50 Bing Coupons

  • Subscribe to our RSS feed.
  • Twitter
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • Facebook
  • Digg

Monday, 30 September 2013

HOJA YA HAJA: TUIENZI AMANI YETU KWA GHARAMA YOYOTE ILE

Posted on 16:13 by Unknown
Barua ya wazi kwa Wapendwa Watanzania wenzangu

Kwanza nianze kwa kuwapa pole jirani zetu na ndugu zetu wakenya kwa tukio baya kabisa la ujasusi lilotokea mwisho wa juma lilopita. Ni jambo ya kusikitisha na lenye kujaa na maswali mwengi ya kujiuliza. Imefika mahali kuna watu hawathamini utu wala maisha ya binadamu mwenzake. Poleni sana ndugu zetu na tuko pamoja.
Mambo ya kujifunza:
1.     Mwenzako akinyolewa, na wewe anza kutia maji. Ninasema hivi kwasababu tusidhani kwa sababu tupo mbali na Somalia basi tuko salama. La hasha, hawa jamaa hawalali, na chokochoko  na dalili tulianza kuziona mapema kabisa. Tumeona  matukio ya mabomu na tindikali, na jana bomu kurushwa Zanzibar. Inatisha kabisa. Nashauri vyombo vya usalama vifunguke macho na viache kufanya mabo kwa mazoea, tubadilike na tujifunze mbinu mpya za kukabiliana na ugaidi. Tusione aibu kuomba msaada wa kitaalamu na vifaa kutoka kwa wenzetu waliotutangulia kiitelijinsia
2.     Somo la uzalendo ndiyo mahali pake hapa. Mtu mzalendo hawezi kuiuza nchi yake kwa ajili ya njaa zake. Kutokana naa umbwe la umasikini kuongezeka, inakuwa rahisi sana mtu kukubali kushirikiana na watu wenye nia mbaya kuumiza nchi yetu. Hizo ni tama na badala ya kutatua matatizo inazidisha maana:
a.     Utalii utakufa
b.     Wawekezaji wataogopa kuja kuwekeza
c.      Hata vile vichache tulivyo navyo vitahujumiwa
d.     Uhai wa kila mmoja wetu utawekwa rehani pamoja na aliyechonga line
e.     Kisiwa cha amani kitatoweka (Mungua tupitishie mbali)
f.       Tutaanza kunyoosheana vidole kati ya kabila na kabila, dini na dini, bara na visiwani. Hatutakuwa wamoja. Lazima tutaanza kutafuta mchawi
g.     Hata wenye mali hawataishi kwa amani,maana wao ndiyo watakaoviziwa kwanza; kama tulivyoona Westgate
Nini cha kufanya:
1.     Nakumbuka enzi za Mwalimu kulikuwa na mabalozi wa nyumba kumikumi. Hawa watu walikuwa na nguvu sana kwenye eneo lao. Japo ilikuwa sera ya CCM,lakini kutokana na vyama vingi, basi tuifanye sera ya Taifa. Nakumbuka wakati wa utoto wetu ukipata mgeni lazima utoe taarifa kwa mjumbe wa nyumba kumi. Hii ilisaidia vitu vifuatavyo:
a.     Kujua mgeni ni nani, anakaa muda gani na anashughuli gani. Ikitokea uhalifu, basi inakuwa rahisi kupata pa kuanzia. Najua wengi mtasema mambo ya ujamaa, lakini tukumbuke ujamaa ndiyo unaofanya tunajiona wamoja. Yes kuna mambo ambayo hayakwenda vizuri,lakini utu na undugu viliimarika. Ukiangalia jirani zetu ambao walifuata ubepari waligombana na kuuana, sisi tu ndiyo tulishikamana. Kuanzia  nyumba kumi, kata, tarafa, wilaya, mkoa hata taifa tulijivunia mshikamano na kila mtu alikaataa kurubiniwa kusaliti nchi yetu
b.     Pia ilisaidia mambo ya sensa. Balozi wa nyumba kumi alijua idadi ya watu wake hata mtoto akizaliwa leo. Kipindi cha sensa, walichokuwa wanafanya ni kuhakiki idadi, hata kama mmoja ameenda likizo au amesafiri mjumbe anajua mtu wake hayupo.
c.      Maswala ya sera za taifa kama elimu afya na uzazi wa mpango viliwezekana kutoka na ushirikiano na mabalozi wa nyumba kumi.
d.     Mwanzoni balozi alikuwa anajitolea, lakini kutokana na sababu za kiusalama, basi serikali iwape hata kifuta jasho, na baadae waingie kwenye maswala ya usalama wa raia.
e.     Tukishawawezesha hawa, basi kila mgeni anayeingia kwenye eneo lake lazima ajue au ajulishwe, la sivyo uhalifu ukitokea eneo lake yeye ndiye atakuwa wa kwanza kuhojiwa.
Mwisho nimalizie kwa kusema, kwa yaliyotokea kwa jirani zetu tusidhani sisi tuko salama. Hii kwetu ni nafasi nzuri ya kujiweka mguu sawa. Ulinzi mipakani iimarishwe, tuache kuweka siasa kwenye vitu vinavyohatarisha usalama wa Taifa letu teule. Porojo za mabomu ya Arusha, Zanzibar, Tindikali nk vizifanyiwe masihara hata kidogo. Wananchi wapewe taarifa ya kila jambo na watu wawajibike au wawajibishwe wanaposhindwa kutekeleza majukumu yao.

Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania.

Mdau G. Lyimo
Email ThisBlogThis!Share to XShare to Facebook
Posted in | No comments
Newer Post Older Post Home

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to: Post Comments (Atom)

Popular Posts

  • tamasha la 32 la sanaa la bagamoyo lawasha moto, Mhe Makala asema utamaduni ni ajira kwa vijana
    NAIBU Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Mhe. Amos Makala amesema Sanaa na Utamaduni nchini itaendelea kuenziwa ili kuwaleta a...
  • wadau farida na paul wameremeta
     Wakila pozi baada ya kumeremeta katika Kanisa la Mtakatifu Petro jijini Dar es salaam kabla ya kwenda kwenye mnuso wao wa nguvu katika hote...
  • WAZIRI DK. NCHIMBI AMTEMBELEA PADRI ALIYEMWAGIWA TINDIKALI HOSPITALI YA MUHIMBILI LEO
    Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akisalimiana na Padri Joseph Monesmo Magamba wa Kanisa la Romani Katoliki Pa...
  • Naibu Spika aongoza Mkutano wa ACP nchini Ubelgiji
    Mhe.Job Ndugai,Mbunge wa Kongwa na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania akiongoza Mkutano wa Kamati ya Mazingira na Jamii cha Umoja wa Mabunge y...
  • Sherehe za kufunga mafunzo katika kikosi cha 842 Kj Mlale Jkt, Songea
      Mkuu wa wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma Mhe Senyi Ngaga kushoto akiangalia shehena ya mahindi ya chakula katika kikosi cha 842 Kj mlale Jkt...
  • barabara ya Mtoni-mbagala ilivyo
  • BACK TO THE SUA SEASON 2 EPISODE 2, KIJENGE, ARUSHA
    YECHU! YECHU! YECHU! HII HAILIPIWI HATA KUMI ARIFU  YAANI KIINGILIO NDO KITU HAMNAGA Pale Pale fasi ya K-JUU mwisho wa daladala mkabala na k...
  • JK ALIPOKUTANA NA WADAU WASHINGTON DC
    Rais wa Tanzania Dr.Jakaya Kikwete alipokutana na mpiganaji SundayShomari wa VOA siku ya Jumatano kwenye ofisi za ubalozi washington Dc. Rai...
  • KATIBU MKUU UTUMISHI, Bw. GEORGE YAMBESI AFUNGUA MAFUNZO YA MFUMO WA KUSIMAMIA RASILIMALI WATU SEREKALINI (HUMAN CAPITAL MANAGEMENT INFORMATION SYSTEM, HCMIS - LAWSON) KWA WAKURUGENZI NA MAKATIBU
    TAWALA WA MIKOA Katibu mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bw. George Yambesi leo amefungua rasmi mafunzo ya mfumo wa komp...
  • WAZIRI MEMBE AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA KOSOVO
    Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Kosovo, Mhe. Enver...

