50 Bing Coupons

  • Subscribe to our RSS feed.
  • Twitter
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • Facebook
  • Digg

Monday, 30 September 2013

HIKI HAPA KILIO CHA WANAFUNZI WA UDAKTARI BUGANDO KWA SERIKALI YA RAIS KIKWETE

Posted on 23:20 by Unknown

Rais wa Serikali ya Wanafunzi Madaktari wa Chuo cha Bugando (CUHASSO) Musa Leonard Mdede (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa tamko kwa niaba ya wanachuo kuiomba Serikali kutoa udhamini wa ada kwa asilimia 100 kwani wanafunzi wengi wanashindwa kumaliza masomo yao kutokana na kujikita kwenye shughuli za usakaji pesa kwaajili ya malipo, nazo ada zikiendelea kupanda kila misimu huku Serikali ikiendelea kutoa ufadhili kwa asilimia ileile.

"Tunaiomba Serikali kuongeza kiwango cha ufadhili ili wanafunzi au vijana walio na nia ya kusoma fani ya udaktari wakiwa wanalenga kuokoa maisha ya watanzania watimize ndoto zao. Tunatambua kuwa nchi yetu ina upungufu wa asilimia 60 ya madaktari wa sekta ya afya"

"Na kwa takwimu daktari mmoja anahudumia zaidi ya wagonjwa 33,000 kutokana na idadi ya watanzania wote, sasa kuendelea kuwa na vijana wanaoshindwa kuendelea na masomo ya sekta ya afya kwa sababu ya kukosa karo, nikurudi nyuma na kamwe malengo hayatotimia" Alisema Musa Leonard Mdede

Makamu wa Rais wa Serikali ya Wanafunzi Madaktari wa Chuo cha Bugando (CUHASSO) Atukuzwe Mordekai Gwihangwe (katikati) akitoa ufafanuzi jinsi ada kubwa inayotozwa kwa wanafunzi inavyokwamisha malengo ya wanafunzi wa sekta ya Afya nchini hali inayopelekea serikali kukosa wataalamu wa kutosha. Kushoto ni Rais wa CUHASSO Musa Leonard Mdede na kushoto ni Benjamin Thomas.



Ndugu wana habari,napenda kuchukua nafasi hii kama Rais wa serikali ya wanafunzi chuo kikuu katoliki cha sayansi ya Afya na Tiba(CUHAS-Bugando) kwa niaba ya wanazuoni wote wa chuo hiki na kwa niaba ya wanafunzi wa sekta ya Afya wa vyuo vikuu vyote visivyokua vya umma nchini(yaani vyuo vikuu vikuu vyote vya fani ya afya vinavyomilikiwa na mashirika ya dini na mashirika ya watu binafsi).Kuweza kueleza kilio chetu kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na vyombo mbalimbali vya kiserikali vyenye mamlaka ya kusimamia Elimu ya juu na vyuo vikuu nchini.

I:DHANA YA ASILIMIA MIA MOJA YA MKOPO.Watanzania wengi  wakiwemo ndugu na jamaa wa karibu wanaotugharamikia katika masomo yetu wanaelewa kwamba mwanafunzi anayesoma fani za Afya kama Udakatari,Ufamasia,Uuguzi na nyinginezo kama hizo analipiwa kila kitu na serikali kupitia bodi ya mikopo kwa hiyo hahitaji msaada wowote wa kifedha kutoka kwa wazazi au walezi kwa kua anjitosheleza kwa kila kitu.Dhana ambayo kwa mwanafunzi anayesoma katika chuo kikuu kisichokua cha Umma ni tofauti kabisa.Kwa kua asilimia mia moja inayoongelewa ni kama asilimia hamsini tu ya karo zinazotozwa katika vyuo hivi.

Wanafunzi wote wa vyuo hivi vya fani ya Afya visivyokua vya umma tumekua tukipokea kiasi cha shilingi za kitanzania milioni mbili na laki sita tu(Tsh.2,600,000/=)  toka bodi ya mikopo kama mkopo kwa ajili ya Ada.Kiwango hiki kipo hivo toka wakati huo ambapo katika vyuo hivi Ada ilikua inatozwa kwa kiwango hicho.Ni takribani miaka sita sasa kiwango hiki kimebakia kama kilivo bila kuongezeka.Wakati kutokana na kuongezeka kwa gharama za uendeshaji wa taasisi hizi.

Ada zimekua zikiongezeka mwaka hadi mwaka na sasa kufikia takribani milioni nne,na zaidi kama karo katika vyuo hivi mbalimbali Ikiwa ina maana kwamba kiasi kinachobaki baada ya Tsh.2,600,000/= kutolewa kama mkopo mwanafunzi mwenyewe inatakiwa ajilipie pamoja na gharama zingine ambazo si sehemu ya karo zinazohitajika kutolewa.Wanafunzi wengi katika vyuo hivi wanasoma na kuishi katika mazingira magumu sana kwa kua gharama anazotakiwa kuchangia binafsi ni kubwa kiasi cha kuwalemea wanafunzi wengi ambao wengi wetu ni watoto wa wakulima ila tukiwa na haki ya kupata Elimu bila kujalisha hali ya uchumi wa familia zetu

.CHANGAMOTO;hali hii imepelekea wanafunzi wengi wanaochaguliwa kushindwa kujiunga na vyuo hivi kwa kushindwa kumudu gharama hizi,lakini pia imepelekea wanafunzi wengi kupoteza mda wao mwingi katika kufanya vibarua ili kupata kiasi cha kumalizia ada ambayo imepelekea ufaulu wao kushuka na wengine kupoteza kabisa nafasi ya kuendelea na masomo.

OMBI LETU KWA SERIKALI;kwa kua tumejiunga na vyuo hivi kwa mfumo halali wa Tume ya vikuu Tanzania(TCU) ambao haukuangalia hali ya kiuchumi ya familia zetu kama tutamudu au hatutamudu kulipa gharama hizi,kwa kua tulijiunga na vyuo hivi kwani tulikua na vigezo vya kusoma fani hizi kama wenzetu wanaosoma katika vyuo vikuu vya umma na hata zaidi na kwa kua tukihitimu sisi wote yaani wenzetu wanaosoma vyuo vikuu vya umma na sisi tunaosoma vyuo vikuu visivyokua vya umma tunakwenda kuhudumia na kuokoa uhai wa watanzania walewale.

Tunaiomba serikali iongeze kiwango hiki tunachopewa kama mkopo kwa ajili ya ada,ili hiyo Asilimia mia moja inayosemwa iwe na maana kwetu kwa kua kwa sasa ni kama nusu tu.Wengi wanashindwa kujiunga na vyuo hivi kwa kushindwa kumudu gharama hizo.Katika nchi yenye upungufu wa 60% ya madaktari na wataalamu afya kwa ujumla,pia katika nchi ambayo daktari mmoja anahudumia wagonjwa zaidi ya 33 elfu.Si vema kuona vijana wenye dhamira na nia thabiti ya kuokoa maisha ya watanzania wanashindwa kutimiza ndoto hizo za kua wataalamu wa Afya ati kwa kushindwa kulipa karo.

Tume ya vyuo vikuu Tanzania(TCU):Upandishwaji Ada katika vyuo vikuu visivyokua vya umma usiofuata utaratibu na Kile kinchojulikana kama “List of Approved programme fees” ikiainisha gharama za ada zinazotozwa katika vyuo vikuu vyote nchini.Tume vya vikuu Tanzania imepewa mamlaka kisheria kwa mujibu wa sheria ya vikuu No.7,2005.Kusimamia kuanzia udahili na uendeshaji wa vyuo vikuu vyote nchini vya umma na visivyokua vya umma.Central Admission system
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII;Institute of Health and Allied Health sciences.

Kumekuwa na changamoto kubwa katika gharama za ada, chakula na makazi kwa wanafunzi wa stashahada katika vyuo vya Afya hasa vile vya binafsi ambapo gharama za uchangiaji zinazidi kuwa kubwa ikizingatiwa kuwa wanafunzi hao hutejigemea kiasi kikubwa na kuwa serikali kupitia wizara ya afya imekua ikitoa fedha kwa ajiri ya wanafunzi hao.

OMBI LETU:-Tunaiomba Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii kuweka wazi ni kiasi gani inachangia kwa kila mwanafunzi mmojammoja wa stashada katika vyuo vya afya kwa kueleza mchanganuo halisi ili kuwawezesha wanafunzi hao kutambua ni kwa kiasi gani Serikali kupitia wizara ya Afya na ustawi wa jamii inachangia kama ulivyo utaratibu wa bodi ya mikopo kwa wanafunzi wa shahada .

 Vilevile kumekuwa na changamoto ya mabadiliko ya gharama za ada kwa wanafunzi wa stashahada katika vyuo vya afya na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wanafunzi hao hivyo Tunaiomba Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii Kutoa gharama halisi ambazo wanafunzi wa stashada katika vyuo vya Afya watapaswa kuchangia katika vyuo mbalimbali ikiwemo vile vya binafsi.

Kulingana na changamoto mbalimbali zinazozidi kujitokeza kwa wanafunzi wa stashahada katika vyuo vya afya, Tunaiomba Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii Kuboresha  mfumo wa uwezeshaji kwa wanafunzi wa stashada na kuweka mfumo na taratibu zitakazosimamia mabadiliko ya ada katika vyuo mbalimbali vya Afya ili kuweza kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza vyuoni hasa vya binafsi.

Kumekuwa na uchakavu wa miundombinu inayomilikiwa na wizara ya Afya katika vyuo vya afya na hivyo kupunguza ufanisi wa masomo kwa wanafunzi hivyo Tunaiomba Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii Kuboresha miundombinu mbalimbali inayomilikiwa na wizara ya afya katika vyuo vya Afya vinavyotoa stashahada.
Email ThisBlogThis!Share to XShare to Facebook
Posted in | No comments
Newer Post Older Post Home

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to: Post Comments (Atom)

Popular Posts

  • tamasha la 32 la sanaa la bagamoyo lawasha moto, Mhe Makala asema utamaduni ni ajira kwa vijana
    NAIBU Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Mhe. Amos Makala amesema Sanaa na Utamaduni nchini itaendelea kuenziwa ili kuwaleta a...
  • wadau farida na paul wameremeta
     Wakila pozi baada ya kumeremeta katika Kanisa la Mtakatifu Petro jijini Dar es salaam kabla ya kwenda kwenye mnuso wao wa nguvu katika hote...
  • WAZIRI DK. NCHIMBI AMTEMBELEA PADRI ALIYEMWAGIWA TINDIKALI HOSPITALI YA MUHIMBILI LEO
    Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akisalimiana na Padri Joseph Monesmo Magamba wa Kanisa la Romani Katoliki Pa...
  • Naibu Spika aongoza Mkutano wa ACP nchini Ubelgiji
    Mhe.Job Ndugai,Mbunge wa Kongwa na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania akiongoza Mkutano wa Kamati ya Mazingira na Jamii cha Umoja wa Mabunge y...
  • Sherehe za kufunga mafunzo katika kikosi cha 842 Kj Mlale Jkt, Songea
      Mkuu wa wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma Mhe Senyi Ngaga kushoto akiangalia shehena ya mahindi ya chakula katika kikosi cha 842 Kj mlale Jkt...
  • barabara ya Mtoni-mbagala ilivyo
  • BACK TO THE SUA SEASON 2 EPISODE 2, KIJENGE, ARUSHA
    YECHU! YECHU! YECHU! HII HAILIPIWI HATA KUMI ARIFU  YAANI KIINGILIO NDO KITU HAMNAGA Pale Pale fasi ya K-JUU mwisho wa daladala mkabala na k...
  • JK ALIPOKUTANA NA WADAU WASHINGTON DC
    Rais wa Tanzania Dr.Jakaya Kikwete alipokutana na mpiganaji SundayShomari wa VOA siku ya Jumatano kwenye ofisi za ubalozi washington Dc. Rai...
  • KATIBU MKUU UTUMISHI, Bw. GEORGE YAMBESI AFUNGUA MAFUNZO YA MFUMO WA KUSIMAMIA RASILIMALI WATU SEREKALINI (HUMAN CAPITAL MANAGEMENT INFORMATION SYSTEM, HCMIS - LAWSON) KWA WAKURUGENZI NA MAKATIBU
    TAWALA WA MIKOA Katibu mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. George Yambesi leo amefungua rasmi mafunzo ya mfumo wa komp...
  • WAZIRI MEMBE AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA KOSOVO
    Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kosovo, Mhe. Enver...

