachotakiwa ni kuboresha na kutumia njia sahihi ambazo hazita waumiza wananchi ambao ndiyo wateja wenu.
Diwani wa kata ya Kikiyu kusini Ancelmu Kutaka akifafanua jambo mbele ya Wananchi wa kata hiyo waliondamana kupinga kubomolewa na Mamraka ya ustawishaji makao makuu [CDA] walipanga kuboa wakati wowote kuanzia leo.
Kaimu Mkurugenzi wa CDA Paskas Mulagili Akifafanua jambo wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali kuhusu maandamano ya wananchi wa kata ya Kikuyu Kusini walioandamana kupinga ubomoaji unaotarajiwa kufanywa na mamlaka hiyo siku yoyote kuanzia leo. 

Habari na picha na 
John Banda, Dodoma
WAKAZI wa Kata za Kikuyu Kusini na Kilimani mkoani Dodoma wameandamana kupinga amri iliyotolewa na Mamlaka ya Ustawishaji ya Makao Makuu (CDA) ambayo inawataka kuhama katika eneo hilo ndani ya siku saba.
Wakazi hao walioandamana kutoka Kikuyu hadi Viwanja vya Nyerere Square katikati ya mji wakimtaka mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi kuzungumza nao.
Maandamano hayo yalisindikizwa na ulinzi wa polisi hadi katika viwanja hivyo huku wakazi hao wakiwa wameshikilia mabango yenye jumbe mbalimbali.
Wakazi hao wakiwa wanaimba nyimbo huku wakiinua mabango yao juu yenye ujumbe kama Cda ni zaidi ya Alshababi, CCM mnaiona bomoabomoa, Cda ni zaidi ya Nduli Idd Aminini Dada na lingine likisomeka Hata wanyama hupewa hifadhi.
Wakizunguza na waandishi wa habari katika viwanja hivyo wakati wakimsubiri mkuu wa mkoa baadhi ya wananchi na viongozi wao wa mitaa walidai kuwa lengo la maandamano hayo ni kufikisha kilio chao kwa serikali ya mkoa.
Andrew Mdumi mwenyekiti wa mtaa wa Mkalama ambao ni sehemu ya eneo linalotakiwa kuvunjwa alisema kuwa wameamua kufanya maandamano hayo mara baada ya kupewa amri ya kuondoka katika eneo wanaloishi kwa kipindi kirefu.
Mdumi alisema, kuwa Mamlaka ya ustawishi Makao makuu imekuwa ikiwapatia namba kila wakati na kudai kuwa itakuja kuwapimia lakini katika hali ya kushangaza imewapa amri ya kuondoka ndani ya siku saba kwa madai kuwa wamevamia katika eneo hilo ambalo lilikuwewa limetengwa kwajili ya bustani za mbogamboga na matunda.
“Wanataka tuondoke ili kupisha kilimo cha mbogamboga na matunda hivi kweli mboga na maisha yetu kipi cha msingi kuna nyumba zaidi ya 1000 ambazo watakakuzibomoa kwajili tuu ya kupisha bustani” alisema
Alisema kuwa wamekuwa wakishirikiana na CDA kwa kipindi kirefu ili kuweza kufanikisha zoezi la upimaji wa viwanja hivyo hata kwa gharama zao wenyewe.
Mwekiti wa kamati ya upimaji katika Kata ya Kikuyu kusini Mathew Ndallu, alisema kuwa katika kufuatilia suala hilo la kupimiwa viwanja walikutana na CDA na kukubaliana kuwa waje wafanye utambuzi wa nyumba zilizopo, mapagale na misingi ili waweze kufanya upimaji.
Ndallu alisema kuwa walikubaliana na kuwa kutokana na eneo hilo kuwa halijapimwa wao wako tayari kuchangia gharama za upimaji ili kuwezesha zoezi hilo kufanyika.
“Tulikubaliana nao mara baada ya wao kuja kutambua idadi ya nyumba mapagale na misingi watupimia na sisi tuko tayari kuchangia kiasi cha sh.500,000 kwa kila mwenye eneo” alisema Ndalllu.
Aidha alisema kuwa katika hali ya kushangaza pale ambapo walikuwa wanasubiri kupimiwa CDA waliwageuka na kuwataka kwanza wao wapatiwe viwanaja 500 ili waweze kuwapiamia.
“Mara baada ya kukubaliana nao kuwa tuko tayari kuchangia lakini Mkurugenzi alituambia kwanza tuwape wao viwanja 500 ili waweze kuja kutupimia na kama hatutakubali basi watakuja kutubomolea” alisema.
Alisema kuwa mara baada ya wao kukataa kumpa mkurugenzi huyo viwanja hivyo aliwaandikia barua hiyo ambayo ilikuwa inawataka wakazi wa maeneo hayo kuondoka kabla ya tarehe 30 ya mwezi Septemba (jana).
“Walituandikia barua ambayo inatutaka kuaondoka ndani ya siku hizo saba ikiwa ni kuanzia tarehe 23 ya mwezi huu ambapo inaishia leo (jana) na kesho (leo )wanakuja kuanza kubomoa” alisema Ndallu.
Alisema kutokana na hali hiyo ambayo imeonyesha kuwa CDA imeshindwa kuwasikiliza kilio chao wameona kuwa hiyo ndiyo njia sahihi ya wao kupata suluhu ya tatizo lao.
Alisema kuwa jumla ya mitaa mnne katika kata hizo ndiyo inayotakiwa kubomolewa ambayo ni mitaa ya Mkalama, Chidachi pamoja na Image A na B.
Akizungumza na kundi la wakazi hao mkuu wa mkoa wa Dodoma Dk Rehema Nchimbi, alisema kuwa anatengua amri hiyo iliyotolewa na CDA na kumtaka Mkurunzi wa mamlaka hiyo kukutana na viongozi wa maeneo husika.
“Naitengua amri hiyo na namwagiza Mkurugenzi akutane na wananchi hawa pamoja na viongozi wao ili kuweza kufikia muafaka kwani kubomoa sio suluhu hamuwezi kubomoa Dodoma nzima na ningependa kuletewa taarifa juu ya sula hili … mnachotakiwa ni kuboresha na kutumia njia sahihi ambazo hazita waumiza wananchi ambao ndiyo wateja wenu.
Read More
Posted in | No comments

