TANGAZO LA UFADHILI KWA WASANII CHIPUKIZI WA FILAMU NA MUZIKI.
1. Wewe ni msanii chipukizi wa filamu au maigizo ?
2. Wewe ni mwandishi chipukizi wa filamu ?
3. Wewe ni mtayarishaji chipukizi wa filamu ?
4. Wewe ni muimbaji / mwanamuziki chipukizi Unataka kukamilisha ndoto zako lakini haujui pa kuanzia ?
Kama jibu ni ndio basi hii ni habari njema sana kwako.
Taasisi ya RafikiElimu Foundation inapenda kuwatangazia wananchi wote kuwa sasa, tumeanza kutoa ufadhili na udhamini kwa wasanii chipukizi wa filamu, waandishi chipukizi wa filamu, watayarishaji (Producers) chipukizi wa filamu pamoja na waimbaji(wanamuziki ) chipukizi wenye sifa zifuatazo :
1. Awe na kipaji cha kuigiza AU
2. Awe na kipaji cha uandishi wa filamu AU
3. Awe na nia thabiti ya kuwa mtayarishaji wa filamu AU
4. Awe na kipaji cha uimbaji.
5. Awe raia wa Tanzania na mkaazi wa jijini Dar Es salaam.
6. Awe na umri wa kuanzia miaka 14 hadi 55.
UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI
Tuma maombi yako kupitia barua pepe yetu ambayo ni : rafikielimutanzania@gmail.com . Maombi yaelekezwe kwa Mkurugenzi Mtendaji,RafikiElimu Foundation, S.L.P 35967, Dar Es salaam.
AU
Unaweza kuleta maombi yako moja kwa moja katika ofisi zetu. Ofisi zetu zipo katika eneo la CHANGANYIKENI karibu na CHUO CHA TAKWIMU.
Kufika katika ofisi zetu, panda daladala za UBUNGO- CHANGANYIKENI kisha shuka kituo cha TAKWIMU halafu tembea hatua ishirini mbele kisha tazama upande wako wa kulia utaona ofisi imeandikwa RAFIKIELIMU FOUNDATION.
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 30 SEPTEMBA 2013.
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu 0782405936 au 0756606085 Au Tembelea : www.rafikielimu.blogspot.com
Thursday, 19 September 2013
TANGAZO LA UFADHILI KWA WASANII CHIPUKIZI WA MUZIKI NA FILAMU
Posted on 06:57 by Unknown
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment