Na Tamimu Adam, Jeshi la Polisi Moshi.
MAAFISA wanadhimu, waasibu pamoja na maafisa mipango wa Jeshi la Polisi wametakiwa kuongeza kasi ya Usimamizi wa rasilimali ndani ya Jeshi la Polisi ili kuboresha utendajikazi wao na kutoa huduma bora kwa Jamii.
Hayo yalisemwa na Naibu katibu MKuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya NChi, Mwamini Maleme Wakati wa ufunguzi wa mkutano wa maafisa wanadhimu, waasibu na maafisa mipango wa mikoa na Vikosi mbalimbali vya Jeshi la Polisi kinachoendelea mkoani Kilimanjaro katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi (MPA).
Mkutano huo hufanyika Kila mwaka ambao una lenga kutathimini hali ya utendaji wa jeshi la polisi na usimamizi Wa rasilimali za Jeshi la Polisi pamoja na kuboresha usalama wa raia na Mali zao ili kupunguza malalamiko na kuongeza kasi ya utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
Aidha, alisema kuwa mkutano huo utawawezesha watendaji wote wa Jeshi la polisi kuweka mipango ya pamoja itakayo saidia kupunguza uhalifu na kuimarisha amani na utulivu nchini ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa sera, mipango na bajeti ya Jeshi la Polisi.
Kwa upande wake, Kamishina wa utawala na rasilimali wa Jeshi la Polisi (CP) Clodwig Mtweve ambaye ndiye Mwenyekiti wa mkutano huo, alisema kuwa mkutano huo utawawezesha watendaji kuboresha mikakati na mipango ya kuimarisha usalama wa raia na Mali zao pamoja na kuzuia ajali barabarani ikiwa ni pamoja na kudumisha nidhamu na maadili ndani ya Jeshi la Polisi.
Alisema kuwa hivi sasa Jeshi hilo linaendelea na mkakati wake wa kufikisha huduma ya usalama hadi ngazi ya familia, mkakati huo unatekelezwa kupitia Mradi wa Askari Tarafa ambao jukumu Lao kubwa ni Kushirikiana na Jamii katika kutatua kero mbalimbali za kiusalaam ndani ya jamii.
Naye Mhasibu mkuu wa Jeshi la polisi Bw. Frank Msaki alitoa shukrani kwa niaba ya ya Jeshi la Polisi na kuwataka wajumbe kutumia mkutano huo Kama fursa ya kuboresha utendaji katika sehemu zao ili kuleta matokeo makubwa.
0 comments:
Post a Comment