Spika wa Bunge na Rais wa Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Madola barani Afrika,Mhe Anne Semamba Makinda akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Chama cha Wabunge Wanawake wa Jumuiya ya Madola Tawi la Seychelles ambapo alipongeza nchi za Jumuiya ya Madola kwa kuongeza idadi ya wanawake katika mabunge yake.Alitolea mfano nchi za umoja huo zilizopo Afrika Mashariki ambapo Uganda,Kenya Rwanda na Tanzania idadi ya wanawake imeongezeka katika chaguzi walizofanya hivi karibuni.Aidha alisema Afrika Mashariki ni mfano wa kuigwa ambapo Maspika wa Uganda Rwanda na yeye mwenyewe ni wanawake
Spika Makinda katika picha ya pamoja na viongozi wa Chama cha Wabunge Wanawake wa Jumuiya ya Madola barani Afrika.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti Mhe.Beatrice Shellukindo ambae pia ni Mwakilishi wa Chama hicho Afrika Mashariki na katikati ni Mwenyekiti Mhe.Lucia Witbooi toka Namibia.
Mhe.Spika Anne Makinda akipokea zawadi toka kwa Mwenyekiti wa Chama cha Wabunge wa Jumuiya ya Mandola katika ngazi ya kimataifa ambae pia ni Spika wa Uganda,Mhe Rebecca Kadaga wakati wa uzinduzi wa Chama cha Wabunge Wanawake wa Jumuiya ya Madola nchini Seychelles.
Picha zote na Saidi Yakubu wa Ofisi ya Bunge.
0 comments:
Post a Comment