Rais Barack Obama amelihutubia taifa Jumatatu usiku akisiistiza kwamba jeshi la taifa litaendelea na kazi zake wakati sehemu za serikali kuu zinafungwa kuanzia leo Jumanne baada ya bunge kushindwa kukubaliana juu ya bajeti ya mwaka 2013 - 2014. Hatua hii inajulikana kama Government Shutdown.
Baada ya wabunge wa Baraza la Wawakilishi kushindwa kukubaliana ilipofika usiku wa manane Jumatau, juu ya bajeti ya matumizi, serikali kuu ililazimika kutangaza kwamba sehemu za idara kadhaa zitabidi kufungwa.
Mvutano wa kisiasa umekuwa ukiendelea bungeni kuhusiana na sheria ya kihistoria ya Rais Obama, ya kutoa huduma nafuu za afya ambayo imekuwa mashuhuri kwa jina la "Obamacare".
Baraza la wawakilishi linaoongozwa na chama cha Republican liliidhinisha mswada wa matumizi ya serikali lakini kwa kuambatanisha kufutwa kwa sheria ya Obamacare. Na mara tatu Baraza la Seneti linalodhibitiwa na chama cha Demokrat limepinga mswada huo.
Kutokanana Bunge kutokubaliana juu ya kupitisha mswada wa kuongeza muda wa matumizi ya serikali kuu sheria ya Marekani inahitaji idara zote ambazo hazina shughuli muhimu kusita kufanya kazi kuanzia Oktoba mosi, yaani leo Jumanne
Jumla ya wafanyakazi wa serikali wapatao 800,000 wanakwenda likizo bila malipo
ambapo inatarajiwa kutakuwa na hasara ya dola bilioni moja kwa wiki.
Chanzo:VOA
Jumla ya wafanyakazi wa serikali wapatao 800,000 wanakwenda likizo bila malipo
ambapo inatarajiwa kutakuwa na hasara ya dola bilioni moja kwa wiki.
Chanzo:VOA
0 comments:
Post a Comment