Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Twiga Cement, Pascal Lesoinne (kulia) akimkabidhi Redds Miss Tanzania Happiness Watimanywa mfano wa hundi wakati akimkabidhi msaada wa mifuko 300 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa shule ya watoto wenye ulemavu wa ngozi (albino) itakayojengwa mkoani Shinyanga. wa pili kushoto ni Mkuu wa itifaki wa Miss Tanzania, Albert Makoye na Meneja Mahusiano ya Jamii wa Twiga Cement, Natasha D’souza. Hafla ya makabidhiano ilifanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Twiga Cement, Pascal Lesoinne (kulia) akimkabidhi Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige mfano wa hundi wakati akimkabidhi msaada wa mifuko 600 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa shule na zahanati zitakazojengwa mkoani Shinyanga. Katikati ni Meneja Mahusiano ya Jamii wa Twiga Cement, Natasha D’souza. Hafla ilifanyika jijini Dar es Salaam leo.
Mshindi wa tatu wa Redds Miss Tanzania 2013, Clara Bayo akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Twiga Cement, Pascal Lesoinne wakati wa hafla hiyo. Katikati ni mshindi wa pili, Latifa Mohamed na kulia ni Redds Miss Tanzania 2013, Happiness Watimanywa. Msaada wote wa mifuko 900 ya saruji unagharimu shs milioni 30.
0 comments:
Post a Comment