50 Bing Coupons

  • Subscribe to our RSS feed.
  • Twitter
  • StumbleUpon
  • Reddit
  • Facebook
  • Digg

Wednesday, 18 September 2013

Tanzania kuwa miongoni wa wazalishaji wakubwa wa chuma Afrika.

Posted on 07:46 by Unknown
 Central hill Liganga iron ore
 Core inspection

Drill rig on site Mchuchuma.
 Drilling Rig servicing
 Exploraton shaft Mchuchuma
picha mchoro wa kiwanda chaliganga
picha mchoro wa kiwanda mchuchuma.

=====  ======  ======

Tanzania kuwa miongoni wa wazalishaji wakubwa wa chuma Afrika.

DAR ES SALAAM: Tanzania inatarajia kuwa mmoja wa wazalishaji wakubwa wa chuma barani Afrika kwa kuzalisha tani milioni moja kwa mwaka mara uzalishaji wa madini hayo utakapoanza mwaka 2018/19 chini ya kampuni ya Tanzania China Mineral Resources Limited (TCIMRL), ambayo ni kampuni ya ubia kati ya Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) na Shirika la Sichuan Hongda Group (SHG) ya China.

Ripoti ya utafiti wa TCIMRL ambayo ni sehemu ya maandalizi ya kuanzishwa mgodi na kiwanda cha chuma katika eneo la Liganga wilayani Ludewa, iliyofanywa katika eneo la kilomita za mraba 10 pekee inabainisha kuwapo kwa tani milioni 219 za chuma ambazo zitadumu kwa zaidi ya miaka 70 kwa uchimbaji wa juu (open cast mining). Eneo lililobakia lina kilomita za mraba 156 na kukadiriwa kuwa na rasilimali kubwa zaidi.

Tanzania itashika nafasi ya nne ikizifuatia nchi za Afrika Kusini itakayozalisha bidhaa za chuma tani milioni 8.5 kwa mwaka, Misri tani milioni 8.0 na Libya tani milioni 2.0 kwa mwaka. Chuma kinachozalishwa duniani ni takribani tani bilioni 1.55 kwa mwaka, mzalishaji mkubwa ikiwa ni China inayotoa tani milioni 711 kwa mwaka ambayo ni sawa na asilimia 46 ya chuma chote kinachozalishwa duniani. Mbali na chuma, madini mengine yatakayotokana na mgodi huo ni Titanium tani 175,400 kwa mwaka na Vanadium tani 5,000 kwa mwaka.

Mradi huu ni moja ya miradi miwili iliyopo katika mkataba kati ya NDC na SHG uliotiwa saini Septemba 21, 2011 ya uanzishwaji wa mgodi wa makaa ya mawe na ujenzi wa kituo cha kufua umeme wa megawati 600 katika eneo la Mchuchuma pamoja na ujenzi wa msongo wa umeme wa kilovoti 220 kati ya Mchumchuma na Liganga; na uanzishwaji wa mgodi wa chuma na ujenzi wa kiwanda cha kuchenjua chuma na kiwanda cha kuzalisha bidhaa za chuma, pamoja na ujenzi wa barabara kati ya Mchuchuma na Liganga.

Kiasi cha Makaa ya mawe kulingana na utafiti wa TCIMRL katika eneo la kilomita za mraba 30 ni tani milioni 370 ambazo zinaweza kuchimbwa kwa miaka zaidi ya 100. Kkuna eneo la ziada la kilomita za mraba 110 ambalo linakadiriwa kuwa na rasilimali zaidi ya makaa yam awe.

Miradi hii miwili itakayogharimu Dola za Kimarekani bilioni tatu (USD 3.0bil) inatarajiwa kuliingizia taifa mapato ya Dola bilioni 1.7 kwa mwaka itakapoanza uzalishaji kamili mwaka 2018/19, mapato ambayo yatatokana na uuzaji wa umeme wa megawati 600, uuzaji wa makaa ya mawe kwa nishati ya viwandani, chuma, titanium, vanadium na itatoa ajira ya moja kwa moja watanzania 6,000 na 35,000 kwa zisizo za moja kwa moja.

