Kaimu Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Iringa Inspekta Ahimidiwe Msangi akiwa katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya samora mkoani Iringa.(picha na denis mlowe)
======= ========== =========
AJALI ZAPUNGUA MKOANI IRINGA
Na Denis Mlowe, Iringa
TAKWIMU za ajali za vifo na majeruhi kwa ajali za magari kwa kipindi cha miezi nane cha mwaka 2013 mkoani Iringa zimepungua kutoka kwa ajali zote zilikuwa 76 kwa mwaka 2012 hadi 69 kwa mwaka huu ikiwa ni ongezeka la sifuri pungufu ya ajali 7 sawa na asilimia 9 kwa kipindi cha miezi nane.
Akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani mwishoni mwa wiki Kaimu Mkuu wa Usalama Barabarani Mkoa wa Iringa Inspekta Ahimidiwe Msangi alisema ajali za vifo zilikuwa 62 kwa mwaka 2012 mwaka 2013 kulitokea ajali 45 zikipungua kwa ajali 17 sawa na asilimia 27.
Msangi alisema ajali za majeruhi zimeongezeka kutoka ajali 14 mwaka jana hadi kufikia ajali 24 likiwa ni ongezeko la ajali 10 sawa na asilimia 41 za ajali kwa kipindi cha miezi nane ya mwaka wa 2012 na 2013
Alisema katika ajali hizo watu 69 walifariki kwa kipindi cha miezi nane cha mwaka jana, mwaka huu watu waliofariki 62 ikiwa pungufu ya watu 7 waliofariki sawa na asilimia 10.
Aidha alisema kutokana na ajali hizo waliokutwa na makosa wamewezeshwa serikali kupata shilingi milioni 465.2 zaidi ukilinganisha na pato la mwaka jana shilingi milioni 292.3 sawa na ongezeko la asilimia 37.
Akizungumzia ajali za pikipiki kwa mkoa wa Iringa kwa kipindi cha kuanzia Januari 2012 hadi hadi Agosti mwaka huu Msangi alisema zimeongezeka kwa asilimia 69 kwa ajali zote.
Alisema matukio ya ajali kwa kipindi cha Januari hadi Agosti mwaka 2012 ajali zote zilikuwa 8, ajali za vifo zilikuwa 6, ajali za majeruhi zilikuwa 2 na kati ajali hizo watu waliokufa ni 7 na majeruhi walikuwa 5 kutokana na ajali hizo.
“Kipindi cha Januari hadi Agosti mwaka huu ajali za boda boda zimeongezeka kutoka 8 hadi 26 kwa ajali zote sawa na ongezeko la ajali 18 sawa na asilimia 69, ajali za vifo zimeongezeka kutoka 6 hadi 20 ongezeko la ajali 14 sawa na asilimia 70 na ajali za majeruhi zimeongezeka kutoka 2 hadi 6 sawa na ongezeko la ajali 4 sawa na asilimia 67” alisema Msangi
Alisema watu waliokufa kwa kipindi cha mwaka jana walikuwa 7 na kipindi cha mwaka huu watu 12 wamefariki kutokana na ajali hizo ikiwa ongezeko la watu 7 sawa na asilimia 5.
Msangi alisema majeruhi walikuwa watu 5 kipindi cha Januari hadi Agosti mwaka jana kwa huuu ajali zimeongezeka na kufikia idadi ya ajali 12 sawa na ongezeka la ajali 7 ikiwa ni asilimia 58.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Usalama barabarani Mkoani Iringa Salim Asas Abri aliwataka madereva kuwa makini katika uendeshaji wa vyombo vya moto na kufikiria zaidi taifa linapoteza nguvu kazi kutokana na ajali za kizembe ambazo zinaweza kuzuilika.
Kauli mbiu ya mwaka huu ya wiki ya kwenda kwa usalama barabani ilikuwa ‘Usalama Barabarani Vinaanza Mimi,wewe na Sisi sote’.
0 comments:
Post a Comment