Na. Catherine Sungura (MOHSW),Dodoma
Timu ya Mpira wa miguu ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, leo imefanikiwa kuingia robo fainali baada ya kuitoa Timu ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali kwa Mikwaju 3-1 mjini hapa.
Mchezo ulikuwa wa kukamiana kati ya timu hizo mbili zilizoweza kutoka sare bila ya kufungana hadi mwisho wa mchezo huo. Baada ya mchezo kuisha mwamuzi wa mchezo huo aliamuru timu hizo zipige mikwaju ambayo iliweza kuwatoa kimasomaso timu hiyo ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Ukaguzi ndio iliyokuwa ya kwanza kuanza kupiga mikwaju hiyo ambapo golikipa wa Afya Said Kidamba aliweza kuzuia mipira mitatu kati ya minne iliyopigwa kwenye nyavu za Afya.
Afya wao walifanikiwa kuziona nyavu za wapinzani wao katika penati zote tatu walizozipiga. Wachezaji waliyoiwezesha afya kuingia robo fainali alikuwa Patrick Mangungulu penati ya kwanza, Selemani Juma penati ya pili na penati ya tatu na iliyoamsha shamrashamra kiwanjani hapo ni ile iliyopigwa na Bakari Magoma.
Katika mchezo huo uliochezwa kwenye kiwanja cha Jamburi, mwamuzi aliweza kutoa kadi za njano nne kwa timu hizo ambapo Afya ilipata kadi moja kwa mchezaji wake Emmanuel Zunda kipindi cha kwanza na Ukaguzi zilitolewa kwa George Mlelwa na Abdul Athumani kipindi cha kwanza na kipindi cha pili dakika ya nane ilienda kwa Ally Mpondo.
Timu ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii (kulia) wakisalimia watazamaji kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma kwenye mpambano wao dhidi ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali (walovaa jezi nyeupe).Katikati ni waamuzi wa mpambano huo. Afya ilishinda 3-1.
Penati ya tatu na ya mwisho iliyowawezesha timu ya afya kutinga robo fainali ilivyopigwa na mchezaji Bakari Magoma.
achezaji wa Afya na Ustawi wa Jamii wakiwa kwenye picha ya pamoja kiwanjani hapo mara baada ya timu yao kuilaza timu ya Ukaguzi kwa mabao 3-1.
0 comments:
Post a Comment