ngoma azipendazo ankal

Posted on 20:00 by Unknown
Orchestra Super Mazembe walitamba sana na ngoma yao ya 'Kassongo'
Read More
Posted in | No comments

wadau farida na paul wameremeta

Posted on 17:47 by Unknown
 Wakila pozi baada ya kumeremeta katika Kanisa la Mtakatifu Petro jijini Dar es salaam kabla ya kwenda kwenye mnuso wao wa nguvu katika hoteli ya Golden Tulip si wengine bali ni wadau wakubwa wa Globu ya Jamii Farida Hussein Muyinga na Paul Herman Kirigini
 Wadau Farida na Paul wakiwa na keki maalumu kwa kamati ya maandalizi iliyofanikisha kumeremeta kwao
 Ni wakati wa kukata na kulishana keki kwa wapendanao hao
 Ufunguzi rasmi wa dansi
Vigeregere na hoi hoi wakati maharusi wakiingia ukumbini 
Kwa mapicha mengine ya kumwaga BOFYA HAPA
Read More
Posted in | No comments

ACCT members attend Master Builders South Africa Congres 2013 in Johannesburg

Posted on 17:44 by Unknown
A  delegation of the  Association of Citizen Contractors Tanzania (ACCT) pose for a souvenir picture  when attending a two-day Masters Builders South Africa Congress 2013 in Johannesburg, South Africa, at the invitation of the country's  Construction Industry Development Board.

