Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akiongea na Afisa Mwandamizi mradi wa FHI 360 Road II Bi Florence Lema na Mratibu wa Mradi eneo la Sumbawanga Ndugu Nsajigwa Richard walipofika ofisini kwake leo kushukuru kwa msaada wa ofisi waliopewa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo ambayo waliitumia kwa muda wa miaka mitatu.
Afisa Mwandamizi mradi wa FHI 360 Road II Bi Florence Lema akimkabidhi Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima barua ya shukurani kwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo kuwasaidia Ofisi waliyoitumia kwa mda wa miaka mitatu katika kipindi chote cha mradi ambao ambao hivi sasa umekamilika.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima akionyesha barua hiyo mara baada ya kukabidhiwa ofisi iliyokuwa ikitumika na mradi wa FHI 360 Road II Mkoani Rukwa. Afisa Mwandamizi wa mradi huo Bi. Florence Lema ameishukuru Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kwa ushirikiano Mkubwa ilionao katika kusaidia na kujumuika pamoja na sekta binafsi na mashirika ya kijamii ya kitaifa na kimataifa.


Picha ya Pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na wawakilishi kutoka FHI 360 Ofisi kwake mapema hii leo.
(Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa....rukwareview.blogspot.com)
0 comments:
Post a Comment