50 Bing Coupons

  • Subscribe to our RSS feed.
  • Twitter
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • Facebook
  • Digg

Thursday, 19 September 2013

Wanne waongezwa kesi ya mauaji ya bilionea wa madini, ndugu wa marehemu wanyanyasa wanahabari mahakamani moshi

Posted on 02:41 by Unknown
Na Dixon Busagaga 
wa Globu ya Jamii, Moshi. 
 KESI ya mauaji ya mfanyabiashara wa madini, Erasto Msuya (43), imelazimika kusikilizwa katika mahakama ya ndani baada ya kutokea sintofahamu huku mmoja wa waandishi wa habari aliyekuwa akifuatilia kesi hiyo akishambuliwa na ndugu wa Marehemu. 
Kesi hiyo iliyotajwa kwa mara ya kwanza katika mahakama ya hakimu Mkazi Moshi, Agosti 21 mwaka huu, ilipangwa kusikilizwa katika mahakama ya wazi lakini kutokana na kuwepo kwa umati mkubwa mahakamani, kesi hiyo ilihamishiwa mahakama ya ndani jambo lililowakera ndugu wa marehemu ambao walianza  kufanya vurugu na kulazimisha maaskari wa mahakama kuingilia kati wakisaidiwa na wale wa kutuliza ghasia (FFU). 
 Katika tukio hilo, waandishi wa habari wachache walioruhusiwa kuingia kusikiliza kesi hiyo walijikuta katika wakati mgumu, huku mmoja wao, Venance Maleli wa kituo cha Redio cha Moshi FM akishambuliwa na wanandugu hao ambao pia walitishia kumnyang’anya kamera yake. 
 Tukio hilo halikuishia hapo kwani hata mwandishi wa Globu ya Jamii alifanyiwa fujo na ndugu wa Marehemu ambao hawakutaka kupigwa picha wakati wakifanya juhudi za kumkimbiza hospitalini Mama yao, aliyepoteza fahamu baada ya kupata taarifa za kuahirishwa kwa kesi hiyo. 
 Aidha baadhi ya waandishi wa habari waliokuwa mahakamani hapo walilazimika kuondoka kwa kujificha kwa kuhofia usalama wao. Wadau wengi wameshangazwa na hatua ya baadhi ya wanafamilia wa marehemu kuwanyanyasa wanahabari ambao wanawasaidia wao kutangaza maendeleo ya kesi hiyo ili haki itendeke. "Hivi wanahabari wakiamua kususia kuripoti kesi hii wanadhani itakuwaje? Hivi hawajui kuwa kesi hii inapewa uzito kwa kuwa  wanahabari wanaifuatilia kwa karibu?" walisikika wadau wakishangaa kitendo cha baadhi ya wanafamilia hao.
 Katika kesi hiyo dakika hiyo iliyochukua takribani dakika 25 tu, watuhumiwa wengine wanne waliunganishwa katika shtaka hilo la mauaji kwa kukusudia kinyume na kanuni namba 16, kifungu cha 196 ya sheria za makosa ya jinai. 
 Watuhumiwa hao ni Joseph Damas maarufu Chusa mkazi wa Jijini Arusha, Jalila Zuberi Said (28), mkazi wa Babati, lakini pia anakaa Manyara na Kondoa , Sadiki Mohammed Jabir “msudani” au “mnubi”(32), mkazi wa Dar es salaam na Langata wilayani Hai na Karim kihundwa (33) mkazi wa kijiji cha Lawate wilayani Siha na kufanya jumla ya watuhumiwa kufikia 7 mpaka sasa. Hata hivyo maelfu ya wananchi waliofurika mahakamani hapo kufuatilia kesi hiyo, walionesha kukerwa na kitendo cha kutoruhusiwa kusikiliza kesi hiyo ambapo mara tu baada ya kesi hiyo kuahirishwa walionekana kukimbilia mlango wa kutokea. Watuhumiwa hao wote 7 waliondolewa mahakamani hapo kwa ulinzi mkali wa Jeshi la polisi wakiwa wamepakizwa katika Gari ya polisi, namba za usajili T 743 ADC iliyokuwa na Madirisha Meusi (tinted). Kesi hiyo inayoendeshwa na wakili wa Serikali, Stella Majaliwa akisaidiwa na Janeth Sikule katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Ruth Mkisi imeahirishwa hadi October 2 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa tena.
 Mtuhumiwa namba moja, Sharifu ‘Athumani’ Mohammed (31), wa kesi ya mauaji ya mfanyabiashara Erasto Msuya, akiwasili mahakamani, katika Mahakama ya hakimu mkazi ya Moshi, Kilimanjaro.mtuhumiwa huyo na wenzake 6  anatuhumiwa kumuua Erasto msuya mnamo 7 kwa kumpiga risasi
 Maelfu ya wananchi waliofurika katika mahakama ya hakimu mkazi Moshi,Mkoani Kilimanjaro, wakifuatilia kesi ya mauaji ya mfanyabiashara wa madini wa Mererani, Erasto msuya , aliyeuwawa na watu wanaosadikiwa kuwa ni
majambazi.
Baadhi ya ndugu wa marehemu, Erasto Msuya awaliofurika katika mahakama ya hakimu mkazi Moshi, Mkoani Kilimanjaro, wakimpakiza Mama yao ili kumkimbiza katika Hospitali ya KCMC baada ya kuanguka na kupoteza fahamu mahakamani hapo.
Email ThisBlogThis!Share to XShare to Facebook
Posted in | No comments
Newer Post Older Post Home

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to: Post Comments (Atom)

Popular Posts

  • tamasha la 32 la sanaa la bagamoyo lawasha moto, Mhe Makala asema utamaduni ni ajira kwa vijana
    NAIBU Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Mhe. Amos Makala amesema Sanaa na Utamaduni nchini itaendelea kuenziwa ili kuwaleta a...
  • wadau farida na paul wameremeta
     Wakila pozi baada ya kumeremeta katika Kanisa la Mtakatifu Petro jijini Dar es salaam kabla ya kwenda kwenye mnuso wao wa nguvu katika hote...
  • WAZIRI DK. NCHIMBI AMTEMBELEA PADRI ALIYEMWAGIWA TINDIKALI HOSPITALI YA MUHIMBILI LEO
    Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akisalimiana na Padri Joseph Monesmo Magamba wa Kanisa la Romani Katoliki Pa...
  • Naibu Spika aongoza Mkutano wa ACP nchini Ubelgiji
    Mhe.Job Ndugai,Mbunge wa Kongwa na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania akiongoza Mkutano wa Kamati ya Mazingira na Jamii cha Umoja wa Mabunge y...
  • Sherehe za kufunga mafunzo katika kikosi cha 842 Kj Mlale Jkt, Songea
      Mkuu wa wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma Mhe Senyi Ngaga kushoto akiangalia shehena ya mahindi ya chakula katika kikosi cha 842 Kj mlale Jkt...
  • barabara ya Mtoni-mbagala ilivyo
  • KANISA LA TGMIT LAFANYA IBADA MAALUMU KUIOMBEA AMANI TANZANIA
     Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akishiriki kuwasha mshumaa kama tendo la kuiangaza nchi ya Tanzania.  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape ...
  • GLOBAL LANGUAGE NETWORK (GLN) ILIYOFANYIKA WASHINGTON, DC YAFANA
    Katibu wa Jumuiya ya Tanzania akielezea nini maana ya GLN na kwanini Jumuiya ya Tanzania DMV ni moja ya washiririki  Banda la Tanzania lilki...
  • BACK TO THE SUA SEASON 2 EPISODE 2, KIJENGE, ARUSHA
    YECHU! YECHU! YECHU! HII HAILIPIWI HATA KUMI ARIFU  YAANI KIINGILIO NDO KITU HAMNAGA Pale Pale fasi ya K-JUU mwisho wa daladala mkabala na k...
  • IN LOVING MEMORY of DORA HOSEA TALAWA 1ST ANNIVESSARY
    28 th September 2013 marks the first year of the passing away of our beloved mum.  Memories continue to linger around us because there are ...