Read More
Posted in | No comments

magari yanauzwa

Posted on 17:36 by Unknown
ALTEZAA  MODEL 2004 CC 2000 ASKING PRICE TSHS.11,000,000/-
TOYOTA IST MODEL 2004 ASKING PRICE  10,000,000/- 
CONTACTS  SELLER +25575722586
Read More
Posted in | No comments

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Fedha za Serikali Bw Ludovick Utouh atua mkoani Kagera kufanya Ukaguzi maalum katika Manispaa ya Bukoba

Posted on 17:32 by Unknown
  Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Fedha ya Serikali Ludovick Utouh akifungua mkutano wa maelekezo ya ukaguzi maalum katika Manispaa ya Bukoba

Madiwani wa Manispaa ya Bukoba wakisiliza maelekezo ya CAG wakiongozwa na Meya wa Manispaa hiyo Mstahiki Antory Amani

--------------------------------------------------
Na Angela Sebastian, Bukoba 
 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Fedha za Serikali Bw. Ludovick Utouh amewasili mkoani Kagera kwa ajili ya kufanya Ukaguzi maalum katika Manispaa ya Bukoba ili kutafuta ufumbuzi wa kutatua mgogoro uliodumu takribani miaka miaka miwili na kukwamisha maendeleo ya wananchi wa Manispaa hiyo. 
Bw. Utoh mara baada ya kuwasili katika mkoa wa Kagera Septemba 30, 2013 (jana) kilifanya kikao cha ufunguzi wa Ukaguzi Maalum katika Manispaa ya Bukoba na kufafanua madhumuni ya Ukaguzi huo ikiwa ni pamoja na ni namna gani ukaguzi huo utafanyika. 
Bw. Utouh alisema chimbuko la Ukaguzi Maalum lilitokana na hoja zilizojitokeza baada ya kutokea kutoelewana baina ya Waheshimiwa Madiwani wa Manispaa ya Bukoba ambapo ilisababisha mgawanyiko mkubwa wa makundi na kuchangia kuzorotesha utendaji kazi wa Manispaa hiyo. Hoja hizo kuu zikiwa ni pamoja na kukosekana kwa uwazi kuhusu miradi ya uwekezaji ilivyopatikana, Mstahiki Meya kufanya maamuzi yake binafsi bila kushirikisha maamuzi ya Waheshimiwa Madiwani kupitia Baraza la Madiwani. 
Akifafanua kifungu cha sheria kinachompa mamlaka ya kufanya ukaguzi maalu Utouh alisema, “Kwa mujibu wa kifungu cha 36 cha sheria ya Ukaguzi wa Umma Na. 11 ya mwaka 2008, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali anayo mamlaka ya kufanya ukaguzi pale atakapoona kuwa inafaa katika masuala yanayohusiana na fedha na mali za Umma.” 
Aidha Bw Utouh alieleza kuwa alichelewa kufika katika Manispa ya Bukoba kufanya Ukaguzi Maalum ili kufanya maandalizi ya kutosha kabla ya ukaguzi huo ikiwemo  kuuandaa Adidu za Rejea wakati wa kufanya ukaguzi huo ili kutenda haki katika pande zote mbili na kuumaliza mgogoro. 
Adidu za Rejea 13 za Ukaguzi Maalum Manispaa ya Bukoba Kuchunguza usahihi wa utaratibu uliotumika kumpata mwekezaji wa kituo cha kuosha magari (ACE Chemical Ltd), Kuchunguza uhalali wa nyaraka na kiasi kilichowekezwa cha sh.297,000,000 kwenye mradi wa kuosha magari Kuchunguza tatizo na sababu zilizopelekea viwanja 800 kutogawiwa kwa wananchi waliochangia gharama za upimaji.
Pia kuchunguza wa upimaji viwanja 5,000 Kuchunguza miradi wa ujenzi wa soko, ujenzi wa kitega uchumi na kituo cha Mabasi, ujenzi wa chuo cha ualimu, ujenzi wa kituo cha maarifa na ujenzi wa Bwawa kwa ajilli ya utalii. 
Na pia Kuchunguza Kiwanja cha Shule ya Msingi Kiteyagwa, Barabara ya kupitia Kagondo Kaifo hadi Kagondo Karuguru na kuchunguza masuala mengine ya matumizi ya fedha yanayoashiria ubadhirifu. 
“Ukaguzi huu maalum unawagusa waheshimiwa kadhaa wenye nyadhifa za juu kisiasa na Serikalini na pia katika uongozi wa Halmashauri;kwa hiari hiyo ningependa kutoa tahadhari kubwa kwa uongozi wa Manispaa ya Bukoba na kwa wale wote wanaotuhumiwa kwa njia moja au nyingine kujiepusha na vitendo vyovyote vyenye mwelekeo wa rushwa ambavyo vinaweza kuvuruga mwenendo mzima wa ukaguzi huu maalum na kusabisha matokeo yaliyokusudiwa kushindwa kufikiwa”, alisisitiza.
 “Wakaguzi hawa ni wenye ujuzi wa kutosha na wa muda mrefu msije mkajaribu kuwapelekea vibahasha mtajisumbua bure kwani hawatapokea.” Aliongeza Utouh. 
Vilevile Bw.  Utouh aliwaagiza Katibu Tawala Mkoa na Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Bukoba Kuhakikisha kuwa watendaji wote waliokwishahama na watahitajika kutoa maelezo katika ukaguzi huo maalum wapatikane ili kutoa ushirikiano wa dhati. 
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Kanali Mstaafu Fabian Massawe alimshukuru Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Fedha ya Serikali kufika mkoani hapa ili kutoa suruhu ya mgogoro wa muda mrefu uliokwamisha jitihada za kuwaletea maendeleo wananchi wa Manispaa ya Bukoba. 
Taarifa ya ukaguzi maalum katika Manispaa Bukoba itakamilika ndani ya siku 35 kuanzia Septemba 30, 2013 na mara baada ya kukamilika taarifa hiyo itakabidhiwa Ofisi ya Waziri Mkuu ili kuwawajibisha wale wote watakaobainika kufuja fedha na mali za serikali na kuuumaliza mgogoro uliodumu miaka miwili.
Read More
Posted in | No comments

