KAMANDA wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Misungwi Mkoa wa Mwanza, John Lupemba akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Jimbo la Chwaka Wilaya ya Kati Unguja , ambapo alimwakilisha Ridhwan Kikwete .
VIONGOZI mbali mbali wa Chama cha Mapinduzi (CCM) waliohudhuria mkutano wa hadhara katika Jimbo la Chwaka Wilaya ya Kati Unguja wakimsikiliza mgeni Rasmi Kamanda wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Wilaya ya Misungwi Mkoa wa Mwanza, John Lupemba (hayupo pichani) wakati akihutubia mkutano huo uliofanyika katika viwanja vya Chuo cha Uongozi wa Fedha Chwaka.
WANACHAMA wapya 126 waliojiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) ambapo 61 walitoka chama cha CUF na 65 wanachama wapya wa CCM wakila kiapo baada ya kukabidhiwa kadi za chama hicho na Kamanda wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Wilaya ya Misungwi Mkoa wa Mwanza, John Lupemba katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Chuo cha uongozi wa fedha Chwaka Wilaya ya Kati Unguja.
0 comments:
Post a Comment