Blog Archive

  • ▼  2013 (500)
    • ►  October (22)
    • ▼  September (478)
      • HIKI HAPA KILIO CHA WANAFUNZI WA UDAKTARI BUGANDO...
      • No title
      • BREKING NYUUZZZZZZ: SERIKALI YA MAREKANI YAFUNGA S...
      • No title
      • NATURAL PRODUCTS FOR your skin
      • SIKU YA UTALII DUNIANI YENYE KAULI MBIU UTALII NA ...
      • President Kikwete sends Congratulatory Message to ...
      • WAKAZI WA KIKUYU KUSINI WAANDAMANA KUPINGA BOMOABO...
      • ngoma azipendazo ankal
      • wadau farida na paul wameremeta
      • ACCT members attend Master Builders South Africa C...
      • magari yanauzwa
      • Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Fedha za Serikali Bw L...
      • Spika Makinda apongeza Mabunge ya Afrika kwa kuong...
      • KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA JOHN CASMIR MINJA AH...
      • dk shein aagana na balozi wa marekani aliyemaliza ...
      • KATIBU MKUU UTUMISHI, Bw. GEORGE YAMBESI AFUNGUA M...
      • Maalim Seif aifunga rasmi Ijtimai ya Kimataifa ili...
      • HOJA YA HAJA: TUIENZI AMANI YETU KWA GHARAMA YOYOT...
      • MWIGULU NCHEMBA KUNDURUMA NDANI YA LONDON UINGEREZA
      • mwenge wa uhuru watua jijini mbeya
      • MBUNGE WA VITI MAALUMU TABORA,MH MUNDE TAMBWE ADHA...
      • JK arejea nyumbani kutoka Canada na Marekani
      • JK alipohudhuria Mkutano wa Kukabiliana na Ujangil...
      • Globu ya Jamii yakuletea Exclusive Intavyuuu na Re...
      • KANYABOYA LINGINE LAIBUKA DAR,WADAU KAENI CHONJO
      • WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU AIPONGEZA VODA...
      • TIMU YA WIZARA YA AFYA YATINGA ROBO FAINALI - SHIMIWI
      • SAGCOT CEO meets with the US journalists
      • Redd’s Miss Tanzania 2013/14 atembelea TBL leo
      • KONGAMANO LA WAZEE WASTAAFU LAFANYIKA ZANZIBAR
      • ufunguzi Mkutano wa Chama cha Kimataifa cha Taasis...
      • AJALI ZAPUNGUA MKOANI IRINGA
      • MWAKALEBELA AMWAGA VIFAA VYA MICHEZO KWA TIMU 13 M...
      • MAALIM SEIF AWATAKA WAISLAM NCHINI KUUNGA NA KUSHI...
      • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA AMIRI J...
      • Japanese Grant for the Food Security Project for U...
      • ACCT members attending Master Builders South Afric...
      • Awamu ya pili ya chakula cha hisani cha Taasisi ya...
      • MHE. MWIGULU NCHEMBA AWAKUNA WENGI DMV.
      • MWENGE WAZINDUA UJENZI WA OFISI YA KATA TANDALA WI...
      • WAZIRI CHIKAWE ATEMBELEA GEREZA KUU LA ISANGA,MKOA...
      • MKUTANO WA CCM CHWAKA UNGUJA
      • TAARIFA YA MSIBA
      • SingTel Group and Samsung partner to enhance mobil...
      • TIC yawahakikishia wawekezaji ushirikiano zaidi
      • DIAMOND ALIVYOWAKUNA MASHABIKI WAKE NDANI YA GOLD ...
      • KAPOTIVE STAR SINGER-S BUKOBA KUWASHA MOTO JIJINI ...
      • TFDA YAENDESHA KAMPENI YA UTUMIAJI WA VYAKULA VILI...