Spika Makinda apongeza Mabunge ya Afrika kwa kuongeza idadi ya Wanawake

Posted on 17:18 by Unknown
 Spika wa Bunge na Rais wa Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola barani Afrika,Mhe Anne Semamba Makinda akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Chama cha Wabunge Wanawake wa Jumuiya ya Madola Tawi la Seychelles ambapo alipongeza nchi za Jumuiya ya Madola kwa kuongeza idadi ya wanawake katika mabunge yake.Alitolea mfano nchi za umoja huo zilizopo Afrika Mashariki ambapo Uganda,Kenya Rwanda na Tanzania idadi ya wanawake imeongezeka katika chaguzi walizofanya hivi karibuni.Aidha alisema Afrika Mashariki ni mfano wa kuigwa ambapo Maspika wa Uganda Rwanda na yeye mwenyewe ni wanawake
 Spika Makinda katika picha ya pamoja na viongozi wa Chama cha Wabunge Wanawake wa Jumuiya ya Madola barani Afrika.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti Mhe.Beatrice Shellukindo ambae pia ni Mwakilishi wa Chama hicho Afrika Mashariki na katikati ni Mwenyekiti Mhe.Lucia Witbooi toka Namibia.
Mhe.Spika Anne Makinda akipokea zawadi toka kwa Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Mandola katika ngazi ya kimataifa ambae pia ni Spika wa Uganda,Mhe Rebecca Kadaga wakati wa uzinduzi wa Chama cha Wabunge Wanawake wa Jumuiya ya Madola nchini Seychelles. 
Picha zote na Saidi Yakubu wa Ofisi ya Bunge.
Read More
Posted in | No comments

KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA JOHN CASMIR MINJA AHUDHURIA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAGEREZA NCHINI ZAMBIA

Posted on 17:00 by Unknown
 Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania, John Casmir Minja(wa tatu kulia) akiwa amesimama katika Jukwaa Kuu kupokea heshima wakati Gwaride la Askari wa Magereza wa Zambia likipita mbele ya Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Magereza nchini  Zambia Septemba 26, 2013 (wa kwanza kushoto), Waziri wa Mambo ya Ndani wa Zambia(Mb) Mhe. Edgar Lungu. Wengine ni Mkurugenzi wa Magereza anayesimamia Uzalishaji na Urekebishaji katika Taifa la Sudani Kusini(wa kwanza kulia) akiwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Magereza.
 Askari wa Magereza wa Zambia wakipita mbele ya Mgeni Rasmi, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Zambia, Mhe. Edgar Lungu(hayupo pichani) katika Mwendo wa haraka kama wanavyoonekana Kikakamavu wakati wa Maadhimisho ya Magereza Day ya Zambia ambapo Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania, John Casmir Minja hivi karibuni alihudhuria  Maadhimisho ya Siku ya Magereza huko Kabwe, Zambia.
 Mkuu wa Jeshi la Magereza Zambia, Kamishna wa Magereza Percy Chato(wa kwanza mstari wa kwanza) akiwa na Kamishna Jenerali wa Magereza Tanzania, John Casmir Minja(wa kwanza mstari wa pili) wakiangalia Gwari Maalum la Maadhimisho ya Siku ya Magereza nchini Zambia. Maadhimisho hayo yamefanyika hivi karibuni Septemba 26, 2013 katika Chuo cha Mafunzo ya Maafisa Magereza, Kabwe Zambia
 Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Magereza Nchini Zambia, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Zambia, Mhe. Edgar Lungu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi  mbalimbali wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Zambia pamoja na Viongozi Waandamizi wa Serikali. Wa tatu kulia mbele  ni Kamishna Jenerali wa Magereza Tanzania, John Casmir Minja
Mkuu wa Jeshi la Magereza Zambia, Kamishna wa Magereza Percy Kato( wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja  na Kamishna Jenerali wa Magereza Tanzania, John Casmir Minja(wa tatu kulia) alipotembelea Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza Zambia kufuatia Mwaliko rasmi wa Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Magereza Zambia.Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza.
Read More
Posted in | No comments

dk shein aagana na balozi wa marekani aliyemaliza muda wake wa kazi nchini mhe Alfonso Lenhartd

Posted on 16:50 by Unknown
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Alfonso Lenhartd,alipofika  Ikulu Mjini Zanzibar kumuaga Rais,baada ya kumaliza muda wake wa kazi Nchini.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akizungumza na  Balozi wa Marekani Nchini Tanzania  Alfonso Lenhartd,alipofika leo Ikulu Mjini Zanzibar kumuaga Rais,baada ya kumaliza muda wake wa kazi Nchini.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akibadilishana mawazo na Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Alfonso Lenhartd,baada ya mazungumzo yao alipofika  Ikulu Mjini Zanzibar  kumuaga Rais,akiwa amemaliza  muda wake wa kazi nchini. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.
Read More
Posted in | No comments

KATIBU MKUU UTUMISHI, Bw. GEORGE YAMBESI AFUNGUA MAFUNZO YA MFUMO WA KUSIMAMIA RASILIMALI WATU SEREKALINI (HUMAN CAPITAL MANAGEMENT INFORMATION SYSTEM, HCMIS - LAWSON) KWA WAKURUGENZI NA MAKATIBU

