Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue jana alikutana na aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bwana Jovin Kitambi na Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma ambao wamemaliza muda wao hivi karibuni wa kuiongoza Tume kwa kipindi cha miaka Sita, katika awamu mbili tofauti. Mwenyekiti na Makamishna walikwenda Ikulu kwa lengo la kumuaga rasmi Katibu Mkuu Kiongozi.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (aliyesimama katikati mstari wa mbele), katika picha ya pamoja na Mwenyekiti Tume ya Utumishi wa Umma aliyemaliza muda wake Bwana, Jovin Kitambi (Kushoto) na Katibu wa Tume ya Utumishi wa Umma, Bibi Claudia Mpangala (Kulia), pamoja na Makamishna na baadhi ya Watendaji wa Tume ya Utumishi wa Umma. Mwenyekiti na Makamishna hao walikwenda Ikulu kumuaga baada ya kumaliza muda wao wa Uongozi katika Tume ya Utumishi wa Umma, kwa kipindi cha miaka Sita.
0 comments:
Post a Comment