Ujumbe maalum kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Dodoma imemaliza ziara yake ya siku tatu hapa Nairobi leo tarehe 18 Septemba 2013. Ziara hiyo ililenga katika kutafuta soko la zabibu hapa Kenya.
Ujumbe huo uliongozwa na Bwana Aithan Lucas Chaula (DADO). Wajumbe wengine katika msafara huo ni pamoja na Bwana Ronald Makungaro Wesaka- Farm Manager, Ms. Rehema Hamis, Branch Director CRDB Dodoma, Bwana Titus Tumaini, Manager, Credit CRDB Microfinance na Bwana Genes Suku, Relationship Manager CRDB.
Benki ya CRDB imetoa mchango mkubwa wa kuwawezesha Wakulima wa zao la Zabibu huko Dodoma kwa njia mbalimbali ikiwemo kuwapa mikopo Wakulima hapa walipata fursa ya kuonana pia na Uongozi wa Kiwanda cha KWAL (Kenya Wine Agency Ltd) ambacho kinajishughulisha zaidi na utengenezaji wa wine na Juice.
Pia walionana na uongozi wa kiwanda cha Splash ambacho kinahusika zaidi na kutengeneza juice .
Mheshimiwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Batilda Burian pamoja na uongozi wa Kiwanda cha Splash alipotembelea Kiwanda hicho jana tarehe 17 Septemba, 2013 aliyekaa katika ni Bwana Vijay Budhdev, General Manager. Kulia kwa Mheshimiwa Balozi ni Bwana Aithan Chaula (DADO), Wilaya ya Chamwino.
Sehemu ya ujumbe huo kutoka Tanzania wakifuatilia mazungumzo haya katika ofisi za kiwanda cha splash.
Picha ya pamoja ya ujumbe huo pamoja na Mheshimiwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe. Batilda Burian walipofika kwenye ofisi za Ubalozi.
0 comments:
Post a Comment