50 Bing Coupons

  • Subscribe to our RSS feed.
  • Twitter
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • Facebook
  • Digg

Tuesday, 24 September 2013

Tiketi za Kenya Airways sasa kununuliwa kwa M Pesa

Posted on 07:47 by Unknown
 Mkuu wa Idara ya Uendelezaji Teknolojia ya Habari wa Shirika la Ndege la Kenya Henry Obare (kushoto) na Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Kelvin Twissa wakimfuatilia Ahmed Abdalla Said jinsi anavyolipia tikiti yake ya Ndege kwa njia ya M-pesa kutoka katika simu yake ya kiganjani. Said amekuwa mteja wa kwanza kutumia huduma hiyo muda mfupi baada ya kuzinduiwa leo jijini Dar es salaam.
 Mkuu wa Idara ya Uendelezaji Teknolojia ya Habari wa Shirika la Ndege la Kenya Henry Obare (kushoto) akimkabidhi mteja Ahmed Abdalla Said tikiti yake ya safari ya nje ya nchi baada ya kuilipia kwa njia ya M-pesa muda mfupi baada ya huduma hiyo kuzinduliwa jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Kelvin Tiwissa. Huduma hiyo itawawezesha wasafiri wa  Shirika la Ndege la Kenya kulipia tikkiti zao kwa M-pesa na hivyo kuwapunguzia gharama za safari na usumbufu wa foleni.
Meneja Uendelezaji huduma ya  M-pesa Francis Tewele akimuelekeza mteja wa Shirika la Ndege la Kenya Ahmed Abdala Said jinsi ya kulipia tikiti ya Shirika hilo la Ndege kwa njia ya M-pesa wakati wa hafla ya uzinduzi wa huduma hiyo jijini Dar es salaam. Wanaoshuhudia  kutoka kushoto ni Mkuu wa Uendelezaji Teknolojia ya Habari wa Shirika la Ndege la Kenya Henry Obare, Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twissa.
-------------------------------------------------

Shirika la Ndege la Kenya - Kenya Airways limeingia ubia na kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom kupitia huduma yake ya M-pesa kuwawezesha wateja wake kulipia tiketi zao ikiwa ni kwa mala ya kwanza kwa huduma hiyo kuingia ubia na Shirika la la Ndege la Kimataifa kuwawezesha wateja wake kufanya malipo kwa njia ya simu za mkononi.
Akizungumza Wakati wa kutangaza rasmi ubia huo jijini Dar es salaam leo Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa, amesema ni furaha kubwa kuona M-pesa ikiendelea kupanuka katika ngazi ya kimataifa ikiwa ni moja ya mafanikio makubwa kwa huduma hiyo kuendelea kurahisisha maisha ya Watanzania.
"Leo tunaandika historia tukiendeleza ahadi yetu kwa watanzania kupitia M-pesa kuwa tutaendelea kutoa suluhusho la njia rahisi na ya uhakika katika kufanya malipo, utumaji na upoekaji wa fedha mahali popote Wakati wowote."Alisema Twissa.
"Kupitia mtadao wetu mpana ni wazi kwamba sasa tumeyarahisha zaidi maisha ya maelfu ya watanzania wanaotumia huduma za Shirika la Ndege la Kenya kwa shughuli za kiuchumi na kijamii kuwa na njia rahisi zaidi ya kulipia tiketi za safari zao bila kuingia gharama za kulazimika kufika vituo vya mauzo ya tiketi na kupanga foleni."Aliongeza
Twissa amesema M-pesa itaendelea kutoa suluhisho la mahitaji ya watanzania na soko kwa ujumla kwa kuziunganisha biashara mbalimbali na wateja na kwamba hilo halitobadilika.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Kitengo cha Taarifa Ukuzaji Teknolojia wa Shirika la Ndege la Kenya, Henry Obare, ameelezea matumaini yake kwa shirika hilo kutumia teknolojia za kisasa zaidi katika kukuza biashara kwa kuhakikisha linawahudumia wateja wake kwa haraka na usalama zaidi.
"Katika nchi yenye shughuli nyingi za kitalii na biashara huku shirika letu likiwa mstari wa mbele katika kufanikisha shughuli hizo kwa kuwezesha watu wake kuingia na kutoka ndani ya nchi kwa uhakika tunayo kila sababu kumuwezesha kila mmoja na njia kuwa na fursa ya kunufaika na uwepo wetu."Alisema Obare na kuongeza.
"Tunaamini ya kwamba hii ni siku kubwa sana katika historia ya shirika letu tunapokamilisha ndoto yetu ya kuwapatia kile ambacho wamekuwa wakikisubiri kutoka kwetu kwa muda mrefu."  Alihitimisha Obare.
Ili kulipia tiketi kwa M-pesa mteja anapaswa kupiga *150*00# na kuchagua kipengele na biashara na kufuata maelekezo.
Hata hivyo mteja atatakiwa kwanza kuwa na nambari ya kumbukumbu ya tiketi yake pamoja na gharama za tiketi husika kutoka Ofisi za Shirika hilo ambazo ataziingiza wakati akifanya muamala wa malipo.
Ushirikiano na Shirika la Ndege la Kenya ni wa pili kwa M-pesa kuvuka mipaka ya Tanzania ukitanguliwa na ushirikiano kati yake na Western Union unaomuwezesha mteja wa M-pesa kuwa na uwezo wa kupokea fedha kutoka nchi yoyote duniani ambayo Western Union inafanya kazi.


Email ThisBlogThis!Share to XShare to Facebook
Posted in | No comments
Newer Post Older Post Home

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to: Post Comments (Atom)

Popular Posts

  • tamasha la 32 la sanaa la bagamoyo lawasha moto, Mhe Makala asema utamaduni ni ajira kwa vijana
    NAIBU Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Mhe. Amos Makala amesema Sanaa na Utamaduni nchini itaendelea kuenziwa ili kuwaleta a...
  • wadau farida na paul wameremeta
     Wakila pozi baada ya kumeremeta katika Kanisa la Mtakatifu Petro jijini Dar es salaam kabla ya kwenda kwenye mnuso wao wa nguvu katika hote...
  • WAZIRI DK. NCHIMBI AMTEMBELEA PADRI ALIYEMWAGIWA TINDIKALI HOSPITALI YA MUHIMBILI LEO
    Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akisalimiana na Padri Joseph Monesmo Magamba wa Kanisa la Romani Katoliki Pa...
  • Naibu Spika aongoza Mkutano wa ACP nchini Ubelgiji
    Mhe.Job Ndugai,Mbunge wa Kongwa na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania akiongoza Mkutano wa Kamati ya Mazingira na Jamii cha Umoja wa Mabunge y...
  • Sherehe za kufunga mafunzo katika kikosi cha 842 Kj Mlale Jkt, Songea
      Mkuu wa wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma Mhe Senyi Ngaga kushoto akiangalia shehena ya mahindi ya chakula katika kikosi cha 842 Kj mlale Jkt...
  • barabara ya Mtoni-mbagala ilivyo
  • KANISA LA TGMIT LAFANYA IBADA MAALUMU KUIOMBEA AMANI TANZANIA
     Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akishiriki kuwasha mshumaa kama tendo la kuiangaza nchi ya Tanzania.  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape ...
  • GLOBAL LANGUAGE NETWORK (GLN) ILIYOFANYIKA WASHINGTON, DC YAFANA
    Katibu wa Jumuiya ya Tanzania akielezea nini maana ya GLN na kwanini Jumuiya ya Tanzania DMV ni moja ya washiririki  Banda la Tanzania lilki...
  • BACK TO THE SUA SEASON 2 EPISODE 2, KIJENGE, ARUSHA
    YECHU! YECHU! YECHU! HII HAILIPIWI HATA KUMI ARIFU  YAANI KIINGILIO NDO KITU HAMNAGA Pale Pale fasi ya K-JUU mwisho wa daladala mkabala na k...
  • IN LOVING MEMORY of DORA HOSEA TALAWA 1ST ANNIVESSARY
    28 th September 2013 marks the first year of the passing away of our beloved mum.  Memories continue to linger around us because there are ...

