Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mh. Fatima Chohan ( kushoto) akisaini Hati ya Makubaliano ya mashirikiano katika masuala yanayohusu shughuli za Uhamiaji na Wakimbizi katika hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za wizara ya mambo ya Ndani ya Nchi leo Waziri huyo alipofanya ziara ya kikazi hapa nchini jana, watatu kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Tanzania Mh. Amme Silima aliyekuwa mwenyeji wa ugeni huu.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Tanzania Mh. Amme Silima wa kwanza kushoto na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mh. Fatima Chohan wa kwanza kutoka kushoto wakibadilishana Hati ya Makubaliano ya Mashirikiano katika masuala yanayohusu shughuli za Uhamiaji na Wakimbizi katika hafla fupi iliyofanyika leo katika ofisi za wizara ya mambo ya Ndani ya Nchi, hafla iliyoshuhudiwa na Katibu Mkuu wa wizara ya mambo ya ndani ya nchi Mbarak Abdulwakil pamoja na watendaji wa wizara hizo Tanzania na Afrika Kusini
Wajumbe wa Mkutano wa Wataalamu wa Masuala ya Uhamiaji na Wakimbizi kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Tanzania na Wizara ya Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Afrika Kusini wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa kikao cha wataalamu wa wizara hizo mbili ambapo walijadili maeneo mbalimbali watakayoshirikiana kwa pamoja.watatu kutoka kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Tanzania Mh. Amme Silima na watatu kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mh. Fatima Chohan wa pili kutoka kulia ni Katibu Mkuu wa wizara ya mambo ya ndani ya nchi Mbarak Abdulwakil.
0 comments:
Post a Comment