Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Makete Ndugu Francis Chaula akimkabidhi Sadock Mahenge shilingi laki moja.
Mlemavu Sadock Sanga Mahenge akishukuru kwa kupewa fedha hiyo.
======
Na Edwin Moshi
wa Globu ya Jamii, Makete
Chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Makete mkoani Njombe kimetekeleza ahadi yake kiliyoitoa mwezi uliopita kwa mlemavu Sadock Mahenge ya kumpatia shilingi laki moja kwa ajili ya kukarabati baiskeli yake.
Akimkabidhi fedha hizo taslimu nyumbani kwake, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Makete Ndugu Francis Chaula amesema kwa kuwa walimuahidi kumsaidia kurekebisha baiskeli yake na yeye kuaninisha gharama, ndipo wamempatia kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya marekebisho hayo ili kumsaidia kutembea.
"Nakumbuka wakati wa ziara yangu mwezi uliopita nilikuahidi mimi kwa niaba ya chama, hivyo ahadi hiyo tumeitekeleza naomba nikukabidhi fedha hizi shilingi laki moja zilizotolewa na CCM" alisema Chaula
Kwa upande wake Sadock Sanga Mahenge amekishukuru chama hicho kwa kutekeleza ahadi hiyo, na kuahidi kuzitumia fedha hizo kama zinavyotakiwa kwa kurekebisha baiskeli yake ili imsaidie kuzunguka maeneo mbalimbali kutekeleza wajibu wake
0 comments:
Post a Comment