Blog Archive

  • ▼  2013 (500)
    • ►  October (22)
    • ▼  September (478)
      • HIKI HAPA KILIO CHA WANAFUNZI WA UDAKTARI BUGANDO...
      • No title
      • BREKING NYUUZZZZZZ: SERIKALI YA MAREKANI YAFUNGA S...
      • No title
      • NATURAL PRODUCTS FOR your skin
      • SIKU YA UTALII DUNIANI YENYE KAULI MBIU UTALII NA ...
      • President Kikwete sends Congratulatory Message to ...
      • WAKAZI WA KIKUYU KUSINI WAANDAMANA KUPINGA BOMOABO...
      • ngoma azipendazo ankal
      • wadau farida na paul wameremeta
      • ACCT members attend Master Builders South Africa C...
      • magari yanauzwa
      • Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Fedha za Serikali Bw L...
      • Spika Makinda apongeza Mabunge ya Afrika kwa kuong...
      • KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA JOHN CASMIR MINJA AH...
      • dk shein aagana na balozi wa marekani aliyemaliza ...
      • KATIBU MKUU UTUMISHI, Bw. GEORGE YAMBESI AFUNGUA M...
      • Maalim Seif aifunga rasmi Ijtimai ya Kimataifa ili...
      • HOJA YA HAJA: TUIENZI AMANI YETU KWA GHARAMA YOYOT...
      • MWIGULU NCHEMBA KUNDURUMA NDANI YA LONDON UINGEREZA
      • mwenge wa uhuru watua jijini mbeya
      • MBUNGE WA VITI MAALUMU TABORA,MH MUNDE TAMBWE ADHA...
      • JK arejea nyumbani kutoka Canada na Marekani
      • JK alipohudhuria Mkutano wa Kukabiliana na Ujangil...
      • Globu ya Jamii yakuletea Exclusive Intavyuuu na Re...
      • KANYABOYA LINGINE LAIBUKA DAR,WADAU KAENI CHONJO
      • WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU AIPONGEZA VODA...
      • TIMU YA WIZARA YA AFYA YATINGA ROBO FAINALI - SHIMIWI
      • SAGCOT CEO meets with the US journalists
      • Redd’s Miss Tanzania 2013/14 atembelea TBL leo
      • KONGAMANO LA WAZEE WASTAAFU LAFANYIKA ZANZIBAR
      • ufunguzi Mkutano wa Chama cha Kimataifa cha Taasis...
      • AJALI ZAPUNGUA MKOANI IRINGA
      • MWAKALEBELA AMWAGA VIFAA VYA MICHEZO KWA TIMU 13 M...
      • MAALIM SEIF AWATAKA WAISLAM NCHINI KUUNGA NA KUSHI...
      • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA AMIRI J...
      • Japanese Grant for the Food Security Project for U...
      • ACCT members attending Master Builders South Afric...
      • Awamu ya pili ya chakula cha hisani cha Taasisi ya...
      • MHE. MWIGULU NCHEMBA AWAKUNA WENGI DMV.
      • MWENGE WAZINDUA UJENZI WA OFISI YA KATA TANDALA WI...
      • WAZIRI CHIKAWE ATEMBELEA GEREZA KUU LA ISANGA,MKOA...
      • MKUTANO WA CCM CHWAKA UNGUJA
      • TAARIFA YA MSIBA
      • SingTel Group and Samsung partner to enhance mobil...
      • TIC yawahakikishia wawekezaji ushirikiano zaidi
      • DIAMOND ALIVYOWAKUNA MASHABIKI WAKE NDANI YA GOLD ...
      • KAPOTIVE STAR SINGER-S BUKOBA KUWASHA MOTO JIJINI ...
      • TFDA YAENDESHA KAMPENI YA UTUMIAJI WA VYAKULA VILI...