Blog Archive

  • ▼  2013 (500)
    • ►  October (22)
    • ▼  September (478)
      • HIKI HAPA KILIO CHA WANAFUNZI WA UDAKTARI BUGANDO...
      • No title
      • BREKING NYUUZZZZZZ: SERIKALI YA MAREKANI YAFUNGA S...
      • No title
      • NATURAL PRODUCTS FOR your skin
      • SIKU YA UTALII DUNIANI YENYE KAULI MBIU UTALII NA ...
      • President Kikwete sends Congratulatory Message to ...
      • WAKAZI WA KIKUYU KUSINI WAANDAMANA KUPINGA BOMOABO...
      • ngoma azipendazo ankal
      • wadau farida na paul wameremeta
      • ACCT members attend Master Builders South Africa C...
      • magari yanauzwa
      • Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Fedha za Serikali Bw L...
      • Spika Makinda apongeza Mabunge ya Afrika kwa kuong...
      • KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA JOHN CASMIR MINJA AH...
      • dk shein aagana na balozi wa marekani aliyemaliza ...
      • KATIBU MKUU UTUMISHI, Bw. GEORGE YAMBESI AFUNGUA M...
      • Maalim Seif aifunga rasmi Ijtimai ya Kimataifa ili...
      • HOJA YA HAJA: TUIENZI AMANI YETU KWA GHARAMA YOYOT...
      • MWIGULU NCHEMBA KUNDURUMA NDANI YA LONDON UINGEREZA
      • mwenge wa uhuru watua jijini mbeya
      • MBUNGE WA VITI MAALUMU TABORA,MH MUNDE TAMBWE ADHA...
      • JK arejea nyumbani kutoka Canada na Marekani
      • JK alipohudhuria Mkutano wa Kukabiliana na Ujangil...
      • Globu ya Jamii yakuletea Exclusive Intavyuuu na Re...
      • KANYABOYA LINGINE LAIBUKA DAR,WADAU KAENI CHONJO
      • WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU AIPONGEZA VODA...
      • TIMU YA WIZARA YA AFYA YATINGA ROBO FAINALI - SHIMIWI
      • SAGCOT CEO meets with the US journalists
      • Redd’s Miss Tanzania 2013/14 atembelea TBL leo
      • KONGAMANO LA WAZEE WASTAAFU LAFANYIKA ZANZIBAR
      • ufunguzi Mkutano wa Chama cha Kimataifa cha Taasis...
      • AJALI ZAPUNGUA MKOANI IRINGA
      • MWAKALEBELA AMWAGA VIFAA VYA MICHEZO KWA TIMU 13 M...
      • MAALIM SEIF AWATAKA WAISLAM NCHINI KUUNGA NA KUSHI...
      • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA AMIRI J...
      • Japanese Grant for the Food Security Project for U...
      • ACCT members attending Master Builders South Afric...
      • Awamu ya pili ya chakula cha hisani cha Taasisi ya...
      • MHE. MWIGULU NCHEMBA AWAKUNA WENGI DMV.
      • MWENGE WAZINDUA UJENZI WA OFISI YA KATA TANDALA WI...
      • WAZIRI CHIKAWE ATEMBELEA GEREZA KUU LA ISANGA,MKOA...
      • MKUTANO WA CCM CHWAKA UNGUJA
      • TAARIFA YA MSIBA
      • SingTel Group and Samsung partner to enhance mobil...
      • TIC yawahakikishia wawekezaji ushirikiano zaidi
      • DIAMOND ALIVYOWAKUNA MASHABIKI WAKE NDANI YA GOLD ...
      • KAPOTIVE STAR SINGER-S BUKOBA KUWASHA MOTO JIJINI ...
      • TFDA YAENDESHA KAMPENI YA UTUMIAJI WA VYAKULA VILI...
