Pichani ni Mwanadada Irene ambaye amekuwa akifanya vyema kwenye anga ya Bongo Muvi,hapa alikuwa kwenye lokesheni,akiigiza kwenye moja ya filamu yao mpya na Muigizaji mahiri kutoka nchini Ghana, aitwaye Van Vicker,kama walivyonaswa a Globu ya jamii mapema mchana huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere,jijini Dar.
Pichani kulia ni Rais wa shirikisho la Filamu Tanzania,TAFF akiwa sambamba na baadhi ya Waigizaji wa filamu hapa nchini,Irene na mdau sambamba na Muigizaji mahiri wa filamu kutoka nchini Ghana,Van Vicker wakijiandaa kushut muvi yao mpya,ambayo bado jina lake halijawekwa hadharani,wakiwa kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere,jijini Dar leo mchana.
Pichani ni Mzee Hasheem Kambi akiwa na kimwana Irene wakiwa lokesheni wakiigiza kwenye moja ya filamu yao mpya ambayo hawakuitaja jina,huku mkali wa kuigiza kutoka nchini Ghana,Van Vicker akiwa lokesheni wakiigiza kama walivyonaswa na camera ya Globu ya jamii mapema leo mchana kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere,jijini Dar leo mchana.
0 comments:
Post a Comment