AAR Healthcare imefanya vipimo vya afya kwa washiriki wa Bongo Star Search mwaka 2013, vipimo hivyo vikiwamo BMI, BP pamoja na kipimo cha kisukari Washiriki hao ambao kwa sasa wamebaki 15 ,walipewa pia mafunzo ya kiafya kutoka kwa Madactari wa AAR ya jinsi ya kuishi maisha yao kwa afya njema.
“Dhumuni la kuwafanyia washiriki vipimo vya afya, ni wao wenyewe kuweza kutambua afya zao kabla ya kuanza kupanda jukwaani, kupata ushauri wa jinsi ya kutunza afya zao kwa kipindi chote cha mashindano na hata baada ya mashindano” . Alisema Afisa Mahusiano wa AAR Amisa Juma. Bi. Juma alimalizia kwa kusema “ Sisi kama wadau wakubwa katika afya nchini, tumegundua vijana ndo waathirika wakubwa wa afya, kwa hiyo tumeamua kutumia jukwaa hili la BSS kuweza kusaidia na kutoa mchango mkubwa kwa washiriki na jamii kwa ujumla” .
Hii ni mara ya pili kwa AAR kudhamini mashindano haya ya BSS, mara ya kwanza ikiwa ni mwaka 2011.
AAR Healthcare wakiwa na washiriki wa BSS 2013
Afisa Mahusiano wa AAR HealthCare Amisa Juma akiwapa mafunzo washiriki wa BSS 2013 kuhusu afya zao ,kuchoto ni Bi, Fatma Omary, Maina Thadei na Amina Chibaba
Dr. Bamuhimbisa Richard kutoka AAR Healthcare akitoa mafunzo kwa washiriki wa BSS 2013 ya jinsi ya kuishi maisha bora kwa kuwa waangalifu na afya zao,walipokua kwenye kambi yao Mbezi Beach
Muuguzi Salome Mkilima kutoka AAR akimpima BP mshiriki wa BSS 2013 kambini Mbezi Beach Dar-es-salaam
Washiriki wa Bongo Star Search wakipata vipimo vya BMI na BP kabla ya kupanda jukwaani
0 comments:
Post a Comment