MBUNIFU WA MITINDO YA MAVAZI NA BALOZI WA OXFAM TANZANIA,KHADIJA MWANAMBOKA LEO AMEZINDUA PROJECT YA VVK-GROW CAMPAIGN.
PROJECT HII NI KAMPENI ILIYOBUNIWA NA KUENDESHWA NA BALOZI WA OXFAM,KHADIJA MWANAMBOKA IKIWA NA LENGO LA KUAINISHA CHANGAMOTO ZA SOKO KWA WAKULIMA WA CHAKULA HASA WANAWAKE,KUANIKA DHULUMA WANAYOFANYIWA WAKULIMA WA CHAKULA WANAWAKE NA KUHAMASISHA WATUMIAJI WA BIDHAA ZA CHAKULA MIJINI,KUTAMBUA THAMANI YA CHAKULA NA KUWA SOKO LENYE TIJA KWA WAKULIMA WA CHAKULA HASA WANAWAKE.
KAMPENI HII INAHUSISHA WASICHANA"GROW GIRLS" AMBAO NI WANAMITINDO -MODELS WATAKAOKUWA WANAPITA KWENYE MIKUSANYIKO MBALI MBALI, MAOFISINI NA KWENYE TAASISI MBALI MBALI KUHAMASISHA NA KUUZA BIDHAA ZA WAKULIMA WADOGO WANAWAKE.
MBUNIFU WA MITINDO YA MAVAZI NA BALOZI WA OXFAM TANZANIA,KHADIJA MWANAMBOKA AKIONYESHA BANGO LENYE UJUMBE.
SEHEMU YA WASICHANA"GROW GIRLS" AMBAO NI WANAMITINDO WAKIWA KWENYE PICHA YA PAMOJA.
0 comments:
Post a Comment