Anajiita Mzee wa Mahaba kutoka Manzabay,Cassim Mganga akiwaimbisha mashabiki wake kwa shangwe huku mayowe yakitawala kila kona ya uwanja wa Kambarage usiku huu ndani wakati tamasha la Serengeti fiesta likiendelea kurindima usiku huu.
Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya,Rich Mavoko akiimba jukwaani usiku huu sambamba na madensa wake (hawapo pichani).
Baadhi ya wakazi wa mji wa Shinyanga wakiwa wamejitokeza kwa wingi usiku huu kwenye uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga,ambapo tamasha la Serengeti Fiesta 2013 likiendelea kufanyika.
Mwanadada Linah akiimba sambamba na shabiki wake jukwaani usiku huu wakati tamasha la serengeti fiesta likiendelea ndani ya uwanja wa Kambarage,mkoani Shinyanga usiku.
Mwanadada ambaye kwa sasa ameonekana akifanya vyema kwenye jukwaa la Serengeti fiesta 2013,Neylee akiwaimbisha mashaniki wake (hawapo pichani).
Mwanadada Shilole na madensa wake sambamba na shabiki wake pichani kulia,wakilishambulia jukwaa vilivyo usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti fiesta 2013,ndani ya uwanja wa Kambarage.mkoani Shinyanga.
PICHA ZAIDI LIVE INGIA MICHUZIJR.BLOGSPO.COM
0 comments:
Post a Comment