Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) Reginald Mengi akizungumza katika Mkutano uliofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam baina ya taasisi yake na Wizara ya Nishati na Madini kujadili suala la ushirikishwaji wananchi katika utafutaji na uchimbaji wa gesi asilia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Nchini (TPSF) Godfrey Simbeye akisoma tamko la taasisi hiyo kwa waandishi wa habari baada ya kikao chake na Wizara ya Nishati na Madini hivi karibuni jijini Dar es Salaam kuhusu ushirikishwaji wananchi katika masuala yanayohusu utafutaji na uchimbaji gesi asilia.
Baadhi ya Wakuu wa Idara na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati na Madini wakiwa katika Mkutano baina ya Wizara na Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Mkutano ulikuwa ukijadili suala la ushirikishwaji wananchi katika utafutaji na uchimbaji wa gesi asilia.
Baadhi ya Viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini na wa Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF) mara baada ya mkutano wao hivi karibuni jijini Dar es Salaam kuhusu ushirikishwaji wananchi katika masuala yanayohusu utafutaji na uchimbaji wa gesi asilia. Kutoka Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara, Eliakim Maswi, Mwenyekiti wa TPSF, Reginald Mengi, Mkurugenzi wa Utafutaji, Uzalishaji na Shughuli za Kiufundi kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) Dk. Emma Msaki, na Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye.
0 comments:
Post a Comment