Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Juma Ali Simai akiweka jiwe la msingi ujenzi wa ofisi ya kata ya Tandala.
afisa mtendaji kata ya Tandala Ambele Sanga akisoma taarifa ya ujenzi huo
Na Edwin Moshi, Makete
Ujenzi wa ofisi ya kata ya Tandala wilayani Makete mkoani Njombe umewekwa jiwe la msingi na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Juma Ali Simai huku akisisitiza wananchi kutokatishwa tamaa na baadhi ya viongozi wanaowataka wasichangie shughuli za maendeleo
Amesema kumekuwepo na baadhi ya viongozi ambao hawaitakii mema nchi hii kwa kuwadanganya wananchi wasishiriki kuchangia shughuli za maendeleo kwa madai kuwa serikali ndiyo pekee yenye jukumu hilo hivyoa wasubiri hadi itakavyowaletea
Jengo hilo lililogharimu kiasi cha shilingi milioni 36,112,400/= linatarajiwa kutoa huduma bora kwa wananchi wa kata hiyo ukizingatia kata hiyo ni miongoni mwa kata mpya wilayani hapo
Awali akisoma taarifa ya ujenzi huo afisa mtendaji wa kata ya Tandala Ambele Sanga amesema ujenzi huo umeshirikisha wananchia ambapo wananchi wamechangia sh. 16,112,400/= na kiasi kilichosalia cha sh. 20,000,000/= kimetolewa na halmashauri ya wilaya ya Makete
Ujenzi huo ulioanza Desemba 12,2013 unaendelea vizuri
0 comments:
Post a Comment