Posted on 16:42 by Unknown
TAWALA WA MIKOA Katibu mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. George Yambesi leo amefungua rasmi mafunzo ya mfumo wa kompyuta wa kusimamia rasilimali watu Serekalini, kwa Makatibu Tawala wa mikoa (RAS) na Wakurugenzi (DED) kutoka mikoa na wilaya mbalimbali Tanzania. 
Maofisa hawa wa Serikali wamegawanywa katika makundi na watahudhuria mafunzo hayo kwa siku tatu tatu. Mafunzo hayo yanafanyika katika maabara za kompyuta za Wakala wa Serikali wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (Tanzania Global Learning Agency, TaGLA).
Katibu Mkuu Bw. Yambesi (katikati) akifungua rasmi mafunzo hayo. Kushoto ni Bw. Mlay, mkurugenzi rasilimali watu wizara ya utumishi, na kulia ni Bw. Senkondo, mkurugenzi mkuu, TaGLa. Mafunzo haya yanafuatiwa na mafunzo mengine yaliyotolewa kwa maafisa rasilimali watu wa mikoa, wilaya na taasisi zote za UMMA Tanzania.
Dr. Faisal, Katibu Tawala – Kilimanjaro, akisema neon kwa niaba ya washiriki wa mafunzo.

Mafunzo haya yatawaweza maafisa hawa kuufahamu mfumo wenyewe, kujua jinsi mfumo unavyofanya kazi na  kufahamu jinsi ya kutumia taarifa zilizo kwenye mfumo huu ili kuwawezesha kufanya maamuzi sahihi na kwa haraka.
Washiriki wa mafunzo 
Makatibu Tawala katika picha ya pamoja na mgeni rasmi
Kundi la kwanza la Wakurugenzi katika picha ya pamoja na mgeni rasmi
Kundi la pili la Wakurugenzi katika picha ya pamoja na mgeni rasmi
Read More
Posted in | No comments
Newer Posts Older Posts Home
Subscribe to: Posts (Atom)

Popular Posts

  • tamasha la 32 la sanaa la bagamoyo lawasha moto, Mhe Makala asema utamaduni ni ajira kwa vijana
    NAIBU Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Mhe. Amos Makala amesema Sanaa na Utamaduni nchini itaendelea kuenziwa ili kuwaleta a...
  • wadau farida na paul wameremeta
     Wakila pozi baada ya kumeremeta katika Kanisa la Mtakatifu Petro jijini Dar es salaam kabla ya kwenda kwenye mnuso wao wa nguvu katika hote...
  • WAZIRI DK. NCHIMBI AMTEMBELEA PADRI ALIYEMWAGIWA TINDIKALI HOSPITALI YA MUHIMBILI LEO
    Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akisalimiana na Padri Joseph Monesmo Magamba wa Kanisa la Romani Katoliki Pa...
  • Naibu Spika aongoza Mkutano wa ACP nchini Ubelgiji
    Mhe.Job Ndugai,Mbunge wa Kongwa na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania akiongoza Mkutano wa Kamati ya Mazingira na Jamii cha Umoja wa Mabunge y...
  • Sherehe za kufunga mafunzo katika kikosi cha 842 Kj Mlale Jkt, Songea
      Mkuu wa wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma Mhe Senyi Ngaga kushoto akiangalia shehena ya mahindi ya chakula katika kikosi cha 842 Kj mlale Jkt...
  • barabara ya Mtoni-mbagala ilivyo
  • BACK TO THE SUA SEASON 2 EPISODE 2, KIJENGE, ARUSHA
    YECHU! YECHU! YECHU! HII HAILIPIWI HATA KUMI ARIFU  YAANI KIINGILIO NDO KITU HAMNAGA Pale Pale fasi ya K-JUU mwisho wa daladala mkabala na k...
  • JK ALIPOKUTANA NA WADAU WASHINGTON DC
    Rais wa Tanzania Dr.Jakaya Kikwete alipokutana na mpiganaji SundayShomari wa VOA siku ya Jumatano kwenye ofisi za ubalozi washington Dc. Rai...
  • KATIBU MKUU UTUMISHI, Bw. GEORGE YAMBESI AFUNGUA MAFUNZO YA MFUMO WA KUSIMAMIA RASILIMALI WATU SEREKALINI (HUMAN CAPITAL MANAGEMENT INFORMATION SYSTEM, HCMIS - LAWSON) KWA WAKURUGENZI NA MAKATIBU
    TAWALA WA MIKOA Katibu mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. George Yambesi leo amefungua rasmi mafunzo ya mfumo wa komp...
  • WAZIRI MEMBE AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA KOSOVO
    Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kosovo, Mhe. Enver...

Blog Archive

  • ▼  2013 (500)
    • ►  October (22)
    • ▼  September (478)
      • HIKI HAPA KILIO CHA WANAFUNZI WA UDAKTARI BUGANDO...
      • No title
      • BREKING NYUUZZZZZZ: SERIKALI YA MAREKANI YAFUNGA S...
      • No title
      • NATURAL PRODUCTS FOR your skin
      • SIKU YA UTALII DUNIANI YENYE KAULI MBIU UTALII NA ...
      • President Kikwete sends Congratulatory Message to ...
      • WAKAZI WA KIKUYU KUSINI WAANDAMANA KUPINGA BOMOABO...
      • ngoma azipendazo ankal
      • wadau farida na paul wameremeta
      • ACCT members attend Master Builders South Africa C...
      • magari yanauzwa
      • Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Fedha za Serikali Bw L...
      • Spika Makinda apongeza Mabunge ya Afrika kwa kuong...
      • KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA JOHN CASMIR MINJA AH...
      • dk shein aagana na balozi wa marekani aliyemaliza ...
      • KATIBU MKUU UTUMISHI, Bw. GEORGE YAMBESI AFUNGUA M...
      • Maalim Seif aifunga rasmi Ijtimai ya Kimataifa ili...
      • HOJA YA HAJA: TUIENZI AMANI YETU KWA GHARAMA YOYOT...
      • MWIGULU NCHEMBA KUNDURUMA NDANI YA LONDON UINGEREZA
      • mwenge wa uhuru watua jijini mbeya
      • MBUNGE WA VITI MAALUMU TABORA,MH MUNDE TAMBWE ADHA...
      • JK arejea nyumbani kutoka Canada na Marekani
      • JK alipohudhuria Mkutano wa Kukabiliana na Ujangil...
      • Globu ya Jamii yakuletea Exclusive Intavyuuu na Re...
      • KANYABOYA LINGINE LAIBUKA DAR,WADAU KAENI CHONJO
      • WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU AIPONGEZA VODA...
      • TIMU YA WIZARA YA AFYA YATINGA ROBO FAINALI - SHIMIWI
      • SAGCOT CEO meets with the US journalists
      • Redd’s Miss Tanzania 2013/14 atembelea TBL leo
      • KONGAMANO LA WAZEE WASTAAFU LAFANYIKA ZANZIBAR
      • ufunguzi Mkutano wa Chama cha Kimataifa cha Taasis...
      • AJALI ZAPUNGUA MKOANI IRINGA
      • MWAKALEBELA AMWAGA VIFAA VYA MICHEZO KWA TIMU 13 M...
      • MAALIM SEIF AWATAKA WAISLAM NCHINI KUUNGA NA KUSHI...
      • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA AMIRI J...
      • Japanese Grant for the Food Security Project for U...
      • ACCT members attending Master Builders South Afric...
      • Awamu ya pili ya chakula cha hisani cha Taasisi ya...
      • MHE. MWIGULU NCHEMBA AWAKUNA WENGI DMV.
      • MWENGE WAZINDUA UJENZI WA OFISI YA KATA TANDALA WI...
      • WAZIRI CHIKAWE ATEMBELEA GEREZA KUU LA ISANGA,MKOA...
      • MKUTANO WA CCM CHWAKA UNGUJA
      • TAARIFA YA MSIBA
      • SingTel Group and Samsung partner to enhance mobil...
      • TIC yawahakikishia wawekezaji ushirikiano zaidi
      • DIAMOND ALIVYOWAKUNA MASHABIKI WAKE NDANI YA GOLD ...
      • KAPOTIVE STAR SINGER-S BUKOBA KUWASHA MOTO JIJINI ...
      • TFDA YAENDESHA KAMPENI YA UTUMIAJI WA VYAKULA VILI...
