Ningependa kuwauliza wale watanzania walio Marekani kama tunaweza ku-share ni kadi gani za simu zenye dakika nyingi kupiga Bongo cell phones. Wengi wetu kupiga simu nyumbani ni muhimu, sio kila siku ila mara kwa mara. Na gharama za kadi kiasi fulani ni kubwa, mimi kadi ambazo natumia online nyingi ni 17c per minute (.17/min).. which means unapata karibia dakika 58 kwa $10.. Naelewa kuna apps kama viber ambazo zinasaidia kiasi fulani, ila ni vigumu kumwambia bibi akiwa Masasi kwamba weka viber kwenye simu.
Kwa hiyo kama mtu anajua website gani wana kadi zenye deal zenye rates nzuri kupiga Tanzania please naomba tuambizane. Kama itakuwa ya mtanzania itakuwa bora zaidi, kuinuana muhimu. Au kama kuna means za kupiga simu besides kadi mtu unajua please let us share.
Napatikana jmakwanga@yahoo.com
0 comments:
Post a Comment