TAWALA WA MIKOA Katibu mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. George Yambesi leo amefungua rasmi mafunzo ya mfumo wa kompyuta wa kusimamia rasilimali watu Serekalini, kwa Makatibu Tawala wa mikoa (RAS) na Wakurugenzi (DED) kutoka mikoa na wilaya mbalimbali Tanzania.
Maofisa hawa wa Serikali wamegawanywa katika makundi na watahudhuria mafunzo hayo kwa siku tatu tatu. Mafunzo hayo yanafanyika katika maabara za kompyuta za Wakala wa Serikali wa Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (Tanzania Global Learning Agency, TaGLA).
Katibu Mkuu Bw. Yambesi (katikati) akifungua rasmi mafunzo hayo. Kushoto ni Bw. Mlay, mkurugenzi rasilimali watu wizara ya utumishi, na kulia ni Bw. Senkondo, mkurugenzi mkuu, TaGLa. Mafunzo haya yanafuatiwa na mafunzo mengine yaliyotolewa kwa maafisa rasilimali watu wa mikoa, wilaya na taasisi zote za UMMA Tanzania.
Dr. Faisal, Katibu Tawala – Kilimanjaro, akisema neon kwa niaba ya washiriki wa mafunzo.
Mafunzo haya yatawaweza maafisa hawa kuufahamu mfumo wenyewe, kujua jinsi mfumo unavyofanya kazi na kufahamu jinsi ya kutumia taarifa zilizo kwenye mfumo huu ili kuwawezesha kufanya maamuzi sahihi na kwa haraka.
Washiriki wa mafunzo
Makatibu Tawala katika picha ya pamoja na mgeni rasmi
Kundi la kwanza la Wakurugenzi katika picha ya pamoja na mgeni rasmi
Kundi la pili la Wakurugenzi katika picha ya pamoja na mgeni rasmi
0 comments:
Post a Comment