Ankal salama?
Naomba unisaidie msaada tutani.
Niulizie kwa wadau je ni mkono upi unaofaa kuvaliwa saa ya mkononi?
Nauliza hivyo kwa sababu juzi juzi nimenunua bonge moja la saa na kuivaa mkono wa kulia.
Mai waifu wangu na majamaa kibao wakanicheka sana kuwa mwanaume anatakiwa kuvaa saa mkono wa kushoto. Nilipoenda kazini kuna waliosema mkono wa kulia unafaa na wengine wakabakia kudai kwa mwanaume ni mkono wa kushoto na kwa mwanamke ni mkono wa kulia. Yaani nimechanganyikiwa.
Ati jamani wadau nivae saa yangu mkono upi na kwa sababu gani?
Ni hayo tu Ankal
Email yangu kapuni maana najua
nitazodolewa hapa hadi nikome...
Mdau Unyamwezini
0 comments:
Post a Comment