      • Wakazi wa eneo la hifadhi ya Ngorongoro wapokea ch...
      • AZANIA BANK YACHANGIA MIFUKO 100 YA SARUJI SHULE Y...
      • United States 2015 Diversity Visa Program Now Open
      • OPERESHENI KIMBUNGA AWAMU YA PILI YASHIKA KASI KAT...
      • mdau mugassa mwenda ahojiwa na BBC kwa kufurahishw...
      • Airtel yawanoa maafisa waTRA jinsi ya kulipia ada ...
      • NAIBU WAZIRI FEDHA AKAGUA UJENZI WA BARABARA VISIW...
      • 2013 Young Achievers Awards Nomination Open!
      • No title
      • IN LOVING MEMORY of DORA HOSEA TALAWA 1ST ANNIVESSARY
      • ngoma azipendazo ankal
      • TAARIFA YA MSIBA WA MAMA ROSE HEINRICH SANGIWA MATAJI
      • FRANSIC MIYEYUSHO AMTWANGA SADIK MOMBA KWA POINTI
      • Waziri Membe akutana kwa mazungumzo na Wafanyakazi...
      • Mahojiano ya JK na radio ya umoja wa mataifa, New ...
      • J&M Virgo washusha mali mpya
      • Daktari wa Rais Kikwete kupima afya na kuwapa lese...
      • MWENGE WA UHURU WATUA MAKETE
      • Swali la kizushi: Je ni mkono upi unaofaa kuvalia ...
      • No title
      • No title
      • introducing Mchaga na pesa by KiwaStrond ft. Banx
      • bwawa la maini oye! Suarez arudi na kupiga bee kat...
      • HARAMBEE KUCHANGIA CHAMA CHA MAPINDUZI MKOA WA KUS...
      • introducing 'Ni Noma' by Go Getta of the night cra...
      • MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA SERIKALI YA MAPINDUZI ...
      • Ubalozi wetu zambia na wajisiriamali wa Tanzania w...
      • Grace aikaeli Mbowe na mumewe wafariki kwa ajali ...
      • Simba yaibanjua Ruvu JKT 2-0 leo neshno
      • KANISA LA TGMIT LAFANYA IBADA MAALUMU KUIOMBEA AMA...
      • ZUMBA KUKWE AMSHINDA HAMADUU MWALIMU KWA KO RAUNDI...
      • TANZIA: Msiba wa Bi ROSE HENRISCH SANGIWA MATAJI
      • Sherehe za kufunga mafunzo katika kikosi cha 842 ...
      • Benki ya posta Tanzania tawi la Songea yaipiga jek...
      • GLOBAL LANGUAGE NETWORK (GLN) ILIYOFANYIKA WASHING...
      • TAMASHA LA SANAA BAGAMOYO NI KWELI KWAMBA LIMEPOTE...
      • No title
      • Tanzanian Minister of Defence Meets Governor of So...
      • UPANUZI WA BARABARA YA BENDERA TATU HADI KAMATA KU...
      • MISS UTALII TANZANIA KUTANGAZA NYATI WA AJABU NA ...
      • Cheka unenepe
      • WAFANYAKAZI WA IDARA MBALI MBALI ZA SERIKALI WACHU...
      • Kiwanda cha kuzalisha malighafi za kutengeneza Gil...
      • MAMA SALMA KIKWETE APEWA URAIA WA HIARI WA JIMBO L...
      • MKUTANO WA SIKU TATU WA MAOFISA WA JUU WA JESHI LA...
      • NBC YATENGA SIKU MAALUMU KUWASHUKURU WATEJA WAO
      • Serikali yabariki tamasha la Utamaduni Handeni
      • Matukio zaidi ya Mhe. Rais Kikwete alipolihutubia ...
      • ngoma azipendazo ankal
      • chemsha bongo...
      • cassim mganga akitumbuiza kwenye tamasha la fiesta...
Powered by Blogger.

About Me

Unknown
View my complete profile