Mhe.Job Ndugai,Mbunge wa Kongwa na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania akiongoza Mkutano wa Kamati ya Mazingira na Jamii cha Umoja wa Mabunge ya Nchi za Afrika,Caribbean na Pacific.Naibu Spika anashikilia wadhifa huo kwa kipindi cha miaka mitatu baada ya kuchaguliwa na wajumbe hao mwaka jana.Umoja huo una jumla ya nchi wanachama 79.Mikutano ya Umoja huo hufanyika mara nne kwa mwaka ambapo nchi wanachama huandaa katika nchi zao mikutabo miwili na pia miwili hufanyika Brussels ili kuwawezesha kukutana na wabunge wenzao wa Jumuiya ya Ulaya.Mkutano huo aliouongoza Mhe Naibu Spika hicho pamoja na mambo mengine ulifanyika ili kuweka msimamo wa pamoja kabla ya kukutana na wabunge toka Jumuiya ya Ulaya hapo kesho. Wengine pichani ni Nd.Kasule wa Sekretarieti ya ACP(kushoto),Makamu Mwenyekiti toka Chad,Mhe.Dr Mary Mwanjelwa wa Viti Maalum Mbeya na nyuma yake ni Mhe.Mussa Azzan Zungu,Mbunge wa Ilala.Picha na Saidi Yakubu wa Ofisi ya Bunge.
Wednesday, 18 September 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment