MKUU wa Mkoa wa Morogoro Joel Bendela amevitaka vyama vya michezo nchini kutafuta mbinu ya kuwa na wadhamini wa kudumu kama ilivyo kwa mchezo wa pooltable, badala ya kuka na kulalamikia kukosa wadhamini.
Rai hiyo aliitoa mjini hapa wakati akifungua michuano ya pool table ngazi ya taifa inayofanyika kwenye ukumbi wa Tanzanite, nakwamba mchezo huo umekuwa ukidhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania kupitia bia yake ya safari lager (TBL) katika kipindi cha miaka sita mfululizo.
“ Baadhi ya vyama vya michezo vimekuwa vikilalamikia kukosa wadhamini na kudai kuwa mchezo wa soka pekee ndo umekuwa ukidhaminiwa jambo ambalo si kweli, nakwamba mbona chama cha chezo wa pool table taifa kimeweza kuwa na udhamini katika kipindi kirefu. “ Alisema
Aidha Mkuu huyo wa mkoa alisema vilabu 17 kutoka mikoa 17 vinashiriki michuano hiyo, ambapo kati ya wachezaji hao itaundwa timu ya Taifa itakayo iwakilisha nchini mwakani kwenye mashindanohayo nchini Malawi .
Aliwataka wachezaji kuwa na nidhamu pamoja na kuupenda mchezo wanaoucheza , nakwamba kwa kufanya hivyo kutawawezesha kujiongezea kipato, kuiletea nchi sifa na kutolea mfano wa Bondia Francis Cheka.
Kwa Upande wake Meneja kutoka Kampuni ya Bia Tanzania Kupitia bia yake ya Safari Lager Oscar Shelukindo, alisema kampuni hiyo itaendelea kudhamini mashindano hayo, ambayo mwakani yatafanyika nchini malawi na kuwataka wachezaji kuondoa shaka.
Shelukindo aliwataka wachezaji kucheza kwa kujituma ili kupata wachezaji wenye viwango vinavyotakiwa ili waweze kuiwakilisha nchi na hatimaye kuibuka na ushindi.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Pooltable Taifa, Fredy Mushi alisema mchezo huo unashirikisha vijana kuanzia miaka 18 na kuendelea, ambapo umeendelea kukua na kuungwa mkono sehemu nyingi tofauti na awali.
Alisema baadhi ya wachezaji wamekuwa wakisajiliwa na timu nyingine kutoka mkoa hadi mkoa na hivyo kujiongezea kupato, hivyo kuwaomba wazazi na wananchi kutoa ushirikiano, na kudai kuwa bila ushirikiano wao ukuaji wake utashuka.
Hata hivyo alimpongeza mbunge wa jimbo la Morogoro Mjini Aziz Abood kwa kununua meza kwaajili ya wachezaji mkoani hapa nakwamba ni jambo la kuigwa na watu wengine wenye mapenzi mema na machezo huo.
Timu zinazoshiriki mashindano hayo ni pamoja na Morogoro, lindi, Kagera, Tabora, Mwanza, Arusha , Shinyanga, Pwani, Temeke, Ilala, Kinondoni, Mbeya Dodoma , Iringa , Mara, Mnyara na Kilimanjaro.
Timu mbali mbali zitakazoshiriki Mashindano hayo zikiwa kwenye Maandamano.
Meneja wa Bia ya Safari Lager,Oscar Shelukindo (Katikati) akiongoza maandamano hayo kuelekea kwenye Ukumbi wa Mashindano.
0 comments:
Post a Comment