Miradi hii hivi sasa ipo katika awamu ya kwanza ambayo ilikuwa inahusisha utafiti na maandalizi kabla ya Mei mwakani kuingia katika awamu ya ujenzi wa migodi na viwanda katika maeneo ya Mchuchuma na Liganga.

Mradi huu wa ubia na mwekezaji wa kimataifa unakwenda sambamba na mradi mwingine katika eneo hilo la Ludewa uliotiwa saini Septemba 2, 2009 na kampuni ya wazawa ya M.M. Steel Resources Public Limited Company (MMSR PLC). Mradi huu unalenga kuzalisha chuma ghafi kwa kutumia chuma cha Liganga Matitu na  makaa ya mawe ya Katewaka. Kampuni ya ubia iliyoanzishwa ni Maganga Matitu Resource Development Limited (MMRDL). Uwekezaji utakuwa ni dola za Kimarekani milioni 150 na unatazamiwa kuingiza mapato ya dola milioni 183.3 kwa mwaka. Chuma ghafi hiki kitatumika kuwa malighafi kwa viwanda vingine vilivyo ndani na nje  ya nchi, hivyo kuwezesha uzalishaji wa chuma imara kulikoni hiki cha sasa kitokanacho na scrap ambacho ni hafifu. Lakini pia hujuma kwa miundombinu yetu kwa ajili ya scrap utakoma.


Imetolewa na: Abel Ngapemba
Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa Shirika
angapemba@ndc.go.tz, 022 211 1490 0784 273 588/0715
18 Septemba 2013
Email ThisBlogThis!Share to XShare to Facebook
Posted in | No comments
Newer Post Older Post Home

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to: Post Comments (Atom)

Popular Posts

  • tamasha la 32 la sanaa la bagamoyo lawasha moto, Mhe Makala asema utamaduni ni ajira kwa vijana
    NAIBU Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Mhe. Amos Makala amesema Sanaa na Utamaduni nchini itaendelea kuenziwa ili kuwaleta a...
  • wadau farida na paul wameremeta
     Wakila pozi baada ya kumeremeta katika Kanisa la Mtakatifu Petro jijini Dar es salaam kabla ya kwenda kwenye mnuso wao wa nguvu katika hote...
  • WAZIRI DK. NCHIMBI AMTEMBELEA PADRI ALIYEMWAGIWA TINDIKALI HOSPITALI YA MUHIMBILI LEO
    Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi (kushoto) akisalimiana na Padri Joseph Monesmo Magamba wa Kanisa la Romani Katoliki Pa...
  • Naibu Spika aongoza Mkutano wa ACP nchini Ubelgiji
    Mhe.Job Ndugai,Mbunge wa Kongwa na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania akiongoza Mkutano wa Kamati ya Mazingira na Jamii cha Umoja wa Mabunge y...
  • barabara ya Mtoni-mbagala ilivyo
  • Sherehe za kufunga mafunzo katika kikosi cha 842 Kj Mlale Jkt, Songea
      Mkuu wa wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma Mhe Senyi Ngaga kushoto akiangalia shehena ya mahindi ya chakula katika kikosi cha 842 Kj mlale Jkt...
  • BACK TO THE SUA SEASON 2 EPISODE 2, KIJENGE, ARUSHA
    YECHU! YECHU! YECHU! HII HAILIPIWI HATA KUMI ARIFU  YAANI KIINGILIO NDO KITU HAMNAGA Pale Pale fasi ya K-JUU mwisho wa daladala mkabala na k...
  • Mkongo wa Taifa wa mawasiliano wakubalika zaidi kimataifa
    Mhandisi wa kampuni ya Mawasiliano Tanzania (TTCL), Bw. Keneth Makayanga (kushoto) akiwa pamoja na Mkuu wa Idara ya Mauzo, Bw. Kisamba Tambw...
  • KANISA LA TGMIT LAFANYA IBADA MAALUMU KUIOMBEA AMANI TANZANIA
     Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akishiriki kuwasha mshumaa kama tendo la kuiangaza nchi ya Tanzania.  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape ...
  • JK ALIPOKUTANA NA WADAU WASHINGTON DC
    Rais wa Tanzania Dr.Jakaya Kikwete alipokutana na mpiganaji SundayShomari wa VOA siku ya Jumatano kwenye ofisi za ubalozi washington Dc. Rai...