      • Wakazi wa eneo la hifadhi ya Ngorongoro wapokea ch...
      • AZANIA BANK YACHANGIA MIFUKO 100 YA SARUJI SHULE Y...
      • United States 2015 Diversity Visa Program Now Open
      • OPERESHENI KIMBUNGA AWAMU YA PILI YASHIKA KASI KAT...
      • mdau mugassa mwenda ahojiwa na BBC kwa kufurahishw...
      • Airtel yawanoa maafisa waTRA jinsi ya kulipia ada ...
      • NAIBU WAZIRI FEDHA AKAGUA UJENZI WA BARABARA VISIW...
      • 2013 Young Achievers Awards Nomination Open!
      • No title
      • IN LOVING MEMORY of DORA HOSEA TALAWA 1ST ANNIVESSARY
      • ngoma azipendazo ankal
      • TAARIFA YA MSIBA WA MAMA ROSE HEINRICH SANGIWA MATAJI
      • FRANSIC MIYEYUSHO AMTWANGA SADIK MOMBA KWA POINTI
      • Waziri Membe akutana kwa mazungumzo na Wafanyakazi...
      • Mahojiano ya JK na radio ya umoja wa mataifa, New ...
      • J&M Virgo washusha mali mpya
      • Daktari wa Rais Kikwete kupima afya na kuwapa lese...
      • MWENGE WA UHURU WATUA MAKETE
      • Swali la kizushi: Je ni mkono upi unaofaa kuvalia ...
      • No title
      • No title
      • introducing Mchaga na pesa by KiwaStrond ft. Banx
      • bwawa la maini oye! Suarez arudi na kupiga bee kat...
      • HARAMBEE KUCHANGIA CHAMA CHA MAPINDUZI MKOA WA KUS...
      • introducing 'Ni Noma' by Go Getta of the night cra...
      • MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA SERIKALI YA MAPINDUZI ...
      • Ubalozi wetu zambia na wajisiriamali wa Tanzania w...
      • Grace aikaeli Mbowe na mumewe wafariki kwa ajali ...
      • Simba yaibanjua Ruvu JKT 2-0 leo neshno
      • KANISA LA TGMIT LAFANYA IBADA MAALUMU KUIOMBEA AMA...
      • ZUMBA KUKWE AMSHINDA HAMADUU MWALIMU KWA KO RAUNDI...
      • TANZIA: Msiba wa Bi ROSE HENRISCH SANGIWA MATAJI
      • Sherehe za kufunga mafunzo katika kikosi cha 842 ...
      • Benki ya posta Tanzania tawi la Songea yaipiga jek...
      • GLOBAL LANGUAGE NETWORK (GLN) ILIYOFANYIKA WASHING...
      • TAMASHA LA SANAA BAGAMOYO NI KWELI KWAMBA LIMEPOTE...
      • No title
      • Tanzanian Minister of Defence Meets Governor of So...
      • UPANUZI WA BARABARA YA BENDERA TATU HADI KAMATA KU...
      • MISS UTALII TANZANIA KUTANGAZA NYATI WA AJABU NA ...
      • Cheka unenepe
      • WAFANYAKAZI WA IDARA MBALI MBALI ZA SERIKALI WACHU...
      • Kiwanda cha kuzalisha malighafi za kutengeneza Gil...
      • MAMA SALMA KIKWETE APEWA URAIA WA HIARI WA JIMBO L...
      • MKUTANO WA SIKU TATU WA MAOFISA WA JUU WA JESHI LA...
      • NBC YATENGA SIKU MAALUMU KUWASHUKURU WATEJA WAO
      • Serikali yabariki tamasha la Utamaduni Handeni
      • Matukio zaidi ya Mhe. Rais Kikwete alipolihutubia ...
      • ngoma azipendazo ankal
      • chemsha bongo...
      • cassim mganga akitumbuiza kwenye tamasha la fiesta...
Powered by Blogger.

About Me

Unknown
View my complete profile