Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Prof Elisante Ole Gabriel (mwenye mkasi) akifurahia jambo maara baada ya kukata utepe wakati wa uzinduzi wa awamu ya tano ya mbio za Rock City Marathon zitakazofanyika mkoani Mwanza tarehe 27 Oktoba, 2013. Pamoja naye ni baadhi ya wadhamini wa mbio hizo na viongozi wa vyama vya michezo nchini. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Capital Plus International (CPI), Dr. Ellen Otaru Okoedion akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa awamu ya tano ya mbio za Rock City Marathon zitakazofanyika mkoani Mwanza tarehe 27 Oktoba, 2013. Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Prof Elisante Ole Gabriel ambaye alikuwa mgeni ramsi na waliokaa ni wadhamini wa mbio hizo. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam jana.
Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Tanzania (RT), Nyambui Suleiman akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa awamu ya tano ya mbio za Rock City Marathon zitakazofanyika mkoani Mwanza tarehe 27 Oktoba, 2013. Wapili kulia (kwa waliokaa) ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Prof Elisante Ole Gabriel ambaye alikuwa mgeni rasmi akiwa na wadhamini wa mbio hizo zinazoandaliwa na kampuni ya Capital Plus International (CPI). Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam jana.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Prof Elisante Ole Gabriel akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa awamu ya tano ya mbio za Rock City Marathon zitakazofanyika mkoani Mwanza tarehe 27 Oktoba, 2013. Kulia kwake ni baadhi ya wadhamini wa mbio hizo. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dar es Salaam jana.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Prof Elisante Ole Gabriel (wanne kulia) akiteta jambo na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Jamal Malinzi (watatu kulia) mara baada ya kukata utepe kuzindua awamu ya tano yam bio za Rock Marathon zinazoandaliwa na kampuni ya Capital Plus International (CPI) zitakazofanyika tarehe 27 Oktoba, 2013 mkoani Mwanza. Wengine pichani ni wadhamini wa mbio hizo.
0 comments:
Post a Comment