Blog Archive

  • ▼  2013 (500)
    • ►  October (22)
    • ▼  September (478)
      • HIKI HAPA KILIO CHA WANAFUNZI WA UDAKTARI BUGANDO...
      • No title
      • BREKING NYUUZZZZZZ: SERIKALI YA MAREKANI YAFUNGA S...
      • No title
      • NATURAL PRODUCTS FOR your skin
      • SIKU YA UTALII DUNIANI YENYE KAULI MBIU UTALII NA ...
      • President Kikwete sends Congratulatory Message to ...
      • WAKAZI WA KIKUYU KUSINI WAANDAMANA KUPINGA BOMOABO...
      • ngoma azipendazo ankal
      • wadau farida na paul wameremeta
      • ACCT members attend Master Builders South Africa C...
      • magari yanauzwa
      • Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Fedha za Serikali Bw L...
      • Spika Makinda apongeza Mabunge ya Afrika kwa kuong...
      • KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA JOHN CASMIR MINJA AH...
      • dk shein aagana na balozi wa marekani aliyemaliza ...
      • KATIBU MKUU UTUMISHI, Bw. GEORGE YAMBESI AFUNGUA M...
      • Maalim Seif aifunga rasmi Ijtimai ya Kimataifa ili...
      • HOJA YA HAJA: TUIENZI AMANI YETU KWA GHARAMA YOYOT...
      • MWIGULU NCHEMBA KUNDURUMA NDANI YA LONDON UINGEREZA
      • mwenge wa uhuru watua jijini mbeya
      • MBUNGE WA VITI MAALUMU TABORA,MH MUNDE TAMBWE ADHA...
      • JK arejea nyumbani kutoka Canada na Marekani
      • JK alipohudhuria Mkutano wa Kukabiliana na Ujangil...
      • Globu ya Jamii yakuletea Exclusive Intavyuuu na Re...
      • KANYABOYA LINGINE LAIBUKA DAR,WADAU KAENI CHONJO
      • WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU AIPONGEZA VODA...
      • TIMU YA WIZARA YA AFYA YATINGA ROBO FAINALI - SHIMIWI
      • SAGCOT CEO meets with the US journalists
      • Redd’s Miss Tanzania 2013/14 atembelea TBL leo
      • KONGAMANO LA WAZEE WASTAAFU LAFANYIKA ZANZIBAR
      • ufunguzi Mkutano wa Chama cha Kimataifa cha Taasis...
      • AJALI ZAPUNGUA MKOANI IRINGA
      • MWAKALEBELA AMWAGA VIFAA VYA MICHEZO KWA TIMU 13 M...
      • MAALIM SEIF AWATAKA WAISLAM NCHINI KUUNGA NA KUSHI...
      • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA AMIRI J...
      • Japanese Grant for the Food Security Project for U...
      • ACCT members attending Master Builders South Afric...
      • Awamu ya pili ya chakula cha hisani cha Taasisi ya...
      • MHE. MWIGULU NCHEMBA AWAKUNA WENGI DMV.
      • MWENGE WAZINDUA UJENZI WA OFISI YA KATA TANDALA WI...
      • WAZIRI CHIKAWE ATEMBELEA GEREZA KUU LA ISANGA,MKOA...
      • MKUTANO WA CCM CHWAKA UNGUJA
      • TAARIFA YA MSIBA
      • SingTel Group and Samsung partner to enhance mobil...
      • TIC yawahakikishia wawekezaji ushirikiano zaidi
      • DIAMOND ALIVYOWAKUNA MASHABIKI WAKE NDANI YA GOLD ...
      • KAPOTIVE STAR SINGER-S BUKOBA KUWASHA MOTO JIJINI ...
      • TFDA YAENDESHA KAMPENI YA UTUMIAJI WA VYAKULA VILI...