Blog Archive

  • ▼  2013 (500)
    • ►  October (22)
    • ▼  September (478)
      • HIKI HAPA KILIO CHA WANAFUNZI WA UDAKTARI BUGANDO...
      • No title
      • BREKING NYUUZZZZZZ: SERIKALI YA MAREKANI YAFUNGA S...
      • No title
      • NATURAL PRODUCTS FOR your skin
      • SIKU YA UTALII DUNIANI YENYE KAULI MBIU UTALII NA ...
      • President Kikwete sends Congratulatory Message to ...
      • WAKAZI WA KIKUYU KUSINI WAANDAMANA KUPINGA BOMOABO...
      • ngoma azipendazo ankal
      • wadau farida na paul wameremeta
      • ACCT members attend Master Builders South Africa C...
      • magari yanauzwa
      • Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Fedha za Serikali Bw L...
      • Spika Makinda apongeza Mabunge ya Afrika kwa kuong...
      • KAMISHNA JENERALI WA MAGEREZA JOHN CASMIR MINJA AH...
      • dk shein aagana na balozi wa marekani aliyemaliza ...
      • KATIBU MKUU UTUMISHI, Bw. GEORGE YAMBESI AFUNGUA M...
      • Maalim Seif aifunga rasmi Ijtimai ya Kimataifa ili...
      • HOJA YA HAJA: TUIENZI AMANI YETU KWA GHARAMA YOYOT...
      • MWIGULU NCHEMBA KUNDURUMA NDANI YA LONDON UINGEREZA
      • mwenge wa uhuru watua jijini mbeya
      • MBUNGE WA VITI MAALUMU TABORA,MH MUNDE TAMBWE ADHA...
      • JK arejea nyumbani kutoka Canada na Marekani
      • JK alipohudhuria Mkutano wa Kukabiliana na Ujangil...
      • Globu ya Jamii yakuletea Exclusive Intavyuuu na Re...
      • KANYABOYA LINGINE LAIBUKA DAR,WADAU KAENI CHONJO
      • WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU AIPONGEZA VODA...
      • TIMU YA WIZARA YA AFYA YATINGA ROBO FAINALI - SHIMIWI
      • SAGCOT CEO meets with the US journalists
      • Redd’s Miss Tanzania 2013/14 atembelea TBL leo
      • KONGAMANO LA WAZEE WASTAAFU LAFANYIKA ZANZIBAR
      • ufunguzi Mkutano wa Chama cha Kimataifa cha Taasis...
      • AJALI ZAPUNGUA MKOANI IRINGA
      • MWAKALEBELA AMWAGA VIFAA VYA MICHEZO KWA TIMU 13 M...
      • MAALIM SEIF AWATAKA WAISLAM NCHINI KUUNGA NA KUSHI...
      • RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA AMIRI J...
      • Japanese Grant for the Food Security Project for U...
      • ACCT members attending Master Builders South Afric...
      • Awamu ya pili ya chakula cha hisani cha Taasisi ya...
      • MHE. MWIGULU NCHEMBA AWAKUNA WENGI DMV.
      • MWENGE WAZINDUA UJENZI WA OFISI YA KATA TANDALA WI...
      • WAZIRI CHIKAWE ATEMBELEA GEREZA KUU LA ISANGA,MKOA...
      • MKUTANO WA CCM CHWAKA UNGUJA
      • TAARIFA YA MSIBA
      • SingTel Group and Samsung partner to enhance mobil...
      • TIC yawahakikishia wawekezaji ushirikiano zaidi
      • DIAMOND ALIVYOWAKUNA MASHABIKI WAKE NDANI YA GOLD ...
      • KAPOTIVE STAR SINGER-S BUKOBA KUWASHA MOTO JIJINI ...
      • TFDA YAENDESHA KAMPENI YA UTUMIAJI WA VYAKULA VILI...
