Sayansi maana yake ni maarifa . Tunapo zungumzia dhana ya sayansi ya kiafrika , tunakuwa tunamaanisha matumizi ya maarifa ya kiafrika katika kukabiliana na mazingira ya mwanadamu pamoja na changamoto mbalimbali zinazo mkabili .
Tafiti mbalimbali za ki akiolojia na ki-anthropolojia zinaonyesha kuwa sayansi ya kiafrika imekuwapo kwa takribani miaka bilioni mbili sasa, hii ikiwa na maana kuwa sayansi ama ustaarabu wa kiafrika ndio ustaarabu mkongwe kupita ustaarabu mwingine wowote ule katika sayari ya dunia.
Hata ustaarabu wa jamii mbalimbali duniani kama vile waajemi, wayunani (Ugiriki ya kale ), wamisri, wasumeri ( Mesopotamia/babiloni ) ya kale nakadhalika, unatokana na ustaarabu ambao msingi wake ni sayansi ya kiafrika.
• Sayansi ya kiafrika imethibitika kumsaidia mwanadamu katika kukabiliana na mazingira yake kwa zaidi ya asilimia tisini na tisa (99%).
• Kwa bahati mbaya sana, sayansi ya kiafrika imepewa jina baya kwa kuitwa uchawi na kupigwa vita mbaya tangu mamia ya miaka iliyopita, lengo kuu likiwa ni kumuondolea mwanadamu uwezo wa kiungu ulio wekwa ndani yake wa kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazo mkabili katika maisha yake ya kila siku.
0 comments:
Post a Comment