      • Wakazi wa eneo la hifadhi ya Ngorongoro wapokea ch...
      • AZANIA BANK YACHANGIA MIFUKO 100 YA SARUJI SHULE Y...
      • United States 2015 Diversity Visa Program Now Open
      • OPERESHENI KIMBUNGA AWAMU YA PILI YASHIKA KASI KAT...
      • mdau mugassa mwenda ahojiwa na BBC kwa kufurahishw...
      • Airtel yawanoa maafisa waTRA jinsi ya kulipia ada ...
      • NAIBU WAZIRI FEDHA AKAGUA UJENZI WA BARABARA VISIW...
      • 2013 Young Achievers Awards Nomination Open!
      • No title
      • IN LOVING MEMORY of DORA HOSEA TALAWA 1ST ANNIVESSARY
      • ngoma azipendazo ankal
      • TAARIFA YA MSIBA WA MAMA ROSE HEINRICH SANGIWA MATAJI
      • FRANSIC MIYEYUSHO AMTWANGA SADIK MOMBA KWA POINTI
      • Waziri Membe akutana kwa mazungumzo na Wafanyakazi...
      • Mahojiano ya JK na radio ya umoja wa mataifa, New ...
      • J&M Virgo washusha mali mpya
      • Daktari wa Rais Kikwete kupima afya na kuwapa lese...
      • MWENGE WA UHURU WATUA MAKETE
      • Swali la kizushi: Je ni mkono upi unaofaa kuvalia ...
      • No title
      • No title
      • introducing Mchaga na pesa by KiwaStrond ft. Banx
      • bwawa la maini oye! Suarez arudi na kupiga bee kat...
      • HARAMBEE KUCHANGIA CHAMA CHA MAPINDUZI MKOA WA KUS...
      • introducing 'Ni Noma' by Go Getta of the night cra...
      • MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA SERIKALI YA MAPINDUZI ...
      • Ubalozi wetu zambia na wajisiriamali wa Tanzania w...
      • Grace aikaeli Mbowe na mumewe wafariki kwa ajali ...
      • Simba yaibanjua Ruvu JKT 2-0 leo neshno
      • KANISA LA TGMIT LAFANYA IBADA MAALUMU KUIOMBEA AMA...
      • ZUMBA KUKWE AMSHINDA HAMADUU MWALIMU KWA KO RAUNDI...
      • TANZIA: Msiba wa Bi ROSE HENRISCH SANGIWA MATAJI
      • Sherehe za kufunga mafunzo katika kikosi cha 842 ...
      • Benki ya posta Tanzania tawi la Songea yaipiga jek...
      • GLOBAL LANGUAGE NETWORK (GLN) ILIYOFANYIKA WASHING...
      • TAMASHA LA SANAA BAGAMOYO NI KWELI KWAMBA LIMEPOTE...
      • No title
      • Tanzanian Minister of Defence Meets Governor of So...
      • UPANUZI WA BARABARA YA BENDERA TATU HADI KAMATA KU...
      • MISS UTALII TANZANIA KUTANGAZA NYATI WA AJABU NA ...
      • Cheka unenepe
      • WAFANYAKAZI WA IDARA MBALI MBALI ZA SERIKALI WACHU...
      • Kiwanda cha kuzalisha malighafi za kutengeneza Gil...
      • MAMA SALMA KIKWETE APEWA URAIA WA HIARI WA JIMBO L...
      • MKUTANO WA SIKU TATU WA MAOFISA WA JUU WA JESHI LA...
      • NBC YATENGA SIKU MAALUMU KUWASHUKURU WATEJA WAO
      • Serikali yabariki tamasha la Utamaduni Handeni
      • Matukio zaidi ya Mhe. Rais Kikwete alipolihutubia ...
      • ngoma azipendazo ankal
      • chemsha bongo...
      • cassim mganga akitumbuiza kwenye tamasha la fiesta...
Powered by Blogger.

About Me

Unknown
View my complete profile