      • Wakazi wa eneo la hifadhi ya Ngorongoro wapokea ch...
      • AZANIA BANK YACHANGIA MIFUKO 100 YA SARUJI SHULE Y...
      • United States 2015 Diversity Visa Program Now Open
      • OPERESHENI KIMBUNGA AWAMU YA PILI YASHIKA KASI KAT...
      • mdau mugassa mwenda ahojiwa na BBC kwa kufurahishw...
      • Airtel yawanoa maafisa waTRA jinsi ya kulipia ada ...
      • NAIBU WAZIRI FEDHA AKAGUA UJENZI WA BARABARA VISIW...
      • 2013 Young Achievers Awards Nomination Open!
      • No title
      • IN LOVING MEMORY of DORA HOSEA TALAWA 1ST ANNIVESSARY
      • ngoma azipendazo ankal
      • TAARIFA YA MSIBA WA MAMA ROSE HEINRICH SANGIWA MATAJI
      • FRANSIC MIYEYUSHO AMTWANGA SADIK MOMBA KWA POINTI
      • Waziri Membe akutana kwa mazungumzo na Wafanyakazi...
      • Mahojiano ya JK na radio ya umoja wa mataifa, New ...
      • J&M Virgo washusha mali mpya
      • Daktari wa Rais Kikwete kupima afya na kuwapa lese...
      • MWENGE WA UHURU WATUA MAKETE
      • Swali la kizushi: Je ni mkono upi unaofaa kuvalia ...
      • No title
      • No title
      • introducing Mchaga na pesa by KiwaStrond ft. Banx
      • bwawa la maini oye! Suarez arudi na kupiga bee kat...
      • HARAMBEE KUCHANGIA CHAMA CHA MAPINDUZI MKOA WA KUS...
      • introducing 'Ni Noma' by Go Getta of the night cra...
      • MAKAMU WA KWANZA WA RAIS WA SERIKALI YA MAPINDUZI ...
      • Ubalozi wetu zambia na wajisiriamali wa Tanzania w...
      • Grace aikaeli Mbowe na mumewe wafariki kwa ajali ...
      • Simba yaibanjua Ruvu JKT 2-0 leo neshno
      • KANISA LA TGMIT LAFANYA IBADA MAALUMU KUIOMBEA AMA...
      • ZUMBA KUKWE AMSHINDA HAMADUU MWALIMU KWA KO RAUNDI...
      • TANZIA: Msiba wa Bi ROSE HENRISCH SANGIWA MATAJI
      • Sherehe za kufunga mafunzo katika kikosi cha 842 ...
      • Benki ya posta Tanzania tawi la Songea yaipiga jek...
      • GLOBAL LANGUAGE NETWORK (GLN) ILIYOFANYIKA WASHING...
      • TAMASHA LA SANAA BAGAMOYO NI KWELI KWAMBA LIMEPOTE...
      • No title
      • Tanzanian Minister of Defence Meets Governor of So...
      • UPANUZI WA BARABARA YA BENDERA TATU HADI KAMATA KU...
      • MISS UTALII TANZANIA KUTANGAZA NYATI WA AJABU NA ...
      • Cheka unenepe
      • WAFANYAKAZI WA IDARA MBALI MBALI ZA SERIKALI WACHU...
      • Kiwanda cha kuzalisha malighafi za kutengeneza Gil...
      • MAMA SALMA KIKWETE APEWA URAIA WA HIARI WA JIMBO L...
      • MKUTANO WA SIKU TATU WA MAOFISA WA JUU WA JESHI LA...
      • NBC YATENGA SIKU MAALUMU KUWASHUKURU WATEJA WAO
      • Serikali yabariki tamasha la Utamaduni Handeni
      • Matukio zaidi ya Mhe. Rais Kikwete alipolihutubia ...
      • ngoma azipendazo ankal
      • chemsha bongo...
      • cassim mganga akitumbuiza kwenye tamasha la fiesta...
Powered by Blogger.

About Me

Unknown
View my complete profile