      • Wakazi wa eneo la hifadhi ya Ngorongoro wapokea ch...
      • AZANIA BANK YACHANGIA MIFUKO 100 YA SARUJI SHULE Y...
      • United States 2015 Diversity Visa Program Now Open
      • OPERESHENI KIMBUNGA AWAMU YA PILI YASHIKA KASI KAT...
      • mdau mugassa mwenda ahojiwa na BBC kwa kufurahishw...
      • Airtel yawanoa maafisa waTRA jinsi ya kulipia ada ...
      • NAIBU WAZIRI FEDHA AKAGUA UJENZI WA BARABARA VISIW...
      • 2013 Young Achievers Awards Nomination Open!
      • No title
      • IN LOVING MEMORY of DORA HOSEA TALAWA 1ST ANNIVESSARY
      • ngoma azipendazo ankal
      • TAARIFA YA MSIBA WA MAMA ROSE HEINRICH SANGIWA MATAJI
      • FRANSIC MIYEYUSHO AMTWANGA SADIK MOMBA KWA POINTI
      • Waziri Membe akutana kwa mazungumzo na Wafanyakazi...
      • Mahojiano ya JK na radio ya umoja wa mataifa, New ...
      • J&M Virgo washusha mali mpya
      • Daktari wa Rais Kikwete kupima afya na kuwapa lese...
      • MWENGE WA UHURU WATUA MAKETE
      • Swali la kizushi: Je ni mkono upi unaofaa kuvalia ...
      • No title
      • No title
      • introducing Mchaga na pesa by KiwaStrond ft. Banx
      • bwawa la maini oye! Suarez arudi na kupiga bee kat...
      • HARAMBEE KUCHANGIA CHAMA CHA MAPINDUZI MKOA WA KUS...
      • introducing 'Ni Noma' by Go Getta of the night cra...
      • MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA SERIKALI YA MAPINDUZI ...
      • Ubalozi wetu zambia na wajisiriamali wa Tanzania w...
      • Grace aikaeli Mbowe na mumewe wafariki kwa ajali ...
      • Simba yaibanjua Ruvu JKT 2-0 leo neshno
      • KANISA LA TGMIT LAFANYA IBADA MAALUMU KUIOMBEA AMA...
      • ZUMBA KUKWE AMSHINDA HAMADUU MWALIMU KWA KO RAUNDI...
      • TANZIA: Msiba wa Bi ROSE HENRISCH SANGIWA MATAJI
      • Sherehe za kufunga mafunzo katika kikosi cha 842 ...
      • Benki ya posta Tanzania tawi la Songea yaipiga jek...
      • GLOBAL LANGUAGE NETWORK (GLN) ILIYOFANYIKA WASHING...
      • TAMASHA LA SANAA BAGAMOYO NI KWELI KWAMBA LIMEPOTE...
      • No title
      • Tanzanian Minister of Defence Meets Governor of So...
      • UPANUZI WA BARABARA YA BENDERA TATU HADI KAMATA KU...
      • MISS UTALII TANZANIA KUTANGAZA NYATI WA AJABU NA ...
      • Cheka unenepe
      • WAFANYAKAZI WA IDARA MBALI MBALI ZA SERIKALI WACHU...
      • Kiwanda cha kuzalisha malighafi za kutengeneza Gil...
      • MAMA SALMA KIKWETE APEWA URAIA WA HIARI WA JIMBO L...
      • MKUTANO WA SIKU TATU WA MAOFISA WA JUU WA JESHI LA...
      • NBC YATENGA SIKU MAALUMU KUWASHUKURU WATEJA WAO
      • Serikali yabariki tamasha la Utamaduni Handeni
      • Matukio zaidi ya Mhe. Rais Kikwete alipolihutubia ...
      • ngoma azipendazo ankal
      • chemsha bongo...
      • cassim mganga akitumbuiza kwenye tamasha la fiesta...
Powered by Blogger.

About Me

Unknown
View my complete profile