UBALOZI WA TANZANIA ULIOPO LUSAKA, ZAMBIA KWA KUSHIRIKIANA NA KIKUNDI CHA WAJASIRIAMALI CHA “HANDPRODUCTS OF TANZANIA (HOT)” WAMEANDAA WIKI YA TANZANIA KWENYE VIWANJA VYA OFISI YA UBALOZI KUANZIA TAREHE 27 SEPTEMBA HADI 2 OKTOBA 2013.
KATIKA WIKI HIYO KUTAKUWA NA MAONEYESHO YA BIDHAA ZA TANZANIA KAMA VILE MAVAZI YA BATIKI NA “TIE N DYE” KWA WANAUME, WANAWAKE, NA WATOTO, VIATU VYA KIMASAAI, VIKAPU VYA KIASILI, CHAI NA KAHAWA, SABUNI ZILIZOTENGENEZWA KWA MITISHAMBA, LISHE NA VIRUTUBISHO, KHANGA, MVINYO NA VINYWAJI AINA MBALIMBALI VYA TANZANIA. JAMBO LA KUVUTIA ZAIDI PIA KUTAKUWA NA VYAKULA VYA AINA MBALI VYA KITANZNIA NA MENGINE MENGI.
MAONYESHO HAYA YATAANZA SAA TATU ASUBUHHI KILA SIKU NA KUMALIZIKA SAA KUMI NA MBILI JIONI.
KIINGILIO NI BURE
@@@@@@
WOTE MNAKARIBISHWA
0 comments:
Post a Comment