      • Wakazi wa eneo la hifadhi ya Ngorongoro wapokea ch...
      • AZANIA BANK YACHANGIA MIFUKO 100 YA SARUJI SHULE Y...
      • United States 2015 Diversity Visa Program Now Open
      • OPERESHENI KIMBUNGA AWAMU YA PILI YASHIKA KASI KAT...
      • mdau mugassa mwenda ahojiwa na BBC kwa kufurahishw...
      • Airtel yawanoa maafisa waTRA jinsi ya kulipia ada ...
      • NAIBU WAZIRI FEDHA AKAGUA UJENZI WA BARABARA VISIW...
      • 2013 Young Achievers Awards Nomination Open!
      • No title
      • IN LOVING MEMORY of DORA HOSEA TALAWA 1ST ANNIVESSARY
      • ngoma azipendazo ankal
      • TAARIFA YA MSIBA WA MAMA ROSE HEINRICH SANGIWA MATAJI
      • FRANSIC MIYEYUSHO AMTWANGA SADIK MOMBA KWA POINTI
      • Waziri Membe akutana kwa mazungumzo na Wafanyakazi...
      • Mahojiano ya JK na radio ya umoja wa mataifa, New ...
      • J&M Virgo washusha mali mpya
      • Daktari wa Rais Kikwete kupima afya na kuwapa lese...
      • MWENGE WA UHURU WATUA MAKETE
      • Swali la kizushi: Je ni mkono upi unaofaa kuvalia ...
      • No title
      • No title
      • introducing Mchaga na pesa by KiwaStrond ft. Banx
      • bwawa la maini oye! Suarez arudi na kupiga bee kat...
      • HARAMBEE KUCHANGIA CHAMA CHA MAPINDUZI MKOA WA KUS...
      • introducing 'Ni Noma' by Go Getta of the night cra...
      • MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA SERIKALI YA MAPINDUZI ...
      • Ubalozi wetu zambia na wajisiriamali wa Tanzania w...
      • Grace aikaeli Mbowe na mumewe wafariki kwa ajali ...
      • Simba yaibanjua Ruvu JKT 2-0 leo neshno
      • KANISA LA TGMIT LAFANYA IBADA MAALUMU KUIOMBEA AMA...
      • ZUMBA KUKWE AMSHINDA HAMADUU MWALIMU KWA KO RAUNDI...
      • TANZIA: Msiba wa Bi ROSE HENRISCH SANGIWA MATAJI
      • Sherehe za kufunga mafunzo katika kikosi cha 842 ...
      • Benki ya posta Tanzania tawi la Songea yaipiga jek...
      • GLOBAL LANGUAGE NETWORK (GLN) ILIYOFANYIKA WASHING...
      • TAMASHA LA SANAA BAGAMOYO NI KWELI KWAMBA LIMEPOTE...
      • No title
      • Tanzanian Minister of Defence Meets Governor of So...
      • UPANUZI WA BARABARA YA BENDERA TATU HADI KAMATA KU...
      • MISS UTALII TANZANIA KUTANGAZA NYATI WA AJABU NA ...
      • Cheka unenepe
      • WAFANYAKAZI WA IDARA MBALI MBALI ZA SERIKALI WACHU...
      • Kiwanda cha kuzalisha malighafi za kutengeneza Gil...
      • MAMA SALMA KIKWETE APEWA URAIA WA HIARI WA JIMBO L...
      • MKUTANO WA SIKU TATU WA MAOFISA WA JUU WA JESHI LA...
      • NBC YATENGA SIKU MAALUMU KUWASHUKURU WATEJA WAO
      • Serikali yabariki tamasha la Utamaduni Handeni
      • Matukio zaidi ya Mhe. Rais Kikwete alipolihutubia ...
      • ngoma azipendazo ankal
      • chemsha bongo...
      • cassim mganga akitumbuiza kwenye tamasha la fiesta...
Powered by Blogger.

About Me

Unknown
View my complete profile